Nakupenda wewe shani

Tamu3

Member
Feb 17, 2023
25
16
NAKUPENDA WEWE SHANI

Nakupenda wewe Shani, shairi mekutungia,
Kila napokuoneni, nashindwa kukuambia,
Nikwambie neno gani, ujali zangu hisia,
Nakupenda wewe Shani, shairi mekutungia.

Watembea kwa maringo, nyuma umefungashia,
Unaizungusha shingo, madoido waachia,
Fungua chako kifungo, ndani nikichungulia,

Udenda unanitoa, kiona lako furushi,
Mwilini jasho natoa, ninahitaji beleshi,
Meshindwa kuvumilia, kukwambia kwa utashi,

Embe dodo metamani, kumung'unya mdomoni,
Utamu ukoleeni, kisogoni hadi chini,
Tafadhali unipeni, nitulike mtimani,

Embe ukinipatia, nitalila na kushiba,
Ndani nitashindilia, hata kama litakaba,
Mwishoni tatapikia, kutosheka mahabuba,

Denny Jeremias kitumbika
Mtunzi wa mashairi na ngano za Kiafrika
Mufindi Tanzania 6/6/2016
 
Attachments

  • 1710781135551.jpg
    1710781135551.jpg
    181.8 KB · Views: 3

acha uoga sasa...
 
Kijana nikupe namba ya wa 30,au 50?

Wa 150 kwa hii mada yako utapoteza hela tu😁😁😁😁
 
Back
Top Bottom