Nakunda John Pombe Joseph Magufuli

Nakunda John Pombe Joseph Magufuli

manento93

Member
Joined
Jul 19, 2018
Posts
54
Reaction score
33
Magufuli ndiye raisi pekee aliyefufua vitu nilivyotamani kuviona vinainuka tena.

Nilipokuwa mdogo nilishuhudia reli ya Tanga - Arusha ikijifia,

sikufaidi kuziona treni vizuri kwani zilianza kudorora wakati ndo naanza kujua hili na lile,

Nilitamani reli ile iendelee, nilikuwa mdogo miaka ya 2000's ila sikuchelewa kuzitafakari fursa ambazo zingeendelea kupatikana kwa wakazi wa maeneo yale ya Tanga, Same, Mwanga. Chekereni na Arusha (kama sikosei jiografia ya sehemu hizo)

MH. JPM ametia chachu katika miradi mikubwa, mfano miradi inayoendelea ya miundombinu ya maji kanda ya ziwa, Kilimanjaro, SGR, Umeme, Barabara na Madaraja.

Naweza kukiri kuna changamoto katika suala zima la utekelezaji wa baadhi ya mambo ambayo ni shauku ya rais wetu., mfano ELIMU BURE, Ila nampomgeza sana Rais wetu kwa uthubutu wa kizalendo kabisa.

Rais Magufuli ni muendelezo wa baraka za mungu katika taifa la Tanzania.

Rais wetu mungu akupiganie. Hata manabii walipingwa, wanapingwa na wanaendelea kupingwa. Wewe ni baba wa taifa letu kwa sasa.

Nikiri pia kwamba si kila litekelezwalo chini ya uongozi wako limenibariki ila hakika nimeshindwa kukulaumu kwa uimara na uthabiti wako John kwani mazuri unayatenda kwa moyo na dhati.

Nimalizie kwa kusema, kero nyingi za wanachi zimetatuliwa haraka kwa sauti yako yenye kumaanisha usemacho.

Watumishi wenye madai kama walimu na madai ya uhamisho, na kero zingine zinazowakabili wafanyakazi zinaweza kutatuliwa Mara moja kwa ile sauti yako kama baba na kiongozi wetu.

Mungu akupiganie. Akubariki.

Amina.
 
Kwa waalimu nadhani unawadhihaki, hawajapanda madaraja wala nyongeza ya mishahara toka 2015...kikwete
 
Inadaiwa duniani kote Mkubwa anapimwa na mambo mawili tu, mengine ni mbwembwe...Ajira na Ku control mfumuko wa bei.
 
Sema ajae atakuta mifupa tupu,anamwachia Kazi kubwa ya kulipa madeni aje
 
Magufuli ndiye raisi pekee aliyefufua vitu nilivyotamani kuviona vinainuka tena.

Nilipokuwa mdogo nilishuhudia reli ya Tanga - Arusha ikijifia,

sikufaidi kuziona treni vizuri kwani zilianza kudorora wakati ndo naanza kujua hili na lile,

Nilitamani reli ile iendelee, nilikuwa mdogo miaka ya 2000's ila sikuchelewa kuzitafakari fursa ambazo zingeendelea kupatikana kwa wakazi wa maeneo yale ya Tanga, Same, Mwanga. Chekereni na Arusha (kama sikosei jiografia ya sehemu hizo)

MH. JPM ametia chachu katika miradi mikubwa, mfano miradi inayoendelea ya miundombinu ya maji kanda ya ziwa, Kilimanjaro, SGR, Umeme, Barabara na Madaraja.

Naweza kukiri kuna changamoto katika suala zima la utekelezaji wa baadhi ya mambo ambayo ni shauku ya rais wetu., mfano ELIMU BURE, Ila nampomgeza sana Rais wetu kwa uthubutu wa kizalendo kabisa.

Rais Magufuli ni muendelezo wa baraka za mungu katika taifa la Tanzania.

Rais wetu mungu akupiganie. Hata manabii walipingwa, wanapingwa na wanaendelea kupingwa. Wewe ni baba wa taifa letu kwa sasa.

Nikiri pia kwamba si kila litekelezwalo chini ya uongozi wako limenibariki ila hakika nimeshindwa kukulaumu kwa uimara na uthabiti wako John kwani mazuri unayatenda kwa moyo na dhati.

Nimalizie kwa kusema, kero nyingi za wanachi zimetatuliwa haraka kwa sauti yako yenye kumaanisha usemacho.

Watumishi wenye madai kama walimu na madai ya uhamisho, na kero zingine zinazowakabili wafanyakazi zinaweza kutatuliwa Mara moja kwa ile sauti yako kama baba na kiongozi wetu.

Mungu akupiganie. Akubariki.

Amina.
Ukikua utaelewa
 
Haya maneno hayapendwi hapa na powers that be sasa hivi itahamishiwa ,,Viva Magufuli, viva”
 
We mwehu Reli Ya Tanga-Arusha imekufa long ago....

Lete hotuba yoyote ya yule Kichaa aliyewahi kuongelea kuifufua hiyo Reli..

Yaani aache kujenga reli ya kwenda Rwanda ajenge Reli ya Kaskazini? Atakua sio mwehu labda.

Ni mradi gani mkubwa au ziara aliyoifanya Kaskazini zaid ya ile ya ukuta wa Mererani ama sikukuku ya Mei mosi?

Kaskazini mna faida gani gani kwake..si mlimpigia kura Lowassa nyie??
Sasa hivi ziara ni Mwanza kwa watu waliomchagua. Period.
 
Je ni lazma ahutubie?
 
Back
Top Bottom