Namchukia mzee wangu!

Wewe ndo mjinga wa mwisho anahasara alokuuzaa
 
Yani mzee mzima wa miaka 33 umeshindwa kumjengea nyumba Baba ako.

Unakuja kutupigia kelele za ku fight (Eti bado una fight?)

Unatuaibisha
 
Nilitegemea kuona labda mzee ni mnyanyasaji, mtesaji lakini maskini baba watu hajaweka sakafu tu.

Kweli kuzaa unaweza zaa kizaazaa..watoto hatuna shukrani
Yaanj kamdharau mzee kisa sakafu .

Hizi mzee wake angeaamua kumtupa chooni enzi hizi angesemaje
 
Utakuwa una matatizo ya akili, mzee wako labda angejenga nyinyi msingepata fursa ya kusoma, labda pia alitumia pesa nyingi kuwapa elimu akijua kuwa nanyi mkifanikiwa mtakuja kulipa fadhila kwa kumjengea nyumba mzee wenu, nazani kwa umri wako tayari wewe ni mtu mzima je mipango yako yote huwa una mshirikisha mke wako? Na je huyo mama yako pamoja na nyie mlikuwa mnashirikisha mzee wenu mipango yenu? Nakushauri nenda kamwombe baba yako msamaha kabla laana haijakukuta, baba yako alipambana mpaka leo umeota ndevu adi mkun%& leo unamwona fala.
 
mwanangu e, we bado mvulana! ukikua utayajua mengi! so tuseme point kubwa ni kitendo cha mzee kutokusakafia nyumba, na unaaibika unavyowaleta madem zako!! je kuna tofauti gani wewe na mtu aliemkana mama yake kisa mama yake kimwonekano hayupo sawa!
.
.
acha mambo ya kipuuzi naukatubu kwa Mungu wako, tafuta hela wewe ndo uje uonyeshe nyumba inapaswa kuweje, unaanza kumkosoa mwanaume aliekuleta duniani? wewe mpka sasahivi umefanya nini??
.
.
yaani kijana mzima unamchukia bana yako kisa hajasakafia nyumba? Je kama yeye anapenda nyumba ikiwa hivyo yes wapo ambao wanapenda udongo ule ukipigwa maji ukafagiliwa vizuri,
.
.
acha kujilinganisha na watu, umetokea katika familia yenye uwezo wa kawaida, pambana uje kuwa na maisha mazuri! af mtoto wa kiume unawapelekaje madem nyumbani?
.
.
serious kabisa unampeleka dem kwenu eti mnatembeleana, nachojua wanaume ndo tunapelekana makwetu, tunakula pamoja nk. mwanaume mwenzio hawezi zungumzia hali ya kwenu hata kama kupoje, hao madem tafta namna muwe mnakutana out, kwa miadi!!
.
.
inshot nakuona unajiaminisha sana hapo ni kwako pia, HAPO SI KWAKO, NA UMRI WA KUKAA HAPO UMEISHA TOKA KAJENGE NYUMBA YAKO YENYE SAKAFU, usimchoshe mzee!!
.
.
na uwe unaenda kumwona, na hio nyumba ukaiweke sakafu otherwise unatafuta laana ya kufa kifo kibaya sana!! BABA HAKOSEI,
 
Mtoto asiye na shukrani ni mzigo kwa wazazi wake. Weka wewe sakafu na ubadili muonekano wa nyumbani kwenu,si unao uwezo sasa?. Unangoja nn?
 
Labda hawezi kufanya kila kitu..na ameamua kufanya vile anavyoona vinampa furaha. Mfano kama hivyo kawasomesha na kuwapa mahitaji yenu yote.

Si mumrekebishie hapo home, au hataki?
Kusomesha ni kazi sana halafu unakuta watoto wanne au watatu wamefuatana,mshahara wote unakuwa ada na matumizi ya nyumbani pamoja na kukopa juu.

Halafu wanamaliza shule mzee astaafu au aachishwe kazi na watoto bado watoto wapo nyumbani hata matumizi na kula wanamtegemea .

Then anakuja mtu anasema kwanini hujajenga nyumba ya maana jibu ni kwamba ondoka kama huwezi kukaa,mzazi kahangaika yeye anawaza atamletaje dem nyumba ya vumbi?
 
kinacho kusumbua wewe ni kushindwa kuosha kwa marafiki zako na mademu zako kuwa mna nyumba sio nzuri, hiyo ni sababu ya kijinga sana, maana mzee wako amejitahidi kuwalipia elimu kwa maisha yenu ndo muhimu
 
Mkuu, kumbuka una miaka 33 sasa. Amka usingizini...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…