Nakuheshimu Dr Slaa ila nenda tu

Nakuheshimu Dr Slaa ila nenda tu

tafakari kali

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2012
Posts
211
Reaction score
39
Binafsi namheshimu sana dr Slaa,amefanya kazi kubwa kwa kweli tena iliyoleta mabadiliko makubwa na kukuza upinzani kwa kiwango kikubwa sana akishirikiana na wenzake.
Amefanya upinzani uwe na nguvu sana kwa kushirikiana na wenzake.

ILA NI LAZIMA AELEWE KUWA KINACHOTAKIWA KWA SASA NA WANANCHI SI NANI YUPO WAPI,WANANCHI WANATAKA CCM IONDOKE MADARAKANI KWA NJIA YOYOTE ILE. ANAPASWA KUELEWA WENGINE SIE HATUKUWA NA MAPENZI NA CHAMA CHOCHOTE ILA TULITAKA MABADILIKO,TULISHAICHOKA CCM TANGU KITAMBO SANA KABLA CHADEMA HAIJAWA NA UMAHARUFU HUU ULIOPO,HATA KAMA WANGEKUWEPO WATU WENGINE TUNGEWASAPOTI TU. AELEWE KUWA KINACHOTUWEKA CHADEMA NA UKAWA SI KINGINE NI CHUKI TULIYONAYO DHIDI YA MACCM AMBAYO YANABAKA MAENDELEO YA WATU NA KUKIMBIZIA KWENYE MATUMBO YAO NA FAMILIA ZAO.

BINAFSI HATA CHIZI AKIONEKA ANA UWEZO MKUBWA WA KUIONDOA CCM MADARAKANI KULIKO CDM NA UKAWA NITAWAACHA NA KWENDA KUUNGANA NAYE..TUPO HAPO SI KWAKUWA TUNAKIPENDA SANA CDM ILA NI KWA SABABU YA KUWA NDO CHAMA NA HASA NDANI YA UMOJA WA UKAWA KIMEONEKANA KINA NGUVU YA KUIONDOA CCM MADARAKANI...NANI YUPO WAPI HAITUHUSU SISI ILA NANI ANANGU U YA KUWAONDOA HAWA JAMAA ZETU NDO SWALA LA MSINGI. KAMA LENGO LETU NI 1 KUIONDOA MADARAKANI CCM KWA NN UWE NA KINYONGO? NI UKWELI USIOPINGIKA KUWA LOWASA ANA USHAWISHI MKUBWA SANA NA HASA YALE MAENEO AMBAYO CCM BADO WANANGUVU NAYO. KQMA UNAONA UTAPASWA KULA MATAPISHI YAKO BASI NI VEMA UKAWA UNAONEKANA NA WENZAKO ILA USISEME WALA KUCHANGIA CHOCHOTE . UKITAKA TUKUSUJUDIE KWA HILI HAIWEZEKANI,TUNAWEZA MPA NCHI MTU YOYOTE KAMA KWANZA ANA NIA YA DHATI KUIONDOA CCM MADARAKANI...KIU YETU NI KUJENGA NIDHAMU TUHESHIMIANE,MTU AKIINGIA MADARAKANI AJUE FIKA KUWA IPO SIKU AKIVURUNDA ATATOKA,NA HATA UKAWA TUKIFANIKIWA KUINGIA NA MKAVURUNDA HATUTA WANG'ANG'ANIA TUTAWAPIGA CHINI TU BILA KUJALI WE NI SLAA AU NANI. BUSARA LAZIMA ITANGULIE KWA KUANGALIA MASLAI MAPANA YA MATAKWA YA WANANCHI,HAKUNA SEHEMU MAMBO YANAKUWA SAWA TU KILA SIKU KWA KILA KITU. SLAA ANAPASWA KUELEWA KUWA HAPA TUNAPIGANIA NINI. HIVI KIPI CHA MSINGI KWA SASA KWAKE? CCM KUBAKI MADARAKI KISA YEYE AKUBALIANI NA MAONO YA WENGI KTKA CDM NA UKAWA?JE ,ANAONA NI VEMA AKARUDISHA NYUMA JUHUDI ZA KUITOSA CCM KISA HAMTAKI LOWASA? ANAONA CCM IBAKI KISA MASHARTI YAKE NA HOJA ZAKE HAZIKUFANIKIWA KUMZUIA LOWASA.
NAOMBA NIACHE UNAFIKI BINAFSI NAAMINI LOWASA ANAMCHANGO MPANA SANA NA UWEZO MKUBWA SANA WA KUWAONDOA CCM MADARAKANI..

DR KAMA UNAENDA NENDA TU SISI TUTAENDELEA KUWA PAMOJA NI KWELI KUWA KUNA MADHARA KUINDOKA KWAKO ILA NI.MADOGO KULIKO UNAVYOTAKA IWE..KWELI KUNA HASARA KUONDOKA KWAKO LAKINI HAIZIDI MATWAKWA YETU WANANCHI YA KUITOA CCM MADARAKANI..NI KWELI TUNAKUHESHIMU ILA HATUTOKUFATA..
TUMWACHE LOWASA ACHUKUE NCHI HII TOKA KWA CCM MENGINE YANAFATA MSTARI YENYEWE.
ASANTE MHESHIMIWA DR SLAA NAKUTAKIA SAFARI NJEMA ISIYO ILA ISIFANIKIWE KAMA INALENGO LA KUIBAKISHA CCM MADARAKANI
 
Najuwa mna hasira sana kwa ukimya wa dr slaa ila tuweni wavumilivu kidogo tuone mwisho wake,kama naye kaamuwa kuwasaliti watanzania basi tujue kimoja
 
Yaani kati ya aliyekitumikia chama na aliyekiuza chama unasema nani kasalitiwa na kusaliti? Mmemdhihaki sana huyu Mzee kisa pesa
 
inakera sana kuona mtu anayelewa malengo ya upinzani naye analeta uponzani ni bora aende tena mapema tu ili tutakapoanza tuwe tumeanza safari yenye uhakika
 
we uelewi na huto elewa inaonekana hata mwalimu wako drsan alipata tabu pole ... ila sisi hatuangalii nani kafanya nini? ila nani anamalengo gani juu ya kuwaondoa nyie ccm.
binafsi hata aje shetani ilimradi lengo lake ni kuiondoa ccm madarakani nitamsapoti...hapa najenga heshima..na kumbukeni ni vigumu mtu mwema kuendelea kuwa mwema katika kundi la waovu vibaka kama ccm ila ni rahisi mno kwa mwovu kuwa mwema ndani ya kundi la watu wema.
 
naanza kupata wasiwasi na ile kadi yake ya ccm ambayo bado anayo hivi yeye anaweza kutueleza kilicho mtoa council of bishops pale kurasini kutoka padre mpaka kuwa civilian ? no one is perfect kama bwana yesu aliweza kukaa na wakosaji na makahaba hakuwatenga itakuwa yeye cdhani kama kamati kuu ya cuf ,nccr mageuzi ,NLD wote mpaka wameridhia lowassa kuwa presidential candidate wa ukawa hawakujua threat za lowassa kwa umoja wetu hivi mzee unajua chain in command ww hivi kipandi uko padre ukipokea amri kutoka kwa papa unaweza kuipinga?
 
Yaani kati ya aliyekitumikia chama na aliyekiuza chama unasema nani kasalitiwa na kusaliti? Mmemdhihaki sana huyu Mzee kisa pesa

Mim binafsi nilikuwa nataman Lowassa akatwe ccm na sikuwa na wazo kama atakuja Chadema, lakn baada ya tetesi niligundua kule kumpinga kwangu kulikuwa ni uwoga kwamba angepita Ukawa tungepata shida sana japo na kumsema kwamba ni fisad nina amani na ujio wake kwakweli Slaa usitugawe
 
naanza kupata wasiwasi na ile kadi yake ya ccm ambayo bado anayo hivi yeye anaweza kutueleza kilicho mtoa council of bishops pale kurasini kutoka padre mpaka kuwa civilian ? no one is perfect kama bwana yesu aliweza kukaa na wakosaji na makahaba hakuwatenga itakuwa yeye cdhani kama kamati kuu ya cuf ,nccr mageuzi ,NLD wote mpaka wameridhia lowassa kuwa presidential candidate wa ukawa hawakujua threat za lowassa kwa umoja wetu hivi mzee unajua chain in command ww hivi kipandi uko padre ukipokea amri kutoka kwa papa unaweza kuipinga?
Leo huku jukwaani kuna nondo za maana sana.
Big up mkuu, nimeipenda hoja yako.
 
naanza kupata wasiwasi na ile kadi yake ya ccm ambayo bado anayo hivi yeye anaweza kutueleza kilicho mtoa council of bishops pale kurasini kutoka padre mpaka kuwa civilian ? no one is perfect kama bwana yesu aliweza kukaa na wakosaji na makahaba hakuwatenga itakuwa yeye cdhani kama kamati kuu ya cuf ,nccr mageuzi ,NLD wote mpaka wameridhia lowassa kuwa presidential candidate wa ukawa hawakujua threat za lowassa kwa umoja wetu hivi mzee unajua chain in command ww hivi kipandi uko padre ukipokea amri kutoka kwa papa unaweza kuipinga?
CHADEMA kwa sasa hawana ubavu wa kumnyoshea kidole Lowassa na timu zake.

Lowassa kwa sasa ni chama ndani ya CHADEMA.

Hukumuona Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa anavyo mnyenyekea Lowassa mpaka anamsindikiza Lowassa kwenye gari yake wakati yeye ni mwenyekiti wa CHADEMA Taifa.

Kiitifaki, Lowassa inabidi amsindikize mwenyekiti wa chama taifa kwa sababu Lowassa ndani ya CHADEMA ni mwanachama tu na hana cheo chochote. Kwa sasa ni kinyume chake!

Pesa na umaarufu wake ndiyo unawafanya viongozi wakuu wa CHADEMA wajishushe chini yake.

Money talks and money alone sets the entire world in
 
Tukiweka itikadi za vyama pembeni umeongea ukweli. Ukweli ambao wanaukawa wengi hawataki kuusikia
 
Mim binafsi nilikuwa nataman Lowassa akatwe ccm na sikuwa na wazo kama atakuja Chadema, lakn baada ya tetesi niligundua kule kumpinga kwangu kulikuwa ni uwoga kwamba angepita Ukawa tungepata shida sana japo na kumsema kwamba ni fisad nina amani na ujio wake kwakweli Slaa usitugawe

naungana nawe watu wengi tulikuwa na woga sana..tulifurahi alipokatwa kwa kuwa tulikuwa tukisika watu wanavyoongea mitaani na wala hatukudhani kama atakuja kwetu..Alipokuja nikajua kazi imeisha
 
CHADEMA kwa sasa hawana ubavu wa kumnyoshea kidole Lowassa na timu zake.

Lowassa kwa sasa ni chama ndani ya CHADEMA.

Hukumuona Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa anavyo mnyenyekea Lowassa mpaka anamsindikiza Lowassa kwenye gari yake wakati yeye ni mwenyekiti wa CHADEMA Taifa.

Kiitifaki, Lowassa inabidi amsindikize mwenyekiti wa chama taifa kwa sababu Lowassa ndani ya CHADEMA ni mwanachama tu na hana cheo chochote. Kwa sasa ni kinyume chake!

Pesa na umaarufu wake ndiyo unawafanya viongozi wakuu wa CHADEMA wajishushe chini yake.

Money talks and money alone sets the entire world in

maswala ya ubosi yapo kwenu ccm na ndo maana mnatuumiza ,mnapenda sana ubosi matokeo yake nchi imewashinda jamaa anaonyesha kumkubali ili nasi tumkubali,upaswi kuwa na Phd kujua hili ile ni mbinu ya ushawishi na kuonyesha kuwa ubosi ni ujinga unapotafuta mafanikio.
mambo ya uboss tunawaachia nyie sie tunataka utendaji uliotukuka
 
Slaa anasahau kuwa naye alikatwa ccm na kuja chadema na kupata ubunge!pia Mbowe alikubali kumwachia urais iweje yeye ang'ang'anie?? Dr.W.Slaa
 
Last edited by a moderator:
CHADEMA kwa sasa hawana ubavu wa kumnyoshea kidole Lowassa na timu zake.

Lowassa kwa sasa ni chama ndani ya CHADEMA.

Hukumuona Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa anavyo mnyenyekea Lowassa mpaka anamsindikiza Lowassa kwenye gari yake wakati yeye ni mwenyekiti wa CHADEMA Taifa.

Kiitifaki, Lowassa inabidi amsindikize mwenyekiti wa chama taifa kwa sababu Lowassa ndani ya CHADEMA ni mwanachama tu na hana cheo chochote. Kwa sasa ni kinyume chake!

Pesa na umaarufu wake ndiyo unawafanya viongozi wakuu wa CHADEMA wajishushe chini yake.

Money talks and money alone sets the entire world in
Sasa wewe unaweza kulinganisha huyo babu na lowassa
 
aende zake Lissu alisema ni kichaa mtu ambaye hataki kuona nguvu ya Lowasa ndani na nje ya CCM Slaa aende tu
 
inakera sana kuona mtu anayelewa malengo ya upinzani naye analeta uponzani ni bora aende tena mapema tu ili tutakapoanza tuwe tumeanza safari yenye uhakika

Dr. Slaa awezi kuvumilia ujinga kama huu unaoendelea kwa sasa.
 
Back
Top Bottom