#COVID19 Namna gani unaweza kujumuika na muathirika wa COVID-19 ili asione mnamnyanyapaa?

Muuza Kangala

JF-Expert Member
Jul 21, 2021
1,124
4,162
Unyanyapaa ni kitu kibaya sana. Hivyo lazima kuepukwa.

Lakini vipi unapokuwa na mate wako ambae aliugua dalili zote za Uviko na bado anakohoa na kupiga chafya.

Akija kazini mnatakiwa kuishi nae vipi? Maana kilia mtu anaogopa huu ugonjwa.

Kumtenga? Ukimtenga atasema mnafanya unyanyapaa.
 
Covid sio ukimwi bwana, kupata covid ajabu yake nini, ama aibu yake nini!!!! Ni gonjwa ambalo kuna kupona ama kufa kwa mda mfupi, ukilinganisha na ukimwi gonjwa endelevu adi kufa, tena la aibu/kunyanyapaliwa.
 
Anatakiwa kwenda kufanya PCR TEST,mgonjwa wa corona anatakiwa awekwe quarantine,isolating those believed or feared to be infected,achaneni na issue sijui eti ataona unamyanyapaa,hawa virus ni deadly virus sio issue ya kuoneana eti aibu!

Mwenyewe nashangaa, wakati akitumia dawa tu atapona na ataludi kwenye hali yake yamwanzo au kufa kabisa.
 
Yeye huyo ameniambia kua maneno ya waswahili kuhusu kuwakwepa wenye covid. Ndio nikamjibu labda kweli maana nami ni mkwepaji mmoja wapo
Mwenye covid hatakiwi kuchanganyika na watu,anatakiwa ajiweke quarantine.sasa hapo maneno ya waswahili yanaingiaje? fuata maelekezo ya wataalamu achana na maneno ya wafuasi wa Kibwetere.
 
Mbona tunaupata sana na tunaambukizana na kupona tuu?,mbona mi husband alionyesha dalili zote za covid na tulikua tunalala wote na kukohoa ananikooolea kama kawa na sijaambukizwa kikohozi achilia mbali mafua na alipona kitambo tuu. Kwahyo ndo angeenda kukaa karantini? hofu si ndo ingemmaliza? yani tulichukulia simple na nikawa namkandika ma tangawizi na maji ya malimao na kitunguu maji plus antibayotiks alizopewa hospital. Huyo wa kazini kwako labda kwa sbb sio ndugu yako au mtu kama mume au wtt wako kuwatenga its not easy at all. Ni kumuomba tuu Mungu na kufanya vinavyowezekana
 
Huku poli tunaugua tunaambukizana na tunapona wote bila hata kujua. Kwakifupi tunauchukulia kama haupo na kweli umetoroka. Misiba inahudhuriwa na watu 1000 na mnalala pamoja kwenye maturubali. Kwa kifupi corona tumemwonyesha ujasiri mpaka ye ndo akaamza kutukimbia. Zimeni tv na smartphone corona anatembea na mawimbi ya media!!!
 
Unyanyapaa ni kitu kibaya sana. Hivyo lazima kuepukwa.

Lakini vipi unapokuwa na mate wako ambae aliugua dalili zote za Uviko na bado anakohoa na kupiga chafya.

Akija kazini mnatakiwa kuishi nae vipi? Maana kilia mtu anaogopa huu ugonjwa.

Kumtenga? Ukimtenga atasema mnafanya unyanyapaa.
Study zinaonyesha kuwa mtu anaweza kuumwa kati ya siku 1-3 baada ya kuambukizwa, pia anaweza kuambukiza kati ya siku 7-10.
Kwa hiyo hesabu zako ziwe ndani ya siku hizo katika kuambukizana, Mengine ni ya MUNGU.
Office mate alikuwa na dalili zote, tulikuwa tunakunywa na kula pamoja mpaka alipopoteza kabisa ladha, baada ya siku 4 ladha ikaruidi na kazini alikuwa anakuja kila siku kama kawa. Sasa yuko vizuri anapiga kazi na tunaendelea na ushirika wetu, tunashare chai asubuhi, lunch pamoja mchana, Kila kitu kiko sawa.
 
Huku poli tunaugua tunaambukizana na tunapona wote bila hata kujua. Kwakifupi tunauchukulia kama haupo na kweli umetoroka. Misiba inahudhuriwa na watu 1000 na mnalala pamoja kwenye maturubali. Kwa kifupi corona tumemwonyesha ujasiri mpaka ye ndo akaamza kutukimbia. Zimeni tv na smartphone corona anatembea na mawimbi ya media!!!
Duh! Mimi nilitegemea wagonjwa wengi watakuwa ni makonda na madereva wa Daladala, maana konda mmoja kwa siku anakutana na si chini ya abiria 350, kwa wiki? kwa mwezi? Usisahau smart phone ziko ndani ya daladala.
 
Back
Top Bottom