Mkuu Ulichotushauri Ni Kizuri ila Umesahau Kitu Kimoja Muhimu Sana Kukizungumzia Ndani Ya Ushauri Wako! Si Chengine Bali Ni "Tuition Fee & Possible Loan Amount".
Mkuu Kuhusu Program hii ya optometry, Kwenye TCU-GuideBook Wametuelekeza Hivi:-
Tuition Fee: 4,400,000
Possible Loan Amount: 2,800,000
Sasa Hapo Mkuu Nilichofahamu Mimi Ni Kuwa Chuoni Utalipa 4,400,000! Lakini Mkopo utakaopewa Ni 2,800,000/=
Inamana Hapo Kwa Ufahamu Wangu Ni Kuwa Unaongezea Pesa Zako Mwenyewe 1,600,000/=
Sasa Mkuu Masikini Kama Mimi Na Wenzangu Tutaupokeaje Ushauri Kama Huu?
Mkuu 1,600,000 ni Hela Ndefu Sana Kwa Mtu Kama Mimi ambaye Sifa Ninazo Lakini Kwa Vyuo Kama KCMC, CUHAS, HKMU, tunaishia Kuviangaliaga tu Lakini Standard Za Maisha Zinatuzuia Kuvisoma.
Nilipokosea Nirekebishe usinilaumu.