Hasante...alifariki tukiwa bado chuo...nilishaoa tayari.
hahahahhahaahahahahahahh umenchekesha sana aiseee mimi hii valentine naisikiaga tu nikiuliza naambiwa mi nshazeeka hayo ni mambo ya vijana hahaahahahahahahaah
ha ha haaa, Smile mdogo wangu, mimi na wewe inabidi tuwe na mazungumzo mareeefuuuu sana.... maana tangu tumeanza kuziongelea hizi nyuzi za val's kama sikusomi vile!duuh pole sana
wanawake wengi tunapenda siku hii ya leo
mimi sina cha kukumbuka,majanga matupu mkuu
ulijisikiaje alivokufa? uliubeba vipi msiba wake
Pole ndugu sisi sote tunapita,
Mwisho wa story umeninyong'onyeza!
Ni kweli sio story nzuri sana....ila saa nyingine lazima tuwe tayari kwa lolote kwenye maisha.... lazima kama ukiwa na mpenzi ujue kuwa Mungu anampenda zaidi na wakati wowote anaweza kumchukua.
Aisee nimecheka kwa kumbukumbu hii, mwishoni nime huzunika! Pole sana
Ilikua ni mbaya sana.....nakumbuka kipindi cha msiba wale wote waliokua wanajua ni jinsi gani alinipenda na mimi nilivyompenda...walilia sana pindi waliponiona.....walienda kuomba niwekwe kwenye list ya kuweka mashada na udongo kwenye kaburi lake......Nakumbuka pia baada ya miezi miwili baada ya msiba mama yake alikuja kunitafuta chuo......alikuja kunipa pole...aliniambia amesikia jinsi nilivyokua karibu na mtoto wake. Sikuwai kuwajua wazazi wake kabla.