Nakukumbusha Profesa Muhongo, sijui unakumbuka!!

kiduni

JF-Expert Member
Jun 26, 2015
348
341
Wakati wa mgogoro wa gesi mkoani Mtwara tunakumbuka pamoja na hoja uliyoitoa watu wa Mtwara hawana elimu pia uliiaminisha Tanzania ukiwa kwenye kiti hichohicho cha uwaziri unaoshughulikia nishati kwa maana ya kwamba TANESCO iko chini yako.

Ulitueleza umeme ulioko Mtwara ni mwingi kiasi ambacho hata ukisambazwa kwa kila mkazi wa mkoa huo wa Mtwara na Lindi bado umeme utabaki wa kutosha lakini sasa hali ni tofauti. Umeme unaonekana kukosa nguvu na hata mara nyingi kupelekea mgao wa umeme.

Nakuuliza tu muheshimiwa Prof Muhongo unakumbuka kauli yako au ulikuwa unawahadaa watanzania?

Umeme wa mgao ushakua kero Mtwara tunahitaji ufumbuzi umeanza mwezi wa 11 mwaka jana 2015 mpaka leo mwezi wa pili hakuna dalili ya kuisha kwa mgao.

Update;
Tangu post hii iwekwe jukwaani jumatatu tarehe 22/02/2016 saa 2:33 asubuhi umemekatwa leo tarehe 25/02/2016 saa 1:26 usiku na imechukua takribani dakika 2 kurudisha umeme
 
Kiduni wewe unaishi mtwara ipi?! Mtwara lindi umeme ni wa kutosha mbona hakuna mgao na umeme uko stable tu. Au mgao unafanywa nyumbani kwako pekee?
 
Hata mie nashangaa manake walituambia mara tu baada ya gesi kufika kwenye mitambo Dar, kukatika kwa umeme kutakuwa historia

Lakini hali ni tofauti kabisa tangu wazindue kwa mbwembwe mitambo ya KinyereZi na kuipokea gesi toka Mtwara hali iko vile vile

Huku Tandahimba, suala la kukatika ni kawaida tena kila ikifika saa moja ucku na kurudisha tatu ucku huo.
Sasa najiuliza, ile gesi bado haijafika Dar?

Pia gharama za umeme zimepanda, Jana nimeenda tanesco kununua umeme wa elfu kumi kama ilivyokawaida yangu, cha kushangaza nimepata unit 9 tu,wakati huko nyuma nilikuwa napata unit 77.

Prof Mhongo anapaswa kutueleza ukweli
 
Muhongo alikuwa anajigamba tu katika kila jambo na kila neno lililokuwa linamtoka ilikuwa ni majigambo na dharau na kebehi tu, wala hakukmbuki kama alisema hilo.
 
Kwanza kabisa mtoa mada acha kupotosha uma ni lini Tanesco wametanga magao wa umeme. Maana hatujasikia tamko lolote la kuhusu mgao wa umeme. Napa uwe unafatilia jambo kwanza ili uwe na uwakika kabla ya kupost kitu usichokuwa na uwakikia. Maana Kila siku imekuwa ni lawama zisizo na uwakika hata kidogo
 
Hivi unaelewa kusema uongo ni Dhambi. Kwa kumbukumbu yako fupi lini Tanesco wametangaza mgawo wa umeme.natamani TCRA kwa ile sheria ingedil na watu kama nyie.Muhongo alisema itafika wakati tutasahau kukatikakatika kwa umeme.usiwe mvivu wa kufikiri.jipange urudi upya dogo
 
We kiduni nadhani ww huko humu kuupotosha uma maana nashangaa uko Lindi ipi au mtwara ipi ambayo wana mgao wa Umeme maana ninachofahamu mimi hakuna mgao zaidi ya wezakuwa itlafu ndogo tu na hata hivyo Tanesco wamekuwa wakitoa taarifa kwakila Tatizo linalotokea alafu leo unakuja humu unatoa taarifa za uongo na kuupotosha uma. Nanyie manao sema waziri ni muongo sioni uongo wake uko wapi maana alicho sema ni kweli. Zaidi naona nyie ndo waongo Kwa kutaka kuupotosha uma
 
Na Vilevile Mkurugenzi mtendaji wa Tanesco Mhandisi Felchesmi Mramba mwezi huu alitembelea mkoa wa Lindi na Mtwara na kuzungumza na Uongozi wa Mikoa hiyo.kuonyesha jitihada zinazofanywa NA TANESCO kwa sasa ni kupeleka Mtambo wenye uwezo wa kuzalisha Megawatt 20 kwa kutumia gesi.tunakuomba uwe na Subra.ok Kiduni.Acha kulalamika Hapa kazi tu
 
Kiduni wewe unaishi mtwara ipi?! Mtwara lindi umeme ni wa kutosha mbona hakuna mgao na umeme uko stable tu. Au mgao unafanywa nyumbani kwako pekee?
Naishi Masasi, Mtwara, na nyumbani ni Newala Mtwara huo umeme unaosema wa kutosha uko wapi?
 
Kwanza kabisa mtoa mada acha kupotosha uma ni lini Tanesco wametanga magao wa umeme. Maana hatujasikia tamko lolote la kuhusu mgao wa umeme. Napa uwe unafatilia jambo kwanza ili uwe na uwakika kabla ya kupost kitu usichokuwa na uwakikia. Maana Kila siku imekuwa ni lawama zisizo na uwakika hata kidogo
Kwa kua hawajatangaza mgao, huku kukatwa umeme kwa masaa kadhaa haswa majira ya usiku tuite nini? Najua unatumbua we ni muongo mimi niko eneo husika (Masasi, Mtwara) ninalifahamu tatizo na nimeeleza limeanza mwaka jana mwezi wa kumi na moja mpaka jana usiku pia ulikatwa kuanzia saa 1 mpaka saa 4, na huu ukataji wa umemw ni wa mara kwa mara mchana unakatwa mara nyingi na inaonyesha ni makusudi sababu unawezwa kukatwa na ukarudishwa muda huohuo wakakata tena
 
Hivi unaelewa kusema uongo ni Dhambi. Kwa kumbukumbu yako fupi lini Tanesco wametangaza mgawo wa umeme.natamani TCRA kwa ile sheria ingedil na watu kama nyie.Muhongo alisema itafika wakati tutasahau kukatikakatika kwa umeme.usiwe mvivu wa kufikiri.jipange urudi upya dogo
Mimi niko Masasi-Mtwara haya niloyaandika ndo yaliyopo na yanayoendelea na nimefikia hatua ya kushangaa kutokana na muheshimiwa waziri alisema umeme uko mwingi hata uunganishwe kwa wakazi wote lakini sasa iko wazi aliudanganya uma maana wakazi walounganishiwa umeme hawazidi nusu na sasa kuna hili tatizo ambalo dhahiri inaonekana mgao kutokana na namna unavyozimwa sifikirii wafanyakazi watanesco hawawezi kufanya marekebisho mchana wanasubiri usiku wafanye marekebisho haiingii akilini kabisa, ndugu yangu unayekataa hoja hii we uko wapi? Mi niko sehemu husika
 
Back
Top Bottom