#COVID19 Namna gani unaweza kujumuika na muathirika wa COVID-19 ili asione mnamnyanyapaa?

Huku poli tunaugua tunaambukizana na tunapona wote bila hata kujua. Kwakifupi tunauchukulia kama haupo na kweli umetoroka. Misiba inahudhuriwa na watu 1000 na mnalala pamoja kwenye maturubali. Kwa kifupi corona tumemwonyesha ujasiri mpaka ye ndo akaamza kutukimbia. Zimeni tv na smartphone corona anatembea na mawimbi ya media!!!

Hiyo siyo corona babaa.. unazani marelia au pindupindu iyo eee!! Kwa sasa tuna Delta, omba isikupate mzee.
 
Yeye huyo ameniambia kua maneno ya waswahili kuhusu kuwakwepa wenye covid. Ndio nikamjibu labda kweli maana nami ni mkwepaji mmoja wapo

Aisee 🤣 inaonekana uko care sana hongera, nakushauli endelea kujilinda, na ikiwezekana upate chanjo uwe huru. But don't forget to wear a mask
 
Alikwenda hospital wakampima wakasema hana, ila alikuwa na dalili zote. Ndani ya siku nne alikuwa hoi, mafua,kikohozi na homa plus kukonda na kukongoloka. Sasa hapo atajitenga?
Hospitali ipi hiyo ambayo inapima Corona?Unaelewa utaratibu wa kupima Corona hapa Tanzania?
 
Kaka hapo ofisini kwenu kuna tatizo, inakuwaje mwenzenu anaonesha dalili zote za uviko na bado mko nae mjengoni!? Ofisi ilipaswa kumpa hata siku 7 hadi 14 atulie huko nyumbani. Au tuseme Kazini mko wachache hamna mtu mwingine wa kumpa majukumu yake kuyatekeleza!!?
 
Unyanyapaa ni kitu kibaya sana. Hivyo lazima kuepukwa.

Lakini vipi unapokuwa na mate wako ambae aliugua dalili zote za Uviko na bado anakohoa na kupiga chafya.

Akija kazini mnatakiwa kuishi nae vipi? Maana kilia mtu anaogopa huu ugonjwa.

Kumtenga? Ukimtenga atasema mnafanya unyanyapaa.

Muathirika wa UVIKO anatakiwa kuwa hospitali au kuwa in isolation. Labda ulimaanisha ugonjwa mwingine mkuu?

Hata hivyo uvaaji wa barakoa kwa wote popote panapo mashaka ni muhimu sana:

IMG_20210812_130934_176.jpg
 
Duh! Mimi nilitegemea wagonjwa wengi watakuwa ni makonda na madereva wa Daladala, maana konda mmoja kwa siku anakutana na si chini ya abiria 350, kwa wiki? kwa mwezi? Usisahau smart phone ziko ndani ya daladala.
Wanaousoma ugonjwa ndo wanaopata wasiwasi na ugonjwa
 
Mleta mada naona huijui covid wewe ndio maana unaleta hizo stori sijui za unyanyapaa etc

Ushaambiwa huo ugonjwa hadi sasa hauna tiba, hakuna dawa za kuwaua virusi wa Covid-19...

Hivyo kitu cha kwanza ni lazima kuwe na isolation, sasa kwenye hatua hui kwa vile huijui vizuri Covid naona unaanza leta zile mbwembwe za Kitanzania za kuoneana haya...

Baada ya isolation ndipo mgonjwa au muathirika huudumiwa na watu wataojikinga kwa kinga za viganja vya mikono, pua, macho n.k...
 
Duh! Mimi nilitegemea wagonjwa wengi watakuwa ni makonda na madereva wa Daladala, maana konda mmoja kwa siku anakutana na si chini ya abiria 350, kwa wiki? kwa mwezi? Usisahau smart phone ziko ndani ya daladala.
Kwenye maradhi yoyote huwa kuna hizi hatua pindi mtu anapokutana na vijidudu vya maradhi...

1. Asymptomatic - Kutoonesha dalili zozote za kuugua kabisa, mtu huendelea na shughuli zake kama mtu asiye na maradhi.

2. Mild - Dalili chache kwa kiwango kidogo kinachovumilika

3. Moderate

4. Severe

5. Critical

Hivyo huenda watu wengi wapo kundi nambari 1 na 2 kutegemeana na variant aliyepo Tanzania maana kirusi cha Covid at some point kimeoneaha kulenga kushambulia makundi fulani ya watu, hivyo kutoambukizwa kwa wale makondakta n.k hakuna maana ugonjwa haupo...

Pili, sidhani kama tunawafahamu makondakta wote wanaougua na kufariki sio kwa Corina bali hata maradhi mengine, hivyo kwa kuwa huwa hatuna taarifa ni makondakta wangapi hufariki kwa muda fulani basi hatuwezi jiaminisha kwamba wapo salama...

Endelea kujikinga...
 
Back
Top Bottom