Nakumbuaka sana siku za mwanzo.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nakumbuaka sana siku za mwanzo....

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by sarikoki, Sep 13, 2012.

 1. s

  sarikoki JF-Expert Member

  #1
  Sep 13, 2012
  Joined: Sep 30, 2011
  Messages: 1,196
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Nakumbukuka sana tabasamu lako siku za mwanzo liliweza kabisa kutibu magonja yote niliyokuwa nayo hata bila ya Dr.
  Nakumbuka tulivyokua tunatembea tumeshikana mikono huku tunapiga story nzuri za maisha..
  Nakumbuka sana ulikua karibu na wazazi pamoja na ndugu zangu..ulikua ukiwapigia simu mara kwa mara kuwasalimu..
  Nakumbuka siku za mwanzo hukupaona kwetu mbali.... ulitabasamu na kumfurahia kila uliyemkuta nyumbani.
  Nakumbuka pia ulinifanya niwe nadhifu.... mara kwa mara nilikuta suprise ya kabati langu kupangwa vizuri..getto likiwalimefanyiwa usafi na mezani nilikuta umuniandalia chakula na ki-note cha I love u.
  Nakumbuka tulikua tunapiga gemu mpaka ukitembea unapepesuka....
  Nakumbuka sana kunywa kwangu bia hakukutatiza......

  Nakumbuka wakati nakupitia chuo kukurudisha nyumbani kwenu.. nilikushika mkono kukuvusha barabara na kukukinga na fujo za kugombania daladala kama mtoto na mzazi..Ingawa sikuwa na gari lakini ulikua na furaha.

  Kwa kweli ni mengi sana mpaka saa nyingine nikitafakari machozi ya furaha hunidondoka.

  Sikuambayo sita isahau ni pale kanisani St Peters ulipokua unashuka kwenye gari...uzuri wako ulizidi ukawa kama malaika....ulinitabasamia alafu ukanikonyeza ..na mimi nikakukoneza. Ni siku tulipokula kiapo cha ndoa.

  Sasa ivi ni miaka imepita Mungu ametujalia kila kitu kizuri....na cha zaidi ni watoto wazuri na wenye afya nzuri,
  Yote ya nyuma umeyAsahau..umebadilika umekua kiumbe mwingine..sikumbuki ni lini tumeshikana mikono au kiuno barabarani.. nimelisahau tabasamu lako zuri.... hutaki kusikia sina pesa..daladala imekua ni kero kwako...siku izi kwa mama naenda mwenyewe, pamekua mbali. Mama akiniuliza nashindwa kumjibu.
  Bia imekua kero kwako.... nikinywa hata moja unalalamzungu wa nne eti Harufu. Siku hizi Gemu limekua la manati na lakuvizia.

  Sikumbuki tena ni lini umepasi nguo zangu..chakula chako kitamu nimekimiss....
  Nimeumiss urafiki tuliokua nao...umepata marafiki wengine huko kazini kwako.... uko nao busy hata ukirudi home unaendelea kuchati nao kwenye simu.

  Mwanayumba nakupenda sana kwa nini umebadIlika hivyo...nini kimetokea?

  KAMA NDOA/MAUHUSIANO YAKO INAMATATIZO NA MLITOKA MBALI NA MWENZA WAKO TENGENEZA STORY KAMA HII ALAFU UKAMWELEZE MWENZA WAKO. HII NI STORY TU WANA JF.
   
 2. sakapal

  sakapal JF-Expert Member

  #2
  Sep 13, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,824
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Thank you very much sarikoki u heal me.
   
 3. Asulo

  Asulo JF-Expert Member

  #3
  Sep 13, 2012
  Joined: Jun 25, 2012
  Messages: 733
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Sawasawa tumekusoma..Tunashukuru kwa ushauri.
   
 4. s

  sarikoki JF-Expert Member

  #4
  Sep 13, 2012
  Joined: Sep 30, 2011
  Messages: 1,196
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Your very welcome Sakapal..
   
 5. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #5
  Sep 13, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,347
  Likes Received: 2,685
  Trophy Points: 280
  majuto ni mjukuu
   
 6. Mbimbinho

  Mbimbinho JF-Expert Member

  #6
  Sep 13, 2012
  Joined: Aug 1, 2009
  Messages: 6,027
  Likes Received: 2,868
  Trophy Points: 280
  Asee, what a touch. I guess kwa Maisha yangu ya ndoa Bomani inanihusu.
   
 7. happiness win

  happiness win JF-Expert Member

  #7
  Sep 13, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 2,478
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Kama ningeweza, kuzirudisha siku nyuma
  hata magoti ningepiga, ili nipate upendo wako wa mwanzo ......
  ha ha haaaaaaaaaaa nilikuwa naimba tu.....
   
 8. k

  kisukari JF-Expert Member

  #8
  Sep 13, 2012
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 3,764
  Likes Received: 1,052
  Trophy Points: 280
  mapenzi ndivyo yalivyo,saa nyengine hata ukikumbushia,atafanya mwanzo,baadae anarudia yale yale.
   
 9. Mbimbinho

  Mbimbinho JF-Expert Member

  #9
  Sep 13, 2012
  Joined: Aug 1, 2009
  Messages: 6,027
  Likes Received: 2,868
  Trophy Points: 280
  Asee, what a touch. I guess kwa Maisha yangu ya ndoa Bomani inanihusu.
   
 10. s

  sarikoki JF-Expert Member

  #10
  Sep 13, 2012
  Joined: Sep 30, 2011
  Messages: 1,196
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Ni kweli kabisa...lakinia aslimia kubwa kina mama ndio mnabadilika...mnajisahau sana.
   
 11. s

  sarikoki JF-Expert Member

  #11
  Sep 13, 2012
  Joined: Sep 30, 2011
  Messages: 1,196
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Majuto ya nini kiogozi.
   
 12. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #12
  Sep 13, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kukumbushana muhimu, kwa maneno na vitendo.
   
 13. Lisa

  Lisa JF-Expert Member

  #13
  Sep 13, 2012
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 1,568
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Nakumbuka ulivyokuwa unakuja kunisubiri ofisini mpk natoka na kunirudisha home ingawa hukuwa na gari tulipanda daladala,
  nakumbuka ulipokuwa ukisafiri lazima uniletee zawadi hata kama ni kibanio cha nywele
  nakumbuka ikifika jumamosi unanipeleka dinner hata kama ni bonanza pale TCC clab
  Nakumbuka ulipokuwa unanikiss na kunikumbatia na kuniambia maisha yako bila mm hayajakamilika
  Nakumbuka wakati ule hakuna simu za mkononi unipigia simu kwa jirani ili kunijulisha kama umeshafika kwako
  Nakumbuka ulipotoa kiapo chako pale St Joseph na kufunia shela langu na kuniambia unanipenda
  Duh! umenikumbusha mambo mengi sna na nimesikia uchungu sana .....
   
 14. KIKUNGU

  KIKUNGU JF-Expert Member

  #14
  Sep 13, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 853
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Duh..............Sarikoki we acha............Nakumbuka tulivyokuwa tunalalia Toast na Maharage ili mmoja wetu asome.......Nakumbuka siku ulivyomwangalia first born wetu,ukasema mwangalie huyu mtoto ulivyofanana nae............Lakini pia nakumbuka ulivyonisaliti............ulivyonisaliti..........ulivyonisaliti na hatimae nika-give up......baadae tuka-DIVORCE.................

  Duh dada @Kaunga hebu njoo unifute machozi maana huyu Sarikoki kanikumbusha mbali sana.Labda niwaulize walimu @gfsomwin na @Snowhite kwa nini mnatutesa watoto wa wenzenu bwana
   
 15. s

  sarikoki JF-Expert Member

  #15
  Sep 13, 2012
  Joined: Sep 30, 2011
  Messages: 1,196
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Inaumiza sana kama mmeanza mbali alafu mmoja anapotea.......kama binadamuangekua kama gari au simu au radio, ungemfungua alafu utengeneze kilichoaribika ili arudi kuwa kama mwanzo....lakini bahati mbaya ni vigumu. I always tell friends usisubiri mpaka mambo yaharibike ndio uanze kurekebisha....everyday in our life new things happen so human changes as well, tusichoke kukumbushana. Nimesoma comments za mambo mengi ya matatizo ya ndoa....nimegundua wengi hawa take trouble kuwajua wenza wao....ndio maana mabadiliko yanapotokea hawajui...wanakuja kujua too late.
  Pole sana kwa yaliyokukuta.
   
 16. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #16
  Sep 13, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 801
  Trophy Points: 280
  Pole kaka yangu, yaani baada ya kusoma Uzi huu nimskufikiria kabla hata ya kuona post yako KIKUNGU; sina maneno ya kikufariji zaidi ya kukupa a shoulder to cry on.
  I know how it hurts, na it won't go away no matter what hata nikikuambia things happens for a reason, some reasons are not fair kabisa.

  Nikisema, it could have been worse; what can be worse than being betrayed by the person you have loved like that?

  Nikisema, utasahau? How can u do that while you brought those two beatiful kids in the world?

  Ninachoweza sema ni kwamba, you are much loved by us (ur family) and most importantly God!

  Cheer up brother!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. s

  sarikoki JF-Expert Member

  #17
  Sep 13, 2012
  Joined: Sep 30, 2011
  Messages: 1,196
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Msichoke kukumbushana.... binadamu ni wasahaulifu sana.... my dad always tell me not to trust anybody..even my p.nis. Wanandoa wanogopa kukumbushana kwa sababu eti utaonekana humuamini mwenzi wako au hamuaminiani. Its not our culture....
   
 18. KIKUNGU

  KIKUNGU JF-Expert Member

  #18
  Sep 13, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 853
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Asante Sarikoki.Communication kwenye mapenzi/ndoa ni muhimu sana,ikiwa pamoja na kukumbushana.Nimepata uzoefu mwingi sana kupitia machungu i went through.Will i ever fall in love again?Absolutelly
   
 19. KIKUNGU

  KIKUNGU JF-Expert Member

  #19
  Sep 13, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 853
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Asante sana ilumbuye Kaunga for cheering me up,mungu na akubariki sana
   
 20. Babarita

  Babarita JF-Expert Member

  #20
  Sep 13, 2012
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 374
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Ngoja niikariri siku mamarita akianza maswaiba namfungulia kurasa
   
Loading...