Leo nimekuwa nawaza tu kipindi najiandaa kwenda kulipa bill zangu. Jana wakati naangalia mechi ya spurs na manutd jamaa wa DSTV nao wamekata. Nikaanza kujiuliza kipi hasa kinadeserve kulipiwa haraka dstv au umeme? jibu rahisi ni umeme kwani bila umeme kila kitu hamna nyumbani.
Swali ambalo lilinijia haraka tena ni kwanini napata shida kulipia umeme 30,000/= wakati unafanya mengi kwangu and yet nafurahia kulipa dstv 135,000/??
Pia nikawaza nawalipia watoto wangu ada ya primary grade 1 and grade 3 each 1,750,000/= but naumia pale shule ya msingi ya hapa kwetu wanapoomba mchango wa 20,000/=. nikawaza hivi kama wazazi tunaowasomesha watoto hizi shule za kukariri na kufaulishwa kimagumashi tukiunganisha uwezo wetu tukazichangia shule za public kweli hazitafanikisha malengo ambapo tutatoa mchango pia kwa watoto wa wenzetu wenye uchumi duni?. Nawajua wazazi wenzangu wengi tu hapa kwetu ambao tunajifanya wajanja kuwapeleka watoto mbali kumbe tunaliwa pesa nyingi tu.
Jamani nawaombeni tuweke kipengele kwenye katiba kinachomlazimisha mfanyakazi, mtawala, au mwanasiasa ambaye ni miongoni mwa wasimamaizi wa huduma za jamii katika eneo fulani alazimike naye watoto wake na yeye mwenyewe kutumia hizo huduma. Mfano nikosa mwalimu wa shule x kupeleka watoto wake shule y. diwani , mbunge, nk walazimie kuwasomesha watoto wao shule za kata kama wengine kwani haiingii akilini waziri wa elimu anapeleka watoto private schools au special schools. pia dactari na wengineo. ukianzisha sumu nawe uile.
Jamani ni wazo tu!!