Namba za simu

JAYJAY

JF-Expert Member
Oct 31, 2008
7,510
7,534
naomba kuuliza hivi namba za simu kwanini hazitengenezwi kwa mtindo wa mtiririko(series) kama wa mfano namba za magari.maana sidhani kuwa Tanzania kuna wateja wengi wa simu kiasi cha kila mara mitandao kuanzisha code mpya mfano 075XXXXXXX na 076XXXXXXX kwa vodacom.kwa mtiririko XXXXXXXX inaweza kuwa na mpaka tarakimu 9999999 na hao ni wateja wengi ambao sidhani kama kuna mtandao wenye wateja wengi kiasi hicho.
 
We need to Create Future Today!

Kuna siku TZ kutakuwa na Mobile subscriber 40mil (probably in ten years - 2019) kama ambavyo kulikuwa na 0 subscriber in 12 years ago!
 
heheh hii kali.

Mchezo wa zain kuuza namba ambazo wateja wameshindwa kumaintain ni kero sana. Mimi nimenunua namba last week najuuuuta kupewa!!!! kuna mtu ananitukana vibaya mno. sasa nikipata muda nairudisha kule wakae nao wao maana siiwezi.

inawezekana wanatoa code mpya kutokana na u dormant wa number za watu wao wanafikiri eti zina wateja.
 
Telcoms produces a lot of SIM cards everyday ... and recycle the number after a certain period of inactivity ... that's why that happens.

Lakini pia watanzania tabia yetu inachangia katika hili, watu wengi sana hununu line kwa matumizi ya muda mfupi, then kuitupa. Hili linasababisha namba kwenda kwa kasi sana kufikia kumaliza code block.

Achilia mbali wale mafisadi wanaotoa order ya namba nzuri mfano 07XX 111222. Hao nao pia ni kichocheo cha kumaliza code block haraka ili wauze special numbers kwenye next code block.
 
Muanzilishi wa Thread hii umenifurahisha kuwa wewe ni miongoni mwa watanzania wachache sana ambao wanafahamu na kutumia code za simu kama zinavyotakiwa:
071 xxx xxxx - tigo
073 xxx xxxx - ttcl
075 xxx xxxx - vodacom
076 xxx xxxx - ''
077 xxx xxxx - zantel

... na kadhalika na sio 0715 xxx xxx, 0716 xxx xxx, 0754 xxx xxx na kadhalika kama tulivyozoeshwa kusoma na hizi kampuni za simu!! Code za namba za simu ni tarakimu tatu tu jamani na zinazofuata zote ni namba ya mteja! Unapoulizwa nambayako seme "Namba yangu ni Sifuri Saba Moja, na kadhalika.......!!! na sio "Sifuri Saba Moja Tano, ....!!!!!
 
Back
Top Bottom