Kinga kingdom
JF-Expert Member
- Jan 11, 2017
- 769
- 847
Habari wanabodi,
Baada ya kutafakari yanayoendelea kwenye nchi yetu Tanzania nimeona ni vema nikusalimu RAIS wetu mstaafu JMK.
Kwanza kabisa shikamoo MHESHIMIWA, naamini unaendelea Vema na Majukumu yako ya kila Siku na ninamuomba mwenyezi Mungu Azidi kukubariki.
Pia baba mie mtanzania wako ulieniongoza kwa miaka 10 nimeona nikushukuru kwa kuniongoza kwa kipindi chote hicho..
Mkuu katika uongozi wako yapo mambo mengi niliyoyafaidi,ila ntataja machache niliyoyamiss kwa sana:
Kwanza:uhuru wa kuongea na nikawa salama-mkuu kwenye utawala wako ulitupa nafasi ya kuwa na uhuru wa kuongea na kusema chochote na hii ilifanya watu kuongeza kiwango cha udadisi kwa watanzania wengi-hata kama tuliongea tukapitilza mipaka ulituchukulia Poa na kuendelea na Majukumu yako.
Pili😀emocracy:Baba ulituacha tupambane na kila mikakati yetu ya kukuza democrasia nchini,vyama pinzani vilitekeleza operation zake bila kuzuilika na mikutano mbalimbali, Pamoja ya kuwa kuna mengine ulizuia lakini si haba mambo yalikwenda.
Tatu:Baba nakumbuka uwezo wako wa kuhutubia,ulipanga hoja zilizonyooka na zisizo na jazba..hata kama kuna sehemu hukutekeleza Ila ulituaminisha kwa maneno ya staha..ndio maana tulipenda hotuba zako za Kila mwisho wa Mwezi.
Nne:Baba katika utawala wako ulitufundisha ukitaka kula nawe ukubali kuliwa😛amoja na kuwa wapo waliotumia vibaya Kauli hii binafsi niliamini kama nataka kupokea lazima nijifunze kutoa...na kwa hakika kila biashara niliyowekeza ilinilipa vizuri-kwa hili nitakukumbuka..
Tano:Baba tabasamu ni tiba:kila ulipoongea nasi ulituonyesha tabasamu lenye upendo kwa watanzania, hata kama tumekusema vibaya Bado ulionyesha tabasamu,kitaalamu ulituponya kisaikolojia Kwan tabasamu ulilokua Unatoalilituponya.. Hitaji la kwanza la Kila mwanadamu ni kupendwa!!tabasamu lako lilileta raha hata usimamapo kuhutubia.
Mkuu ulinifurahisha Sana usimamapo kuhutubia nchi mbalimbali duniani kwa kujenga hoja na kiingereza kilichonyooka kwa ajili ya kuinadi Tz duniani kote, na hii iliongeza utalii kukua Tz
Baba pamoja na mapungufu yako Mie binafsi naamini hakuna aliyekamilika Ila kwa haya nitakukumbuka..
Wakuu najua wapo wapondaji na wakosoaji, salamu hizi kwa JK si za kumponda ni za kumshukuru kwa yale mazuri aliyofanya na Sio mabaya,kama nawe kuna zuri ulikumbukalo basi changia..
Mh JK pokea salamu na shukrani zangu.
Kinga Kingdom
Sent from my A37f using JamiiForums mobile app