Nakaribia kuoa ushauri tafadhali

Nakaribia kuoa ushauri tafadhali

Hongera ndoa ni taasisi inayohitaji busara na ukomavu kwa pande zote. Na lililo kubwa kuvumiliana katika mapungufu maana hamna aliyemkamilifu.

Kama umepata chaguo sahihi naamini utakuwa na maisha ya furaha.
 
Ukishaoa ukitulize...sio uoe ubaki macho juu juu.....

Makundi na marafiki wa ajabu punguza na delete

Shikamana na mkeo mfikie ndoto zenu na kujenga familia bora

Hakikisheni nyumba yenu inatawala upendo, uvumilivu, kusameheana, kuheshimiana, kusaidiana, kuchukuliana, kuaminiana na mumtangilize Mungu kwenye kila jambo.....wanandoa msichoke kuombeana

Tabia ya kurudi usiku mwingi acha..... dharau na kauli mbovu zisiwepo....

Mwisho mke hapigwi ngumi.....anapigwa na Vanguard au Fortuner
 
Dah..mkuu tumtangulize mungu mbele maana hata mm naoa january 8..hongera kwa kupata wako.
 
Bora usingeomba ushauri humu. Utakatishwa tamaa mpaka ufurahi. Follow your heart...utakayoyakuta huko kwenye ndoa muombe mungu akupe busara. Thats it!
 
Mkeo hatakuwa malaika, ni mwanadamu kama wewe hivyo usitegemee mazuri tu kutoka kwake, jitahidi kumfundisha kile unachokiona ni kizuri kwako ili akitende na jitahidi kutenda wema zaidi kuliko kutegemea wema aumazri kutoka kwake tu.
Kukitokea migongano jitahidi kusuluhisha wewe kwanza kabla ya yeyote na ikishindikana pima ni nani wa kumshirikisha katika matatizo yako ya kifamilia,sio kila mtu anafaa kuelezwa matatuzo ya kifamilia,
(Kuwa kwake mtumwa atakuwa kwako kijakazi)
 
Januari 8 naingia katika ndoa panapo majaliwa nataka ushauri pamoja na nasaha.

unaoa kabira gani?
tuanzie hapo kwanza.
je umejiandaa kulea mimba za wanachuo/wafanyakazi/ma ex wake!
...ntarudi badae kuchukua kadi ya harusi!
 
Kuna kale kawimbo ka vijana wa arusha wanajiita sijui weusi...kawimbo kana ujumbe mzuri sana nadhani katakufaa ukikasikiliza kwa umakini....baba swalehe
 
Hongera kaka...ni uamuzi wa busara na hekima

Jitahd kuheshim mke wako...ila usimwamini 100%.
 
Januari 8 naingia katika ndoa panapo majaliwa nataka ushauri pamoja na nasaha.

Elewa ndoa sahihi ni ile iliyofungwa mukiwa waislamu otherwise kwa kama mumefunga kwa dini nyengine mtakuwa munafanya maasi tu.
 
Kama unaamini ktk sala/dua/maombi fanya hivyo mpaka siku mnakaa pamoja funga inapobidi ili muweke msingi mzuri wa ndoa yenu na vizazi vyenu
 
Januari 8 naingia katika ndoa panapo majaliwa nataka ushauri pamoja na nasaha.

Nimelia kwa uchungu. Kuna mdogo wangu alimaliza elimu yake vizuri na kupata kazi katika moja ya taasisi nyeti Serikalini. Akaomba ushauri anataka kuoa, kaka zake tukamsihi umri ulikuwa bado avute subira ayajue mambo ya mabinti wa zama hizi za Wasapu na Ista. Alioa May mwaka huu na ndoa imevunjika November mwaka huu. Kisa ni vigisu za kwenye ndoa na nature ya kazi ya bwana mdogo. Ingia kwa akili sana mdogo wangu, otherwise Utatuletea kilio humu.
 
Ukishaoa utulie sasa. Usianze mambo ya kuchepuka chepuka au kuendekeza pombe... Kila la kheri katika ndoa yako. Uwe na maisha ya furaha na amani...
 
Ukishaoa utulie sasa. Usianze mambo ya kuchepuka chepuka au kuendekeza pombe... Kila la kheri katika ndoa yako. Uwe na maisha ya furaha na amani...

Je kama alimpata kwenye Pombe? Kuna mdada nliachana nae Sept nae anaolewa tar 8 ya kwako ni wapi mkuu ili nikupe ushauri vzr.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom