Moja ya vipindi vigumu apitiavyo mwanadamu, ni kuona mwenzi wake anatoka nje ya ndoa. Iwe mwanamke katoka au mwanaume, haijalishi jinsi, ni wakati mugumu. Wana jf, tutakuwa hatuna maana, kama hatutafarijiana katika nyakati ngumu kama hizi, hasa pale mwenzetu, kwa imani kabisa, anapoamua kutushirikisha magumu kama haya. Hili si la mzaha, kama kweli mwenzetu yamekupata. Kwanza kabisa nakupa pole.
Zaidi ya hapo, naomba nikutie moyo kuwa magumu hayana budi kutupata wanadamu, kwa kuwa taabu zipo ili zitupate.
Imani za kidini zinatofautiana, kwani kwa uislamu, mkataba wao ni wa wake wengi, ila kwa wakristo, mkataba wao ni wa mke mmoja - mme mmoja. Inapotokea mmoja akakiuka, basi hapo huwa anavunja haki ya mwenzake na inauma sana.
Iwapo yamekupata, basi, mwombe Mungu, akupe moyo wa subira, akujalie umsamehe makosa yake, kwani kujitenga naye si dawa. Mungu akujalie hayo.