Nakuhitaji uwe rafiki yangu, mchumba hadi kuwa mke, njoo Pm tuongee

Mcheza Viduku

JF-Expert Member
Jun 24, 2020
1,049
2,537
Kwa mara nyingine narudia kukuomba wewe mrembo unaeishi Mwanza uwe na umri kuanzia miaka 23 hadi 30, kabila yoyote ipatikanayo kanda ya ziwa..... nakuhitaji uwe rafiki yangu, tukienda vizuri uwe mpenzi wangu, tukifahamiana vya kutosha na tukaelewana ipasavyo tuwe mke na mume.

Kabila yangu ni Msukuma, nina miaka 35, ni Mkristo wa dhehebu la RC (Roman Catholic), ni mweupe, mnene kiasi, sio mfupi wala sipo kwenye kundi la warefu, ninakunywa pombe, sivuti sigara wala bangi, ni Mshereheshaji (Master of Ceremony) pia nafanya vibiashara vingine vidogo vidogo.

Wewe ninaekuhitaji; usiwe unajichubua, uwe mweupe au maji ya kunde ni sawa tu, usiwe mnene sana au mwembamba sana (uwe na mwili wa wastani), usijifanye una uzungu wa kuigaiga mambo ishi kwa kufuata maisha yako halisi, elimu ya kidato cha 4 na kuendelea, sintojali ukiwa mfanyakazi au mama wa nyumbani, usivute sigara wala bangi, kutumia pombe kama mimi ruksa, ukiwa umezaa asizidi mtoto mmoja.

Nakuhitaji uwe rafiki yangu humu kwenye Pm z Jf, wakati tunatengeneza taratibu za kuonana, tukionana na tukaridhiana tuwe wapenzi, mipango ya Mungu ikiwa upande wetu basi tuje kuwa mke na mume.

Karibu sana PM tuyajenge my lovely wife to be.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom