Nalia na bunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nalia na bunge

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kitagya, Mar 14, 2011.

 1. K

  Kitagya New Member

  #1
  Mar 14, 2011
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Napendekeza mishahara na marupurupu ya wabunge viangaliwe upya kwani vinatengeneza tofauti kubwa kati ya wabunge na wananchi wanaowakilishwa. Usibishe. Tunawaona wabunge wanavyotesa mitaani: migari ya nguvu, hoteli wanazofikia, magari wanayowanunulia marafiki, na orodha inaendelea. Mbele ya safari haya matabaka ya waheshimiwa na wanaoheshimu yataleta uhasama ambao utazidi kuhatarisha amani.

  Ubunge imekuwa njia ya kujitajirisha na wataalamu wetu wengi wanaziacha kazi walizozisomea na kuingia bungeni wakifanya kazi ya kulizomea kundi fulani la wabunge na kupayuka "imepita hiyo!". Hii inapunguza tija na hivyo kuzuia ukuaji wa uchumi.

  Kikao kilichopita tumeshuhudia waheshimiwa wetu wakizomeana, wakifanya mipasho, na kushabikia vyama vyao badala ya kujadili masuala yenye masilahi kwa wananchi. hakika kazi iliyofanyika katika kikao hicho haihalalishi malipo waliyolipwa waheshimiwa wetu. wako wengi mno, halafu.Kikao kile kimeliondolea bunge mvuto.
   
Loading...