Namna kuelekea kwenye uchumi usio tegemezi kwa taifa Tanzania

Sirmajizo

New Member
Oct 15, 2007
2
0
Heshima kwenu!

Najitokeza kwa mara kwanza kuanzisha mjadala unogusa maslahi ya taifa.

Jana nilikuwa nikimsikiliza Prof. Sospiter Mhongo waziri wa Nishati na Madini (Kipindi Dakika 45 ITV)
Kimsingi ameeleza namna jinsi ambavyo tafiti zilizofanyika kuonekana kwa kiasi kikubwa cha Gas asilia, Makaa ya Mawe, Madini na kadhalika.

Mtizamo wangu ni kwamba twahitaji umakini mkubwa kwenye utekelezaji wa miradi hii, viongozi wenye uzalendo, wataalamu wenye weledi mkubwa na kutoingiliwa kwa namna moja au nyingine na watunga sera/wanasiasa kwenye utekelezaji wa mikakati na mipango ili kufikia malengo.

Hakika watanzania tusifanye makosa tena, kama ambavyo awali tumefanya kwenye madini au taasisi zingine ilivyodhihirisha taifa kutokuwa na maslahi yeyote.
 
Back
Top Bottom