Namna wanavyofikiri Wakana Mungu (Atheists) - Sehemu ya pili

Kisai

JF-Expert Member
Apr 6, 2018
27,984
28,102
Abrakadabra na Sarakasi za RICHARD DAWKINS

Katika safari yetu ya kuwathibitishia uwepo wa Mola muumba na vyote vilivyomo kwa lengo la kuwatibu wakana Mungu, niliamua kuanza kudodosa juu ya "Self-Evident Truth" ukweli ambao unajitegemea,ukweli usio hitaji ushahidi ili kuthibitika, ukweli ambao unasimama kwa wenyewe,ukweli ambao upo ndani ya kauli hii "Chochote ambacho unakiona na unacho hisi chenye sifa fulani huonyesha, usanifishwaji wa kitu hicho, sifa ya kitu hicho, msanifu wa kitu hicho, na lengo la msanifu". Ukweli huu huitwa "Self Evident Truth".

Ukweli huu wapo watu walio jaribu kuupinga, lakini jaribio lao likawa ni dhidi yao, kwani waliamua kupingana na maumbile, kupingana na akili, kupingana na uwezo, kukataa sifa za wazi na kupingana na matokeo yatokanayo na milango ya fahamu. Miongoni mwa watu hao ni Richard Dawkins, na haya tunayaona katika kitabu chake kiitwacho "The God Delusion" katika ukurasa wa 212. Anasema yafuatayo :


20200506_204512.jpg

Ukweli ni kwamba ameamua kupingana na akili yake, kupingana na taarifa zitolewazo na milango ya fahamu, akaamua kuruka sarakasi na kucheza na maneno. Kwake yeye anasema viumbe hawajaumbwa, bali kusema viumbe wameumbwa (Kusanifiwa, kubuniwa) ni tokeo la kile alichokisema Charles Darwin, ndio maana ili kuweza kuelewa kwa wepesi utendaji kazi wa Moyo, sharti tu assume ya kuwa Moyo umesanifiwa kwa ajili ya kusukuma damu (to pump Blood), kisha kutokea hapo tuendelee, yaani anacho ona yeye ni kuwa Moyo haujabuniwa/haujasanifiwa bali tuchukulie tu ya kuwa hauja sanifiwa,
Hili linapingana na akili salama, kwani tunauliza huo moyo umekuwaje ukawa moyo, je umejitengeneza au la ?

Lakini vipi kuhusu usanifu wa majengo, mambo ya kiteknolojia,mfumo wa viwanda je uwepo wa vitu hivi huthibitisha nini ? Je ni sawa tukisema ya kuwa tuchukulie tu kwamba vimesanifiwa basi tu, ili tuweze kuvielewa kwa wepesi, wakati tunajua ya kuwa kiuhalisia vimesanifiwa na vinaonyesha uwepo wa msanifu, sifa ya kitu husika na lengo la msanifu ? Sasa vipi hili lisiwepo kwa ulimwengu na vilivyomo, kwani vipo katika utaratibu maridhawa wenye kutegemeana kwa kimoja baada ya kingine na kwa mpangilio maridhawa kabisa,bali una sifa kama ya majengo tuyaonayo ?

Maswali ya kimjadala kwa wakana Mungu.

1. Nini wanaona kwa vitu wavionavyo ? Je vimetokana pasi na chochote au vyenyewe vimejitengeneza ?

2. Je ni ipi nafasi ya "Self-Evident Truth" kwao wao ?

Mjadala uendelee....
 
Back
Top Bottom