Namba ya Simu ya Zitto katika TAMKO kuhusu kesi ya Lwakatare

Status
Not open for further replies.
Kuweka namba ya Zitto ni sawa tu na kusema afande mshuti unapofanya ugaidi ili kujenga hisia kuwa aliyetenda hilo tendo ni fulani.

Ndege mjanja hunasa kwenye tundu bovu, atawafuata masalia wenzake. Kuna kitu ambacho si wazi kwa mwanasiasa kama Zitto asitishe kugombea ubunge kule kigoma kupitia Chadema, huenda ana alikuwa na mpango wa dakika za mwisho kuitifua Chadema kwa kuhamia chama kingine cha siasa hasa NCCR Mageuzi. Haya yalishasemwa hapa.
 
Chadema hawana protocol,
Kila mtu ni msemaji mkuu wa chama, bora tu awe mchaga au ana cheo fulani ndani ya chama. Hata yule kijana anayetembeaga na sumu mfukoni ni msemaji pia
 

inafahamika Zitto mn
 
Tumevua gwanda tukavaa gamba baada ya ubabaishaji ndanimwe.
Ila still tumekunywa supu ya maagano na zito hakuna wa kumtoa moyoni mwetu haka akifa/kuuliwa kesho simply for what he did for Tanzanian's.

GAMBA MTALIVUA atakapogombea LOWASA mkristo!
 
Ooh! Masikini Zitto my be mwana siasa hodali na mzalendo anaye fanya kazi ya kizalendo chini ya mwavuli wa wafanya biashara
why always you?
Thinking loudry?
Mbona hajawahi guswa au tajwa Mbowe au Dr Slaa je hawa ni wasafi 100%?? Naamini ipo siku utachoka na utaamua kuwachia ila historia itakukumbuka (Poor blind Chadema wapo wengi hata hawawezi kupima hoja ila wanahalikia conclusion hawapimi wala hawajisumbui kufikilia wanakuchukia bila sababu ila sababu unazijua)

ushauli wangu:

siasa sio mama yako au baba yako au Mungu wako ila pigana kwa sababu bado nia unayo ya kuwatumikia watanzania!
 
Chadema hawana protocol,
Kila mtu ni msemaji mkuu wa chama, bora tu awe mchaga au ana cheo fulani ndani ya chama. Hata yule kijana anayetembeaga na sumu mfukoni ni msemaji pia

Kwa hiyo na wewe ni m-k-w-e-r-e!! maana unatoa matamko ya CCM kila kukicha!.. After all - Shehe ILUNGA atakamatwa lini? au mpaka mapadri waishe?!
 
Kuna mtu kasema amepiga M Pesa na kuthibitisha kuwa namba hiyo bado iko chini ya jina la Zitto. June 2012 mpaka sasa ni zaidi ya miezi 10. Hivi mtu unapoacha kutumia simu inachukua muda gani kwa kampuni ya simu kubadilisha jina la umiliki?


Wewe pia waweza kufannya hii Investigative Technique ya elementary kabisa. Kuna njia mbili. Moja, unataka kujulikana unainvestigate. Hapa utamtumia target kiasi cha pesa ukweli na utapata jina. Lakini kuna njia ya pili ambayo ni discreet.

Fanya Hivi: Ingia kwenye system ya kutuma hela kwa M-PESA.

System ikija, weka namba hii: 255756809535; Ikiuliza unataka kuweka kiasi gani, weka Pesa yoyote kubwa kuliko uliyonayo--say 5,000,000. Itakuletea prompt kukutahadharisha unakaribia kumtumia Zitto Zuberi Tsh 5 million. Abort operation. Ushamjua nani mwenye iyo namba. Upo? Na jina la Zotto Zuberi litakuja.

Kuna kauongo fulani hapa! Try it....
 
Ila nadhani ametoa uhuru kwa Voda kurelease activities za number hiyo kwa takriban mwaka. Kwa hiyo hapo ndiyo labda tungejua nini kilifanyika.

Pili, usipende kuchukulia mambo kirahisi .. hata mimi kuli huku nisiye na elimu nikipewa ukuu wa TISS, huwezi kujua number yangu na nikiwasiliana na wewe nitatumia satelite ... hiyo hata bongo ipo kama hujui.
 
Zitto naona kama kuleta tamko hapa JF umekurupuka ungeanza huko voda sababu namba imesajiliwa kihalali kwa jina lako ni kiasi cha wewe kwenda kuomba details za hiyo namba yako kwa manufaa ya chama chako, alafu ulitakiwa uje hapa JF utuambie jamani hii namba nimeitumia mwisho June/Jully kuanzia hapo nimekuta ina mawasiliano na usajili haujabadilishwa. Alafu uwashtaki Voda kwa kuiuza namba yako ikiwa na jina lako bila kulifuta, hapo wenye akili tungekuelewa.

Na pia kama Chip imekuwa swapped inaonekana kwenye details na mpaka center walio swap hiyo namba, unanambia kuna asiyemjua Zitto Kabwe mpaka akampa mtu mwingine chip? Labda umepitiwa fanya hilo kesho utuleteee feedback nasi tuanze kujadili kuanzia hapo
 
Last edited by a moderator:
unaandika kama huna akili....ile video inamuonyesha nani akipanga mauwaji na mateso....kwa hiyo kwenu msaki si kitu ndio mana mnaona auwawe? Zitto hana lake chadema anajilazimishia tu, namshangaa kweli


We jamaa..
 

dini! ......
 
Halafu wewe Froida ulisema unaenda kulala, lakini naona hata kulala umeahirisha ili tu uharibu mjadala uliokusudiwa.

Haifai namna hiyo...
Nakunywa bia nakuambia umekuja vibaya kuliko kawaida huwezi kuikana namba yako ambayo iko live kwenye businecard,halafu ukamtetea msaky in the expense of Lwakatere umeclear doubt za watu wengi sana kwamba wewe unahusika kuvuruga chama lakini mimi nasema why an inteligebt man like you where you went wrong and it is too late to retify hili la kujitetea hapa ni vi arrogance kibao ni vipropaganda vinacement ukweli you are caught in the circle i feel sorry for you hill halikuachi umeadhirika sana
 
Namba zote zilikuwemo humu thread ilipoanzishwa baadae ndio wakazitoa na kuweka XXX. I guess walioona watakuwa labda wame copy paste yote ilivyokuwa.

Nakumbuka nilishangaa namba zao kuwa nje nje nikasema mmh mambo hayo, maana duh hakikufichwa kitu. Ila as sina chama sikusema as hayanihusu hizi drama zimezidi nasubiri majibua pia.
 
Nadhani kama Taifa
tunahitaji kutenegeneza tuzo ya mwanasiasa mvumilivu na Zitto awe mtu wa
kwanza kupewa tuzo hiyo.

Mwanasiasa mvumilivu kama Zitto bado hajatokea Tanzania. Uvumilivu wa
Zitto unaweza kuwa hazina kubwa kwa taifa...
mkuu mi nadhani hata wewe una moyo mkuu, una uvumilivu sana kutetea chama kama ccm kinachaohusishwa na ugaidi kwa watu wake chenyewe unahitaji uwe na moyo wa mwendawazimu
 
Jamani haya ni matokeo ya uchunguzi uliofanyika kutoka kwenye rekodi ya mawasiliano ya simu.

Kuna mengi nimejifunza humu kutokana na misimamo ya baadhi ya members ambao daima huiombea mabaya Chadema.
 
Siasa za kijinga hizi. Hoja zimewaishia watu, wanaishiakuchafua majina!!!

Binafsi sioni hoja ya kumchafua mtu, hata mimi kama wana mashaka kuhusika simu yangu nitaruhusu ichunguzwe. Anaogopa nini hadi kutoka mishipa? Kama namba hiyo haijahusika anawasiwasi wa nini?
 

Kuna nyakati huwa natatizwa na busara zako Mheshimiwa Zitto.

Tamko limetolewa na Mabere Marando na limewekwa JF kama lilivyowekwa kwenye vyombo vingine mbalimbali vya habari. Kwa vile Marando ni kiongozi mwenzio huko Chadema, kwanini usingetumia busara za kumuuliza kiungwana tu badala ya kujenga picha kuwa kuna uwezekano wa hujuma dhidi yako?

What if namba unayozungumzia ambayo kwa sasa huitumii inatumiwa na TISS? What if namba hiyo imenukuliwa kimakosa? Nadhani majibu ya maswali hayo ungeweza kuyapata kirahisi kutoka kwa Marando kuliko hapa JF (ambako sina hakika kama Marando ni mwanachama).

Halafu, kwa upande mmoja unataka mahakama iachiwe kushughulikia suala hili ili sio tu ukweli ujulikane bali pia haki itendeke. Lakini wakati huohuo, tayari unatoa hukumu kuwa Msaki ni victim. Ni kwa sababu ni rafiki yako au kuna unayoyajua nyuma ya pazia lakini hutaki kuyaweka hadharani?

Mwisho, ninaona hiyo kauli ya "Mtu yeyote anayetaka kutumia urafiki wangu na Dennis Msacky kutaka kujifurahisha kisiasa ajue kuwa furaha yake hiyo itakuwa ni ya muda mfupi sana maana ukweli ukidhihiri atapata aibu kubwa sana" ni kama utoto wa kisiasa/kukimbia kivuli chako mwenyewe. Naamini sote hatujui ukweli katika suala hili, sasa sijui mwenzetu umekuwa mrithi wa Sheikh Yahya kiasi kwamba tayari unafahamu kuwa ukweli ukidhihiri flani atapata aibu kubwa sana.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…