Namba ngeni imenitumia hela

Namba ngeni imenitumia hela

ErickjrJunior

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2015
Posts
328
Reaction score
78
Wandugu juzi mchana kuna namba imetuma pesa kwenye airtemoney yangu, imeanza kutumwa shs.1,00000, kisha kma baada ya dk 1 ikatumwa shs.50,000.

Mtumiaji simfahamu ni namba ngeni kwangu, nikajua moja kwa moja amekosea namba.

Mikatulia ningoje anipgie aanzee kujielezea jinsi alivyokosea na kutaka nimrudishie hizo pesa.

Wandugu ilikua mida ya saa tisa mchana mpka sasa hiyo namba aijanitafuta kwa vyovyote mpka sasa!

Na pesa zote bado ninazo kwenye airtel money, sasa sielewi imekuaje hi?

Nimejaribu kuiifatilia namba iliotuma pesa nimegundua sina uhusiano nayo kwa vyovyote sielew maana yake wakuu.
 
Duh,mkuu embu itume kwangu wakati unaendelea kusubiri.
 
Tuma kwangu niangalie kama pesa hizo sio bandia, manake siku hizi noti bandia zimekuwa nyingi mtaani!
 
RUDISHA kwa mwenyewe, watu wa Mombasa wana tabia hizo sana. Wanatuma hela wakishajua umeila na huwezi kuirudisha ndio wanakuuliza na kuomba urudishe hela yao
 
RUDISHA kwa mwenyewe, watu wa Mombasa wana tabia hizo sana. Wanatuma hela wakishajua umeila na huwezi kuirudisha ndio wanakuuliza na kuomba urudishe hela yao

Shikamoo JF
 
erickjunior Karibu JF sitaki kuamini Kama hujui utaratibu wa kufuata kwenye ishu Kama hiyo.. Iweke wazi hiyo number tukusaidie kumtrace mwenyewe la sivyo hii yaweza kuwa story ya kutunga
 
Mi mwenyewe jana nimetumiwa Tsh. 58,000 na Mpesa faida.

Sasa sijui Mpesa nao wanatoa mafao siku hizi?
 
acha mambo ya ajabu mkuu yani utulie mpaka utafutwe...we mpigie huyo aliyekutumia umuulize...uungwana ni kitu kizuri sana....huwezi jua labda ye huko hajajua kama kakosea
 
Bahati zingine acha tu, mbona kwetu haziji hizo? Wengine toka tumejiunga na huduma za Mobile Money hatuja pata bahati kama hizo.
TUNA NYOTA YA KUNGUNI.
 
Mungu hulipa yale huyatendayo kwa wengine,mtafute mwenye namba kisha mrudishie,kama Mungu alipanga iwe yako,itakuwa tu.cha msingi onyesha jitiada za kumtafuta mtumaji.
 
ndugu rudisha tu maana huwezi jua pengne alikuwa anatuma gharama za mgonjwa au vinginevyo, uungwana ni vitendo
 
RUDISHA kwa mwenyewe, watu wa Mombasa wana tabia hizo sana. Wanatuma hela wakishajua umeila na huwezi kuirudisha ndio wanakuuliza na kuomba urudishe hela yao
Nilimtext akujibu, nikapga apokei, mara aipatikani.
 
Kama hajakupigia ina maana hajagundua kuwa kakosea.no
Kuwa muungwana umpigie
Nimemtext akujibu, nikapga apokei nikarudia apatikani. sijamchek tena. kuna best yangu ameng'ang'ania niitoe kma siwez niitoe nimpe.
 
acha mambo ya ajabu mkuu yani utulie mpaka utafutwe...we mpigie huyo aliyekutumia umuulize...uungwana ni kitu kizuri sana....huwezi jua labda ye huko hajajua kama kakosea
Nishampgia akupokea na nilirudia akupatikana.
 
Back
Top Bottom