Najuta kuoa hususani katika umri mdogo nilionao

colin_morgan

JF-Expert Member
Jun 8, 2015
2,443
2,896
Habari wakuu,

Natumai mko na furaha na amani tofauti na mimi. Hapo nyuma nilikuwa nawashangaa sana vijana wengi tu ambao wanaponda sana kitu kuoa. Nilikua nikiwabeza sana na kuhisi kama wamechanganyikiwa hivi kutokana na experience yangu katika ndoa kwani ilikuwa ni maisha mazuri sana na yenye amani mno.

Ila sasa najutaa, nasema tena najutaaaa! Mimi ni kijana wa miaka 28 na ni muajiriwa Serikalini. Pia najishughulisha na uwekezaji katika kilimo so kipato changu ni cha wastani sio kibaya kihivyo. Kisa cha kuleta huu uzi ni mke wangu kuwa na tabia za ajabu za kununa nuna kila siku bila hata ya sababu ya msingi. Akinuna anakaa siku mzima hanisemeshi na kunitumia sms za vitisho na kunishikilia kwamba nimuache ingawa huwa simjibu lolote.

Jana kuna workmate wangu (me) ambaye ni jirani yetu, mke wake amepata dharura kidogo so hayupo. Wakati natoka job nikaona si mbaya kwa vile nilimsikia anataka kwenda hotelini kula nikaona niongee na wife ili aje kupata chakula cha mchana tu home. Tatizo lilianzia hapo. Wife hakuridhika na hilo akaniambia hataki, kwanini sikumpa taarifa mapema? Ila nikamuelewesha kama imekuwa ni dharura na kwa vile ni chakula cha mchana tu haina shida.

Akakubali ki roho upande ila akanihakikishia kwamba chakula kikiwa kidogo usiku yeye hatopika tena chochote kile kwani amechoka. Nikakubaliana na yeye yakaisha, jamaa akaja kula na kuondoka. Usiku tumekaa mezani tunataka kula wife akaanza kulalama kwamba chakula kimekuwa kidogo na kwa sababu nilileta mtu bila mpangilio. Nikamuambia “wewe kula mimi usiku sipendi chakula kizito so nitakula bites tu”

Bado akawa analalama, nikamuambia hivi mbona nyinyi wanawake huwa mnajali sana kuhusu chakula? Heee! Kesi ilianza hapo yaani aligoma kula na hadi sasa ninavyosema hajala. Hakulala chumbani na nahisi kampigia mama yake kumpasha uongo kwamba namnyanyasa. Yaani hivi ninavyokuambia nipo kazini ila hizo sms zinazoingia kwamba sijui nimuache, sijui nikirudi leo yeye sitomkuta na keshanielekeza ambapo nitakuta funguo ya nyumba na maneno kila aina kwa kweli.

Yaani kama kawaida principle yangu mimi huwa sijibu sms za kijinga (nipo tu kimya). Asubuh nilijihudumia kila kitu nikatoka kuja kazini. Sasa najiuliza kosa langu mimi ni lipi hapo? Yaani najuta, umri huu nilitakiwa nile bata na kutumia ujana wangu vizuri ila daily stress za kipumbavu tu yaani kila siku mtu ananunanuna bila sababu za msingi. Yaani nimechoka nasubiria nikipigiwa simu na wakwe tu basi natoa talaka direct.

=====
MAONI YALIYOTOLEWA NA WADAU:

--------------
--------------
--------------
--------------
--------------
--------------
--------------
 
1.Mkeo mchoyo huyo
2. Ana mambo mengi sana
3. Hana heshima
4. Alitafuta sababu muda mrefu tu, hiyo ya chakula imebust tu.
5. Usiweke kumwamini, huyo kuna kitu kina msukuma. Hawezi kudai kuachana bila mtu anayemhadaa!

Dah! Maisha haya bhaana!
Wakati unawaza kumtimua wife, mimi nawaza mwakani nikimpata nioe!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mambo madogo sana hayo mkuu. Huna haja hata ya kupokea pole.

Communication baina yenu ndio tatizo na pmoja na ww kutosimamia nafas yako vyema. U have to agree in mtters regarding family orientation but whn u think u r not in gud terms, then u have to stand on what u think (n u r sure) is right.
Be bold ( not bull) in ur decisions and stand firm to show ur wife the right path.

Kuish na mwanamke unahitaji akili tu wala sio nguvu. Acha kujitia mawazo kwa mambo unayopaswa kuysimamia na kuhakikisha yanaenda sawa. Dig deep down to what is the root probem.

Kuhusu kukutumia message za kutishia pia mpe shule tu kuwa ni hatari sana kwake yeye mwenyewe.Maana hata lilitokea jambo baya kwako asilohusika yeye, hali itakua mbaya kwake.

Mikosi huwa inasubiri ufungue mlango tu iingie kuwatafuna, sasa ajitahid asiipe nafasi.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…