Namna nilivyopata mke kupitia facebook na kufunga nae ndoa.

Kijana kijana

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2018
Posts
2,546
Reaction score
2,625
Habari za muda wakuu,kama kichwa kinavosema hapa nipotezi muda naingia kwenye mada.

Kwanza kabisa mke hupatikana popote pale,lakini inategemea unataka mke wa aina gani.lakini pia ikiwa wewe una mwanamke umeonana nae kwenye mtandao basi fuata njia yangu hii huwenda ukafanikiwa kupata mke unayemtaka.

Katika pita pita yangu maeneo ya fb miaka ya nyuma huko nilibahatika kupata friend request ya dada fulani hivi nikamkubalia,lakini ikawa kama sio marafiki kwa sababu huyo dada hakuwa na shobo za kutuma picha wala kuwa kimbelembele cha kuongea sanaa katika post mbali mbali.

Sasa siku zilivozidi kwenda nikawa nazidi kumsoma tu wana mtag katika picha mbali mbali hana habari wakati huo wenzie wakikazana kutuma mapicha yao na likes za kutosha ila yeye hakuna na mpango huo.

Sasa na mimi nikawa nafata swaga zake za kuwa kimya mpaka siku moja niakenda inbox nikamsalimia kwa heshima na stori mbili tatu yakaisha siku hiyo,ila sasa tukawa tunasalimiana kama miezi minne hivi sioni kama ana shobo yoyote yani,stori nianze mimi yeye hana habari,basi nikazidi kujiweka fiti ili aone na mimi sio kama wale wapumbavu,ikapita miezi mitano akawa ameniamini kwa sababu sikuwahi kumtongoza jambo ambalo likafanya aniheshimu na kuanza kufunguka kupiga story mbaali mbali huku tukiwa tumesahau kabisa mambo ya mapenzi.

Kilichonivutia ikapita miezi kama 7 hivi hajawahhi kuniomba vocha kama wadada wengine kujuana juzi virungu kibao,sasa basi yule dada alikuwa anakaa mkoani na mm nakaa mkoa tofauti na yeye,nikaanA kuvutiwa nae na mpaka hapo hakuna ambae alimuomba picha mwenzie,jambo ambalo lilifanya tuzidi kuaminiana.

Basi mpaka kufikia miezi 9 kwa kuwa tuna muda mrefu katika mazungumzo basi mimi nikanote vitu vitatu katika maelezo yake kwa mda huo wa miezi 9.kwa chanza jina lake na la baba yake maarufu,mkoa aliokuepo na mtaa aliekuepo cha tatu nikajua baadhi ya wazee wa pale mtaani kwao kwa sababu kuna baadhi yaa stori akinisimulia hutaja wazee maarufu wa mtaani kwao na mm nikawa na note down hayo majina kwa kujua yatanisaidia mbele ya safari.

Basi nikawa nimejiridhisha kwamba mtoto katulia,hana shobo,sio mpiga virungu,ni mpole ila sijawahi kumuona sura sasa hapo ndo nikawa nimedhamiria kumfanya awe mke wangu,ila sasa mm nilisema nataka nipate mke mwem ambaye nilishazoeana nae kama rafiki angu.huyu binti nimezoeana nae kama rafiki yangu tayari ila jeee nitajuaje kama ni mwemaa au mbaya,kama ananiigizia jee hapa????

Basi nikafunga safari mpaka mkoa aliokuepo(nauli 50000/=) kwa sababu data zote nlikuwa nazo,nikashuka nikaanza kuulizia ule mtaa wakee aisee nilipata shida sana mkoani nikaja kuupata huo mtaa daah niko hoi na ilikuwa mida ya jioni.

Basi nikaanza kumuulizia yule mzee ambae nililipata jina lake kupitia yeye,daah uliza ulizaa weee bahati nzuri nikalipata na nikamuulizia jina la yule baba yake binti baada ya salamu na kujitambulisha.akanambia huyo mzee ana mjua.

Kumbuka:hapo sijawahi kumuona huyu binti na wala binti hajui kama nimefunga safari ya kwenda kwao hivyo huwenda tungepishana pale mtaani tusijuane.

Tunaendelea.: yule mzee nikamuambia kwamba huyo mtu ana mwanaweee anaitwa fulani fulani? Akanambia ndio anaye mwanae.

Nikamuuliza vipi huyo binti mienendo yake hapo mtaani iko vipi? Mzee alikuwa anajua sababu ya kuuliza vile na nikamuambia nilikotoka na nikamuambia huyo mtu simjui kuna ndugu yangu kanituma nije kumuulizia hivyo ni kitendo cha kutuambia ukweli juu ya mwenendo wake.

Mzee akasema huyo binti mtaa mzima wanamjjua ni mtulivu,wazee wake wastaarabu hawana shida,na kama hutoamini mtafute mtu mwingine muulizie.

Mimi nikasema hapa hapa inatosha maana ukimchunguza sana bata humli,madhali watu wa mtaa wanamjua kwa tabia nzuri basi sina haja ya kuchunguza sana mwisho kuangukia koroma.

Sasa baada ya kupata tabia zake nikasema naanza mchakato wa kutaka kuonana nae ili nione kama ataniridhisha baada ya kuniridhisha tabia.

Sasa niliamua kutaka kumjua tabia kabla ya kumuona kwa sababu ya kwamba : mimi lengo langu ilikuwa nipate mke mwema mwenye tabia za kuridhisha, sasa nilihofia huwenda ningemuona kwanza alafu akawa mzuri saaaaaaana nikapagawa then ningeenda kuulizia tabia nikaambiwa mbaya wakati huo nimedata na uzuri wake tayari ndo hapo unakuta mtu anasema tabia tutavumilianaaaa alafu mwisho wa siku mateso tu. Sasa hilo nikataka nilisovu mapemaa.

Lakini nimepata tabiaaa kwanza zikaniridhisha then sasa nikafanya mpango wa kuonana nae sasa.

Basi nilipotoka kwa yule mzee nkarudi sehemu kwa ajili ya mapumziko nikampigia simu yule binti nikamuambia nimepata safari ya kuja mkoani kwenu,vipi naweza kukutembelea? Akasema ndio.

Siku ya tatu yake nikafanya mpango tukapeana namba za simu tukawasiliana na alikuwa akiniamini mno kwa sababu sikuonyesha uhuni wa aina yoyote,nilipomuona kwa kweli ALIKUWA NI BINTI MZURI WA KAWAIDA,MREFU KIASI,MAJI YA KUNDE,NA NIKAMPENDA KWA SABABAU ZIFUATAZO.

1.alikuwa katika stara ya hali ya juu

2.sikutaka mwanamke matawi ya juu akipita sehemu wote wamuangalie(aina hii wanawauwaga presha wanaume)

3.si nilishapata tabia zake kwamba ni njema.

Basi haya yakatosha mimi kujiridhisha kwamba huyu ndiye mke.

Basi tukapiga stori mbili tatu na kuagana.na mimi siku ilofata nikapanda gari kurudi homu.
Nilipofika nikampigia simu kumuambia ya kwamba lengo langu nimuoe kwa sababu tumeshazoeana muda mrefu sana na tumejuana vya kutosha.

Akaniuliza inakuwaje unamwamini mtu wa mitandaoni,ndipo nikampa mkanda mzima ulivokuwa,akahemwaaaaa kwaannzaa alafu akanipa hongera kwamba nipo siriaz na kutafta mke hivyo yeye hakuwa na haja ya kunichunguza sana(mume hachunguzwi)

Basi akakubali na taarifa zikafika kwa wazee wake ikabaki posa tu,tukapamga siku kupeleka posa na mwisho wa siku ikakubaliwa posa yetu na tarehe ya harusi ikapangwa hatimae ndoa ikapita na mpaka hivi leo nipo na mke wangu ambae nilimpata kupitia facebook na tunapendana sana ni zaidi ya miaka miwili na wala sijaona tatizo lolote zaidi ya mapungufu madogo madogo tu ya kibinaadamu.

USHAURI KWA VIJANA

Usikurupuke kuoa tu kabla ya kuchunguza japo kidoooooogo ujue tabia zake,sio umekutana nae disko unatangaza kuoa kwa kuwa ana shepu,utaumia sana kwasababu uzuri unakinaisha wakuu,itafika hatua uzuri wake utauzoea wakati huo tabia mbovu sasa hapo ndo utaanza kusema wanawake wabaya mara vile na hivi na hatimaye ndoa utaona chungu.

Pili ukipata mwanamke anaekupenda saaana na tabia zake njema wewe hata kama hujampenda saaaana kiviile oooaaaa huyooo utadumu nae.

Mwanamke anaekupenda rahisi kumfikisha kileleni,jambo dogo ukimfanyia anaridhika kwa sababu ameshakuweka moyoni,ila asiyekupenda daaaah inahitaji nguvu ya ziada sana.

MWISHO WA MWANZO.
 
Huyo bint kipindi unawasiliana nae inamana hakua na mtu? au kisa ilionyesha userious unataka ndoa akaamua kumtema aliekua nae! ni kweli mke anapatikana kokote! kokote kuna ambao wako serious na magume gume! msafara wa mamba na kenge wapo!
 
Safi Sana mkuu mimi mwenyewe miaka 5 imepita Sasa nilipata mwanamke kupitia face books na Sasa tumeowana na tunaishi vizuri Sana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom