Namba 40 Imebeba Ujumbe Mzito wa Kihistoria

Namba 40 Imebeba Ujumbe Mzito wa Kihistoria

John Achila Mukumwa

Senior Member
Joined
Jan 4, 2024
Posts
111
Reaction score
214
Namba 40 Imebeba Ujumbe Mzito wa Kihistoria

Katika Biblia namba 40 ni alama yenye kumaanisha kipindi cha wakati mgumu. Ni wakati wa maumivu, kukata tamaa ya maisha, masumbufu na changamoto mbalimbali na maisha ulimwenguni.

Kwa mfano: wakati wa Nabii Nuhu mvua ilinyesha kwa siku 40. Haukuwa wakati mwepesi. Ulikuwa wakati wa misiba mikubwa, kwani ingawa Nuhu tu alikuwa ameokolewa na familia yake, lakini ni u wazi kuwa alikuwa na huzuni kubwa kufiwa na majirani zake, ndugu na jamaa, ambao huenda hawakutaka kusikiliza maonyo. Hivyo, kimsingi ulikuwa wakati wa majaribu.

Wana wa Israel nao walipita katika jangwa refu kubwa lenye kutisha na kukatisha tamaa, kwani kadiri walivyokuwa wakisonga mbele matumaini ya uhai yalikuwa yakipotea. Ulikuwa ni wakati mgumu kiasi ambacho kwa baadhi, hata uhuru wa kutoka Misri ulionekana kama kwamba hauna maana. Waliteseka na kupoteza matumaini. Jangwa refu kutoka Misri hata kufika Israel liliwagharibu safari ya mapito ya miaka 40.

Naye Masihi Mkuu Yesu Kristo wa Nazareth kabla ya kuanza kuwahudumia watu aliongozwa na Roho wa Mungu kuelekea nyikani ili kujaribiwa akiwa amefunga kwa siku 40.

Namba 40 imekuwa ikitumika pia kwa maeneo mbalimbali duniani na inakubalika kama namba maalum na wakati wote huo ikimaanisha kipindi fulani kigumu cha kupitia majaribu hata kama kipindi hicho siyo lazima kihesabike kama siku 40 lakini ni kipindi fulani cha mapito na changamoto.

Namba 40 Kibiblia ilimaanisha pia vipindi vya kunyenyekea na kuonewa au kutokuwa na uhuru. Namba 40 humaanisha nyakati za kusubiri au subira. Kwa msingi huo 40 humaanisha subira, uvumilivu, mapito, mateso mitihani, maombolezo, hukumu na furaha au kustarehe.

Mifano ya matukio ya kihistoria kuhusiana na namba 40:
1. Kuhusiana na Biblia

1. Mvua ya gharika ilinyesha juu ya nchi, siku 40 mchana na usiku (Mwanzo 7:12).
2. Bwana akamwambia Abramu, ujue hakika ya kwamba uzao wako utakuwa mgeni katika nchi isiyo yake, watawatumikia watu wale, nao watateswa muda wa miaka 400 (Mwanzo 15:13).
3. Musa alikaa miaka 40 katika nyumba ya Farao, Misri, akifurahia maisha ya anasa kabla ya kuamua kwenda kuwaokoa ndugu zake Waisraeli (Matendo 7:23).
4. Baada ya Musa kumuua Mmisri, alikimbilia Midiani, ambako alikaa miaka 40 jangwani akiwa akichunga kondoo (Matendo 7:30).
5. Musa alikuwa kwenye Mlima wa Sinai kwa muda wa siku 40 (Kutoka 24:18).
6. Sheria ilifafanua idadi ya viboko ambavyo mtu angeweza kupokea kwa kutenda uhalifu, ambayo ilikuwa fimbo 40 (Kumb 25:3).
7. Siku 40 Musa alikuwa mlimani akipokea sheria ya Mungu kwa watu wake (Kutoka 24:18).
8. Suku 40 Musa alikuwa mlimani akiwaombea watu wake baada ya kuwakuta wakiabudu sanamu ya ndama wa dhahabu (Kumb 9:18, 25).
9. Kwa miaka miaka 40 akisafiri nyikani, Musa aliishi kama kiongozi wa Israel kuwapeleka Kanaani, hadi alipofariki katika mlima Nebo kabla ya kuingia Kanaani (Kumb 8:2-5, Zaburi 95:10, Matendo 13:18).
10. Wapelelezi wa Israeli walitumia siku 40 kuichunguza Kanaani (Hesabu 13:25; 14:34).
11. Eliya alipokimbia kutoka Yezebeli, alisafiri siku 40 hadi Mlima. Horebu (1Wafalme 19: 8).
12. Goliathi alidhihaki jeshi la Sauli kwa siku 40 kabla ya Daudi kufika na kumuua (1Samweli 17:16).
13. Wakati wa utawala wa Eli, Wafilisti waliwaonea Israel kwa miaka 40 (1Samuel 4:18).
14. Wakati wa utawala wa Sauli, Wafilisti waliendelea kuwasumbua Israel kwa miaka 40 (Matendo 13:21).
15. Kabla ya ukombozi wa Samsoni, Israeli iliitumikia Wafilisti kwa miaka 40 (Waamuzi 13:1).
16. Kwa siku 40 mji wa Ninawi ulipaswa kutubu kwa mahubiri ya Yona kabla ya hukumu (Yona 3:4).
17. Kwa siku 40 Ezekiel alilalia upande wa kulia akitabiri miaka 40 ya taabu ya Yuda (Ezekiel 4:6).
18. Kwa siku 40 Yesu alijaribiwa nyikani na Ibilisi akiwa amefunga (Mathayo 4:2).
19. Wale Yesu aliowadhihirishia nafsi yake, kwa dalili nyingi, baada ya kuteswa kwake, ya kwamba yu hai, aliwatokea muda wa siku 40, na kuyanena mambo yaliyouhusu ufalme wa Mungu (Matendo 1:3).
20. Biblia iliandikwa na watu 40.

2. Kuhusiana na matukio mengine

1. Watu wakifiwa, humaliza msiba kwa kuondoa matanga baada ya siku 40
2. Mtoto mchanga hutolewa nje baada ya siku 40
3. Siku za mwizi ni 40

Hivyo, namba 40 imekuwa ikitumika kwa maeneo mbalimbali duniani na inakubalika kama namba maalum na wakati wote huo ikimaanisha kipindi fulani kigumu cha kupitia majaribu hata kama kipindi hicho siyo lazima kihesabike kama siku 40 lakini ni kipindi fulani cha mapito na changamoto.

Namba 40 katika kibilia inaonekana kuashiria kukamilishwa na kutimizwa kwa kusudi la Mungu.

Katika Biblia, namba 40 imetajwa mara 146 na mara zote hizo imeunganishwa na masuala ya majaribu, mapito na muda fulani usiofahamika wa kipindi cha mapito au mateso.

Biblia inaonekana kutumia namba 40 ili kusisitiza ukweli wa kiroho, lakini hakuna mahali katika Biblia ambapo inalenga maana yoyote maalum katika namba hiyo.

Namba 40 inatumika pia kwa maana mbalimbali kwa matukio mbalimbali ya kijamii.
 
Umri wa chini (minimum age) wa mtu anayetaka kugombea urais wa JMT ni miaka 40
 
Katika numerolojia namba 40 ni sawa na namba nne (4) namba inayobeba uimara au uthabiti wa kitu wamombo wanaita "stable"
 
Back
Top Bottom