Nakukumbuka sana mdada.....

sarikoki

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
1,194
Reaction score
721
Siku ya valentine wengi wanaikumbuka kwa mazuri na wengine kwa machungu.....
Mimi nakumbuka wakati niko chuo nimetoka mkoani, alitokea dada mmoja kunipenda sana pale chuo......huyu dada alikua ni mtoto wa mujini....alikua akijua mambo mengi sana ya town kuliko mimi, (mfano kama wa Lara 1 ivi). alikua ni badgirl ninaweza kusema.
Huyu dada alitumia muda mwingi sana kunibadilisha ili niwe kama vijana wengine, mimi nilisoma shule ya dini kwa hiyo nilivyokuja mjini nilikua bado nina yale maadili ya kila siku saa kumi na mbili lazima niudhurie misa kabla ya darasa..pia nilishiriki sana shughuli za kanisa kama kumsaidia padre na mda mwingi wa ziada niliutumia kwenda kufanya shughuli za kanisa.
Huyu dada nakumbuka alitumia mpaka pesa zake kuninunulia suruali za jeans na shati za bahama.....alikua anakunywa pombe na kwenda disco...alikua kila siku akirudi usiku lazima aje agonge chumbani kwetu aniamshe aanze kunipigisha story.....nilikua nampa ushauri na kumsihi aache tabia hizo....tulizoeana sana mpaka nIkajikuta na mimi ameanza kunichukua na kunipeleka kwenye starehe........Na kote tulikoenda alikua na company ya wasichana wenzake. Alinifanya marafiki zake wengi wanipende jinsi nilivyo.....nilihisi ushamba wangu na jinsi nilivyokua naongea lafudhi ya kichaga ndio kiliwavutia manaa walinifanya ze comedy, kila nilichoongea kilikua kichekesho kwao, nilikua siendani nao hata kidogo kuanzia mavazi hata muonekano...kila nilipokaa nilizungukwa na wasichana.....na mara nyingi niliwafanyia asignment zao na kuwafundisha. nahisi ingekua ni sasa watu wangefikiri nilikua gay.
Namkumbuka huyu dada siku kama ya leo kwa sababu ndiye wa kwanza kunipeleka dinner , namaanisha dinner kwenye hotel ya kisasa. Aliniletea shati jekundu ,suruli nyeusi nilikua nayo....... nilijua tunaenda kula kama ninavyoagiza hapa canteen.... tulipofika kwenye hiyo hotel nilitaka nirudi....sikuwai kuingia kwenye hotel kama ile.....aliuweka mkono wangu kwapani kwake, aliubana kwa nguvu huku akinivuta na kwa sauti ya kunong'oneza alinisihi nisibadilishe mawazo. Tulifika tukakaa......... meza ilijaa vijiko na visu vingi sikujua ni vya nini vyote hivyo......alikuja muhudumu akanipatia kijitabu, kilikua na kurasa kama sita hivi...kwa kweli sikujua nianzie wapi...nilihisi nguo zote zinanibana.....kwa uso wa tabasamu na furaha alini sogelea akanisaidia kunielekeza jinsi ya kuchagua chakula.....chakula kipokuja nilijikuta nikilalamika kuwa wamesahau kijiko...... nilichoka zaidi aliponiambia nitumie umma na kisu......nilimsihi amuite mhudumu alete kijiko la sivyo naondoka..... alikubali ombi langu na mhudumu aliniletea kijiko.
Sikuwai kumuona huyu dada akicheka kama siku hiyo....wakati tunarudi ,njia nzima mpaka tunafika chuo alikua akinicheka kwa ushamba na vituko nilivyomuonyesha pake hotelini hasa pale nilipocomment ndio alicheka mpaka alikaachini.....mimi pia nilifurahi sana.

Mpaka leo nakukumbuka mdada...namshukuru Mungu kwa mda aliotukutanisha kwani ulibadilisha maisha yangu......ni wewe ndio ulinikumbusha kuwa duniani kuna wasichana na pia hukunifundisha tu kutumia umma na kisu pale mezani.....ulinifundisha pia kitandani.
Najiuliza sana hivi ungekuwepo hai mpaka sasa ingekuaje? Sijapata jibu mpaka sasa.
Mungu aiweke roho yako mahali pema peponi mdada.
 
Masikini a story with a bad ending!pole sana.we umeshaoa?au ndio uliapa kutooa kwa sababu mdada alikufa?

Hasante...alifariki tukiwa bado chuo...nilishaoa tayari.
 
duuh pole sana
wanawake wengi tunapenda siku hii ya leo
mimi sina cha kukumbuka,majanga matupu mkuu

Smile majanga si unayakumbuka pia.....umenichekesha sana.
 
Aisee pole tena,naomba nikuulize swali la kizushi hivi mkeo unampenda sana au ndio ile tabia ya wengi ya kutomsahau mpenzi wa kwanza hasa akiwa ameshakufa?na alimwachia mabo mengi ya kukumbuka?
Hasante...alifariki tukiwa bado chuo...nilishaoa tayari.
 
ilikuwa ngoma au nini? Maana umesema alikuwa mtot wa jiji

Hapana walipata ajali.....alifariki yeye na baba yake...walikua njiani wanarudi dar kutoka Morogoro.....walienda kifamilia kwa ajili ya weekend.
 
Aisee pole tena,naomba nikuulize swali la kizushi hivi mkeo unampenda sana au ndio ile tabia ya wengi ya kutomsahau mpenzi wa kwanza hasa akiwa ameshakufa?na alimwachia mabo mengi ya kukumbuka?

Swali zuri sana. My wife and kids is everything for me. Hapa tunavyoongea maua yako njiani yanamfata alipo.:becky:
Siwezi kuishi na past......hata kama namkumbuka lakini hawezi akanifanya nisimpende mke wangu...itabaki kuwa kumbukumbu tu na sio vinginevyo.
 
Dah, mwisho wako umeninyong'onyeza sana. RIP.

Anyway, maisha yaendelee.
 
Aisee pole tena,naomba nikuulize swali la kizushi hivi mkeo unampenda sana au ndio ile tabia ya wengi ya kutomsahau mpenzi wa kwanza hasa akiwa ameshakufa?na alimwachia mabo mengi ya kukumbuka?
Blue G uzoefu unaonesha mtu huendwa zaidi anapotoka (hasa kufariki). Kwa zaidi ya miaka miwili bado nina funda moyoni na nimeshindwa kuanzisha mahusiano mapya.
 
Last edited by a moderator:
Honestly speaking nimefurahi sana kusikia hivyo,coz walio wengi hushindwa kabisa kufuta kumbukumbu za wapenzi wao waliopita,wengine hujikuta hata wakiwaita wake zao jina la mpenzi wake aliyekufa kwa kisingizio kuwa alimpenda sana,mi naona watu wa naman hiyo wasiwe wanaoa maanake husababisha maumivu mengi kwa wenza wao hasa baada ya kujua aliwahi kuwa na mpenzi aliyakufa na ambaye hawezi kumsahau.Hongera kwako mkuu.
 
Masikini MESTOD pole sana.
Blue G uzoefu unaonesha mtu huendwa zaidi anapotoka (hasa kufariki). Kwa zaidi ya miaka miwili bado nina funda moyoni na nimeshindwa kuanzisha mahusiano mapya.
 
Last edited by a moderator:
"YOU WILL NEVER HURT SOMEONE YOU LOVE." sarikoki ni kweli hii??
:focus: Pole kwa yaliyokukuta mkuu.. Ni kweli wanawake wanawapendaga waseminari sijui kwa nini!!
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…