Nakaribia kuoa ushauri tafadhali

Nakaribia kuoa ushauri tafadhali

Ukishaoa ukitulize...sio uoe ubaki macho juu juu.....

Makundi na marafiki wa ajabu punguza na delete

Shikamana na mkeo mfikie ndoto zenu na kujenga familia bora

Hakikisheni nyumba yenu inatawala upendo, uvumilivu, kusameheana, kuheshimiana, kusaidiana, kuchukuliana, kuaminiana na mumtangilize Mungu kwenye kila jambo.....wanandoa msichoke kuombeana

Tabia ya kurudi usiku mwingi acha..... dharau na kauli mbovu zisiwepo....

Mwisho mke hapigwi ngumi.....anapigwa na Vanguard au Fortuner

Umesema vema, nkitaka kuoa ningependa kusoma na kukumbuka kauli hii....

My dada kipenzi
 
Mkuu, mengi yamesemwa ila kumbuka wazazi wako pia walio kusaidia kukufikisha hapo ulipo.

Ndoa ni agano tafatifu, jaribu kuwa mtakatifu kabla ya kuingia huko.

Kila la kheri mkuuu...
 
HONGERA.....ila ujue unaenda kumilikiwa,,, uwe mvumilivu.....uhuru wako , maisha yako.....
 
Nimelia kwa uchungu. Kuna mdogo wangu alimaliza elimu yake vizuri na kupata kazi katika moja ya taasisi nyeti Serikalini. Akaomba ushauri anataka kuoa, kaka zake tukamsihi umri ulikuwa bado avute subira ayajue mambo ya mabinti wa zama hizi za Wasapu na Ista. Alioa May mwaka huu na ndoa imevunjika November mwaka huu. Kisa ni vigisu za kwenye ndoa na nature ya kazi ya bwana mdogo. Ingia kwa akili sana mdogo wangu, otherwise Utatuletea kilio humu.

Dah pole kwa mkasa uliokupata nategemea kwangu itakuwa tofauti Mungu anisaidie..
 
Je kama alimpata kwenye Pombe? Kuna mdada nliachana nae Sept nae anaolewa tar 8 ya kwako ni wapi mkuu ili nikupe ushauri vzr.

Hapana sinywi kilevi chocho wala sivuti hata sigara na yeye ni hivyo hivyo
 
Mkuu, mengi yamesemwa ila kumbuka wazazi wako pia walio kusaidia kukufikisha hapo ulipo.

Ndoa ni agano tafatifu, jaribu kuwa mtakatifu kabla ya kuingia huko.

Kila la kheri mkuuu...

Ahsante mkuu
 
Ndoa raha sana,
Mkipendana kwa dhati,
Mkisikilizana,
Mkishauriana,
Mkijuana tabia,

Pendelea kusema ahsante hata akikubusu,
Ukiona hana raha mfariji na kama umemkosea wahi kusema samahani inayotoka ndani ya moyo wako,

Ndoa ni nzuri, coz ni maisha kama maisha uliyokua unaishi na dada au kaka zako,
Utani, ucheshi, kuelimishana, kuchokozana, kudekezana n.k

Kila la kheir katika safari yako ingine ya maisha.

By the way hakuna kadi ya mwaliko jamani.
 
Shukrani kwa nasaha zako kuhusu kadi ondoa shaka
 
Dah pole kwa mkasa uliokupata nategemea kwangu itakuwa tofauti Mungu anisaidie..

Mkasa haukunipata mimi Bali ulimpata mdogo wangu kitinda mimba wa mama yetu. Mungu akuongoze Aisee.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom