mwali wa giningi
Member
- Nov 14, 2013
- 67
- 42
Viamba vya upishi
1. Manda za sambusa kiachi 40 -50
2. Mafuta ya kukaangia lita moja
3. Nyama ya kuku iliyosagwa kilo moja
4. Kitunguu saumu na tangawizi iliyosagwa kijiko kimoja
5. Pilipili mbichi iliyosagwa kiasi kama utapendelea
6. Pilipili manga kijiko kikoja cha mezani
7. Bizari nyembamba ya unga kijiko kimoja cha chai
8. Bizari ya mchuzi kijiko kimoja cha chai
9. Juisi ya ndimu kijiko kimoja cha mezani
10. Mbogamboga mchanganyiko kikombe kimoja cha chai
11. Chumvi kiasi
12. Vitunguu maji vilivyokatwakatwa kikombe kimoja
13. Kotmiri iliyokatwa vijiko viwili
Jinsi ya kupika
1. Pika nyama ya kuku ya kusagwa kwa kutia chumvi, kitunguu saumu na tangawizi, pilipili, ndimu na bizari zote.
2. Ikikaribia kuiva tia mboga za mchanganyiko. Changanya vizuri kisha ipua na weka pembeni halafu weka vitunguu na kotmiri. Chukua manda zako na weka mchanganyiko wa nyama na kisha funga.
3. Baada ya hapo weka mafuta jikoni na yakishapata moto anza kuweka sambusa zako jikoni na kanga hadi ziwe za hudhurungi. Ipua na weka pembeni.
Sambusa zako zitakuwa tayari kwa kuliwa. Unaweza kula sambusa na kinywaji cha aina yeyote na kufurahia ladha yake.