Nakutafuta Annrosse nikuone mara ya mwisho

Nakutafuta Annrosse nikuone mara ya mwisho

Jembebutu

Member
Joined
Feb 14, 2017
Posts
88
Reaction score
226
Nakutafuta Annrosse. Ni wewe tulikua tukiongea kwenye simu zamani sana. Ilikua miaka ya 2004. Ulikua ni ule msimu wa simu za bure Zantel tukiwa bado watoto Annrosse. Kuna siku nilikosea namba ukapokea wewe. Nilichukua muda kidogo nikakupigia tena kukuomba urafiki. Ulisita sana mwanzo ila sikukata tamaa kutokana na uzuri wa sauti yako, Hekima na majibu yako vilinipa homa.

Sikukata tamaa Annrosse nilikusisitizia sana. Katika maongezi tuliongea mengi kama marafiki lakini nilikua najifunza mengi kwako na kuzingundua weakness zako ili kuukonga moyo wako.

Hakika sijawahi hata kuiona sura yako ila frankly speaking nilikupenda sana Annrosse na niliamini ipo siku nitakuona. Nakumbuka usiku mmoja tuliongea mpaka asubuhi na usiku huo ndio ulinikubalia kuwa mpenzi wako. Nilikua na furaha ya ajabu Annrosse. Uliniambia ni kiasi gani ulinipenda ila hukuwa unaniamini mwanzo.

Huu ulikua ni mwanzo wa safari yangu ya mapenzi na msichana niliyempenda mno japo sikuwa namjua wala kumwona. Sijui kama ulikua ni utoto au ujana kwa savabu yote haya yalitokea nikiwa na umri wa kama miaka 18 - 19. I was so deep in love.

Nakumbuka tuliongea mengi sana tukiwa kwenye uhusiano. Ulinieleza kuhusu maisha yako hapo nyumbani kwamba unaishi na baba kama sikosei na ulikua Dar kwa wakati huo mimi nikiwa Arusha. Ulikua pia unaishi na mdogo wako anayeitwa Mikah na mara nyingi nikikupigia ukawa unasema naosha nguo za Mikah nikakwambia si kuosha nguo ni kufua nguo.

Ulinitambulisha wimbo wa Lionel Richie unaoitwa Good Morning. Nilikwambia nampenda sana Lionel Richie ila ukashangaa why siujui wimbo wake Good Morning. Nilikwambia Lionel Richie ana nyimbo nyingi na nikakambia kuna nyimbo zake kibao pengine we huzijui. Ukaniambia ipi kwa mfano?

Tell me your favourite song of him kama siijui nidai chochote. Nikaanza kuuimba wimbo wa Leonel Richie Cinderella. Cha ajabu it was also your best song na tukawa tunauimba wote. For the first time. It was so romantic. Baadaye ukaanza kulia then ukaniambia kitu ambacho sitokisahau maishani mwangu. Ulisema ''Annrosse nimeshikwa. Nakupenda sana ,,,,,,,,,,,,''

Nakumbuka pia ulikua ukinipigia alafu unakaa kimya unaniambia nikuimbie wimbo wa Jay Z forever young kile kibwagizo cha mwanzo tu. You relly loved it lakini ulikua huwezi kukiimba. Tulipendana sana na mpaka miadi ya kuonana na kuona tuliiweka Annrosse.

Tuliwasiliana kwa miaka kadhaa tukiwa deep in love. Ila nakumbuka baadae niliibiwa simu. Sikuwa na kazi kipindi kile na wala sikuwa na uwezo wa kumiliki smartphone hvyo nba yako ikapotea. Kuna mahali niliiandika namba yako na niliipata baada ya kama miaka miwili Annrosse. Hukuwa unapatikana tena na sikukupata milele. Nakumbuka ulinambia ile line ya Zantel ulikuwa nayo kwa sababu yangu tu. Sielewi labda baada ya kupotea kwa muda nawe ukakata tamaa ukatupa line yako.

Nakutafuta Annrosse. Nipo Arusha nimeoa na nina watoro wawili sasa. Tafadhali jitokeze hata nikuone. Hata kama umeolewa naomba nikujue walau nikuone hata mara moja kabla sijafa. Ewe ndugu kama unamfahamu mwanamke anayeitwa Annrosse mwenye mdogo wake wa Kiume anayeitwa Mikah, popote alipo naomba unijuze.

Atakuwa na umri wa kati ya 27 - 35 kwa sasa mwaka huu wa 2022. Na hata kama atakua ametangulia, natamani hata kuliona kaburi lake. I swear to my living God ntakuja kuliona.

Mungu anisaidie
 
Umuone tuu au kuna sababu nyingine?

Anyway pole sana mkuu.
Darlin
Asee nimuone tu. You can never imagine ni jinsi gani I was in love. Si unajua mapenzi ya ujanani? Nilitamani kutembea kwa mguu mpaka Dar ila nilikua kapuku sina mia. But huyu mtoto we had Chemistry. Nilimpenda sana Annrosse.
 
Yaani miaka yote hiyo awe bado hajaolewa.
 
Darlin
Asee nimuone tu. You can never imagine ni jinsi gani I was in love. Si unajua mapenzi ya ujanani? Nilitamani kutembea kwa mguu mpaka Dar ila nilikua kapuku sina mia. But huyu mtoto we had Chemistry. Nilimpenda sana Annrosse.
Ulikuwa kapuku huna hata mia..si ndio ungetembea hadi Dar! uliona wapi wenye hela wanatembea kwa miguu kama ulivyotamani!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom