Najuta kuwekeza kwenye kiwanja na nyumba ya mwanamke

Azoge Ze Blind Baga

JF-Expert Member
Mar 8, 2019
366
1,377
Wana MMU,

Naandika huu uzi kwa masikitiko na kujuta bora ile pesa ningenywea tu bia na kula kitimoto.

Nina mke na watoto, mke alikopa hela bank na kazini kwao akanunua uwanja. Ushauri huu nilimpa mimi

Nikasimamia ujenzi nyumba ikasimama ingawa kuna vitu vilikuwa havijakamilika nikaanza kuingia gharama kumalizia nyumba.

Kipato changu cha kuunga unga ila kwa kutambua nyumba ni ya familia tuna watoto na ndoa tumefunga nikaona niendeleze ukarabati.

Sasa bwana umetokea mgogoro mdogo mimi na mke wangu kanitamkia hapa sijachangia chochote kodi yote anakula yeye.

Basi nimeamua nianze mdogo mdogo kujitoa kwenye hii nyumba.

Mchango wangu hajauthamini kabisa mwanamke amekua mbinafsi ghafla sana.

Wakuu tuwe makini kuwekeza hela na muda wako kwenye mali ya mwanamke ni kujichimbia kaburi.

KATAA NDOA
NDOA NI UTAPELI
 
Back
Top Bottom