Nakulaani Manka! Ulinifilisi bila tone ya huruma

Nakulaani Manka! Ulinifilisi bila tone ya huruma

kinyamkela mahaba

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2022
Posts
1,180
Reaction score
1,599
Hii ni historia ya jinsi nilivyokutana na huyu Mchagga na kilichoendelea mpaka kufilisika vibaya.

Wengi humu JF mmekuwa mkinichukulia mtu asiyeeleweka na masikini mno. Hasa baada ya kusema nilikusanya 8000 kwa karibu miezi minne kwa kusave sehemu ya hela nilizopata(sio uongo ni kweli nili save na nauza karanga kwa sasa). Hiki ndicho kilichonitokea,,

Ngoja nianzie hapa:

Mwaka 2010 nilikutana na huyu Mzungu raia wa Sweden visiwani Zanzibar, yeye akiwa ni Mhandisi wa kampuni fulani ya simu HQ. Na alikuwa amekuja Zanzibar kutalii na kupumzika.

Tumuite Linda. Wakati Linda akiwa mapumzikoni Zanzibar, nilikuwa na rafiki yangu aliyeitwa Mick(sio jina halisi) na ndiye aliniunganisha na huyu Mzungu mara baada ya huyu dada kuvutiwa na mimi. Wakati huo nilikuwa nahudumu kama kibarua niliyelipwa kwa siku hapo hotelini.

Na tenda hii pia nilipewa na huyu huyu Mick. So ilikuwa rahisi kwa mimi kukutana na Linda mara kadhaa ingawa sikuwa najua kuwa alinipenda.

Tukaanzisha mahusiano ya mapenzi na kwa kweli kwao hela ilikuwepo. Baba yake mzazi alikuwa na jumba kubwa la kifahari Masaki. Naye alikuwa na pesa.

Nilibahatika kupata naye watoto wawili wa kiume wakati tulipohamia Sweden wote. Alinishughulikia kila kitu kuhusu nyaraka za kupata uraia halali wa Sweden.

Nilikuwa nakaa kule miezi hata miwili naruka nakuja TZ nakaa hata miezi 2 au zaidi na kurejea tena. Hela hizi mil 2 sijui 3 nilikuwa nazichezea mno na zilikuwa kama za mboga kwa wakati huo.

Mama yangu alikuwa akiishi dsm na alikuwa na shamba la hekari 1 Mkuranga. Linda alinitumia hela takribani 90M nakumbuka. Ilikuwa kwa ajili ya kumnunulia mama hekari zaidi ya 30 za mashamba huko Mkuranga na zingine nilimpa kwa matumizi yake. Pia Linda aliniambia nigawe kiasi ninunue pick up kwa ajili ya mama kwenda shambani.

Nikiri nilianza kuingiwa na roho ya usaliti ingawa huyu mama watoto wangu aliniheshimu na kunijali alinyenyekea na hakuwahi kunikosea heshima hata siku moja.

Nilianza kum cheat mara kadhaa ukizingatia nilishapata marafiki wengi, pindi nikija huku TZ ilikuwa ni kujirusha na starehe za anasa.

Nakumbuka nilikuwa naweka 1M juu ya meza bar nikiwa na rafiki zangu na kuwaambia 'hiyo hela iishe leo', na walishindwa kuimaliza mara kadhaa.

Niliota mapembe na sikusikia la kaka yangu wala nani. Nilijiona mjanja na kujiuliza nilichelewa wapi. Nikaanza hata kuwatongoza rafiki zake Linda(mke wangu) bila aibu.

Heshima niliyopewa na Linda ilinipa kiburi. Nikaanza kumuona bibi na kinyaa, ingawa hakuwa bibi. Nilihonga sana watoto wa mjini. Itoshe kusema kama starehe nilifanya mno na hela nilichezea sana.

Nakuja kuendelea, leo hii nimekumbuka mbali sana
 
Naendelea:

Ikafika kipindi akanionya zaidi ya mara nne ila nilijirudi na kulia na kuahidi nitaacha mambo yangu, japo hakuwa na uhakika ila alikuwa ananihisi tu.

Mwaka 2017 alinipa 500M kwa ajili ya kujenga nyumba nzuri ya kifahari na kufungua biashara pale Kariakoo ya hardware.

Alifanya hivi ili watoto wakija huku wasipate shida kuishi maisha angalau yenye unafuu. Hela hii aliyonipa ilikuwa ni mgao aliopata baada ya baba yake kuuza nyumba moja ya nyumba zake.

So hela yote akanipa mimi. Siku moja wakati nimeenda kariakoo nilitokea kumpenda dada mmoja ambaye alikuwa mweupe mwenye shape kubwa.

Aliitwa Manka(sio jina halisi na alikuwa Mchagga). Tulianza mahusiano rasmi kwani hakuonesha ugumu sana.

Ile pick up ya mama nilimdanganya nikampa huyu Manka ili abebee mizigo yake pale K/Koo kwani alikuwa na frame zake tatu zimepangana. Hakuwa haba alikuwa na hela.

So mama akawa anachukua usafiri kwenda shamba. Ikumbukwe nilikuwa nimejenga jumba ndogo ya kawaida tu huku Tz kwa wakati huo.

Manka alijitahidi kunizoea haraka haraka na ndani ya muda mfupi tukawa tumeshazoeana sana.

Wakati huo wote mawasiliano na Linda yaliendelea kama kawaida na nikamdanganya nakamilisha ile mipango.

To cut long story short, nilimuambia kuhusu ile milioni miatano kwenye acc na akashauri nimpe aingize kwenye biashara.

Sasa sijui kilitokea nini akampigia Linda simu na kumuambia amuachie mume wake. Linda alichukia mno na akakata mawasiliano na mimi mazima, hakutaka kusikia kitu tena kuhusu mimi.

Niliumia mno ila nilijishangaa nikapotezea(nafikiri huenda aliniroga huyu Mchagga).

Baada ya kumpa zile hela mawasiliano yakaanza kupungua. Akawa anachelewa kupokea simu zangu na wakati mwingine hapokei kabisa. Hiyo ilikuwa 2017 mwishoni mwezi wa 12 hivi.


Mwisho mwaka 2018 mwanzoni kabisa akaniandikia msg ndefu akisema nisimfuatilie tena,,nikithubutu atanitengenezea kesi ya madawa ya kulevya.

Pia akasema hata hicho kijumba ningeamua ningekichukua ila nimekuachia.

Sikuamini, kwa mara ya kwanza nililia nikigumia kama mbwa, nililia kilio cha mbwa. Sitoisahau siku ile***

Maisha niishiyo sasa nafikiri huenda ni laana imechangia,,hakunidai chochote yule Mzungu. Sijawaona tena wanangu mpaka leo hii na sijui wanaendeleaje.

Manka bado yupo kariakoo na anaendelea na biashara yake. Hata dukani kwake nimepigwa marufuku kwenda.

Mpaka leo hii siamini kama 500m imekwenda kizembe hivyo najiona mjinga na najipa moyo huenda ni ndoto.

Daaah ndani ya muda mfupi maisha yamenigeukia namna hii.

nimeamua ku share humu kupunguza uchungu, sijamuambia yeyote. Ila huyo Mchagga kama yupo humu, akisoma atanijua.

Mchana mwema
 
Kwa hiyo ndiyo weye uliyeimbwa kwenye wimbo wa Prof.Jay?Mademu walikuzimia.Unafaa ujitokeze tukutandike bakora "salasini na tisa" shingoni ili kuonesha umejutia makosa yako.Tumekusaka sana sisi wanandugu!
 
Never give up kilichopotea kimepotea endelea kupiga kazi.milioni 500 ni pesa nyingi sana Kwa level ya maisha yetu lakin ishapotea.
 
1652964821304.png
 
Naendelea:

Ikafika kipindi akanionya zaidi ya mara nne ila nilijirudi na kulia na kuahidi nitaacha mambo yangu, japo hakuwa na uhakika ila alikuwa ananihisi tu.

Mwaka 2017 alinipa 500M kwa ajili ya kujenga nyumba nzuri ya kifahari na kufungua biashara pale Kariakoo ya hardware.



Mchana mwema
Ww ungemtag huyo mchaga kwanza maan ni noma sana
 
Back
Top Bottom