[h=2]
Nakubali mahakama ya kadhi[/h]
Kama kichwa cha habari kilivyoonyesha hapo juu, mimi napenda kutoa ukweli wa moyo wangu leo.
Nakubali waislam waanzishe mahakama ya kadhi kwa sababu ya umuhimu mkubwa wa uwepo wa mahakama hiyo, uwepo wa mahakama ya kadhi utasaidia waislam kufuata sheria zinazoendana na imani yao.
Kila jambo linalowahusu waislam litafanywa bila kutatiza maadili yao.
Pamoja na hayo niliwaza uwepo wa mahakama hiyo bila kuwekwa kwenye katiba ili kuepusha:
1.mambo yanayoweza kuvuruga mshikamano wa raia, kwa kuleta dhana kwa kila mtu kwamba kumbe sisi tuko tofauti sana, hii itaongeza ubaguzi.
2.kuwafanya watu wasio waislam kufikiri kwamba serikali inafungamana na dini flani hapa nchini.
3.watu wasio waislam kufikiri kua mahakama hii ititatumia fedha zinazochangiwa hadi na watu wawasiokua waislamu
4. Watu wasio waislamu wanawaza kua uwepo wa mahakama ya kadhi kutaashiria kua uislam ni sehemu ya dora (serikali).
Kwa mtazamo wangu naomba iwepo ila isiingizwe kwenye katiba.
Wadau tafadhali haya ni mawazo yangu naomba nisiulizwe dini yangu, wala nisipewe matusi kwa sababu ni fikra zangu sio lazima kila mtu awaze kama mimi.
Naomba kuwasilisha.
Watanzania wenzangu kila kitu kina uhalisia wake.Duniani kote wanadamu wanazo tofauti za kila aina ,lakini pia kuna mambo wanayofanana .Pamoja na hayo yote munaweza kufanana katika jambo fulani na mukakosan kwenye jingine.huu ndio uhalisia wa viumbe wote tulivyoumbwa na Muumba wetu.
Mfano.wa mafanano yetu makuu ni haya.
1.kundi lakiumbe mtu wote tunafanana kama binadamu.
2.Kula,kunywa,na kuenda haja,kulala,furaha na huzuni nk tunafanan.
3.Hisia wete tuna hisia bili tunatofautiana tuu.
4.Kupena au kuchukia na mengi ya kiutu tunafanana
Lakini ukiingia ndani zaidi ya hapo utaona tunatofautiana kimaumbile,sura,utashi,na hata imani zetu za kidini pamoja na kuwa tunaweza tukawa na imani moja kwa kundi fulani mfani Waislamu,lakini kwa undani kila mtu ana upeo wa uamini wake tofauti na mwengine.
Hivi kweli sisi ni wamoja ?
Swali hili linahitaji uangalifu sana,kulijibu,lakini kwa haraka haraka sisi si wamoja.
Wewe ni mkiristo hawa ni waislamu.
Wewe ni mtanganyika na hawa ni wazanzibari.
wewe ni mnywa pombe na mla nguruwe na wale ni wala nyama za watu na vibudu na wengine Vegeterians.
Kwa hiyo basi Taifa linapoandika katiba inayohitajiwa na watu wenye mchanganyiko kama huu,ni lazima iangalie mmambo yanayo tuunganisha wote,na kisha iangalie makundi makubwa, halafu izilinde haki za makundi madogo madogo bila ya kuathiri uhuru wa mtu mmoja mmoja.
KWA MSINGI HUU NDIPO INAPOKUJA HOJA YA MAHKAMA KAMA ZA BIASHARA,ARDHI,KAZI NA ILE YA KADHI ambazo zitayahusu makundi husika tuu.Kufanya hivi ni kurahisihsa utawala na kuwafikia watu wote kwenye makundi yao.
Mbona sijawahipo kusikia kuwa Mahakama za Biashara zikipingwa wakati Kundi la wafanya biashara Tanzania ni dogo tu.
wafanaya kazi nao mahakama yao inagharamiwa na watanzania wote ilhali wengine hata hizo kazi hawana?
Mahakama ya Ardhi ni kwa wale wanaomiliki ardhi tu . nk
ZINDUKA MSOMI MWENZANGU, HIVI KARIBUNI KUTAKUWA NA MAHAKAMA YA WANAWAKE NA WATOTO UNAJUWA HILO.
JEE WATANZANIA WOTE NI WANAWAKE?
lakini kimsingi sisi ni Watanzania kwa umoja wetu ila tunazo tofauti zetu kubwa tuu za kimakundi.hapa umoja wetu ni wa Kiutaifa tuu si wa kidini,wala kikabila.Ndio maana makabila mengi hapa Tanzania yana umoja wao wa kimaendeleo,misiba na majanga.Haina maana wanavunja umoja wa kitaifa bali naamini ndio wanauimarisha,.
Umoja wa kitaifa unaoutaka wewe hauwezekani kwani kharama yake ni kubwa mno kwa kuzikandamiza haki za Imani za dini yenye kundi kubwa nchini.