Najuta kumpa mwili wangu auchezee atakavyo

Story fupi yenye mafunzo kwenu wanawake.


Nilipoingia katika mahusiano naye nilimuamini, nikampa kila kitu nilichoweza. Nakumbuka enzi zile nyumbani tulikuwa tuna ngo'mbe, niliiba maziwa kila siku na kumpelekea kwao. Akanenepa!
Penzi letu likawa huru alipoanza maisha yake mwenyewe. Sikuwa najua lolote kuhusu mapenzi. Alinifundisha. Nikaegemeza maisha yangu yote kwake.Akanifanya nikawa mtumwa wa ngono kila nikienda chumbani kwake.

Kama haikutosha sasa akaanza kunifundisha kunywa pombe. Niliamini kuwa ndiye mume wangu mtarajiwa, kwa nini nikatae? Nilimkubalia kila kitu.

Alinilazimisha ngono hata nilipokuwa katika siku zangu. Kweli nilikuwa msomina niliyajua madhara ya kufanya hivyo lakini sikutaka kumuudhi huyo niliyeamini kuwa ni mume wangu.

Nilipenda tututmie kinga lakini aliipinga sana. Nikapata mimba ya kwanza! Hakuwa na pesa lakini alinilazimisha niitoe. Nikaiba pesa nyumbani nikafanyaalivyotaka. Kwa mara ya kwanza nikatoa mimba.

Haikuniuma sana! Niliamini kuwa ni yeye atakuja kunioa na atanifichia aibu hii. Nilitegemea sasa tutaanza kutumia kinga. Lakini hapana haikuwa hivyo. Aliendelea kunilaghai. Tayari aliujua udhaifu wangu. Alinishika hapa na pale. Nikishtuka tayari amefanya anavyojua.

Pombe kidogo na nyingine kidogo. Nikazoea lakini nikawa nawahi kulewa. Akautumia udhaifu huu kunifanyia jambo baya lililonifanya niandike haya kwako. Akaniingilia kinyume na maumbile. Alinilawiti!

Nilishindwa kumshtaki popote. Nikavumilia kwa kuwa alikuwa mume wangu mtarajiwa. Mume asiyejulikana hata kwa wazazi. Mchezo ule ukaendelea. Akajitetea eti hataki nipate mimba tena, hivyo hiyo ni mbinu mbadala. Najuta kumuamini lakini huyo alikuwa mume wangu.

Miaka ikapita, ule urembo wangu niliozoea kuuona katika kioo ukatoweka, simu za mara kwa mara kutoka kwake zikatoweka, akawa mkali sana kwangu. Hakutaka niende kwake. Wakati huo nilikuwa nasoma chuo.

Pesa ya mkopo ikitoka ananitafuta na tunakuwa marafiki tena. Anasema ananipenda na atanioa. Ananilewesha na kunitumia kinyume na maumbile. Pesa ikiisha na mapenzi yanaisha nabaki mwenyewe katika msoto. Sasa akaanza kubadilisha wasichana waziwazi. Ningesema nini mimi?

Ninajua alishindwa kusema neno moja tu. Tuachane! Nilijua tayari ameniacha! Afya yangu ikadolola sana, nikalazimikakwenda kupima hospitali. Sikuwa na virusi. Nikapewa ushauri nikautumia. Siku zikasonga nikampata mwanaume mwingine. Huyu alikuwa ananijali sana. Nikaanza kumsahau yule aliyenitenda.

Nilipomaliza chuo akajitambulisha nyumbani na alitaka kunioa. Akanio kweli. Maisha yakaanza. Mwaka wa kwanza, mwaka wa pili na hadi wa tatu. Sikuwa nabeba mimba. Mume wangu alikuwa mvumilivu sana, hakuwa hi kunilaumu. Lakini niliumizwa na mawifi. Nikaamua kwenda hospitali.

Nikaambiwa kizazi change kiliharibiwa kwa kutoa mimba mara kwa mara. Pia mapenzi ya kinyume na maumbile yamenivuruga kabisa. Nililia sana huku nikimkumbuka yule aliyeuleta uchungu huu kwangu.
Dunia haikuwa mahali pangu sahihi.

Nimekuandikia barua hii mdogo wangu.Uisome mwenyewe!! Lakini uwasimulie wengi baada ya kifo changu. Uwasimulie bila kuchoka wasichana wa kileo wanaodanganyika na kufanya mambo magumu kuwaridhisha wapenzi wao. Waambie watakufa kwa mateso kama mimi.

Wasipokusikiliza usijisikie vibaya maana hata mimi nilikuwa siwasikilizi watu waliponambia lolote kuhusu yule mumemdanganyifu. Sitajiua lakini nitakufa kabla ya wakati!

Nimekuandikia wewe kwa kuwa u mwandishi. Japo kwa sasa u mtoto mdogo najua utaipata nafasi siku moja ya kuwafikishia wasichana hawa.

Usilie kwa sababu nitakufa. Lia kwasababu mwanaume mwenzako amenitenda hivi!

shida inaanza dunia ya sasa imekuwa kama paka na panya kuviziana. Hii imetokana na watoto wa kike asilimia kubwa kuwachezea wanaume kwa kupenda wawahudumie na mwisho wa siku kuwatosa. Unakuta binti anataka i phone mara sijui nini na hapo unakuta pengine mmepangwa hata wanaume 10 kila mmoja na huduma yake anayoombwa. Sasa vijana nao siku hizi wameshashtuka hiyo michezo kwahiyo kilichobaki ni timing tu mbzui kala mbuzi yaani nani anakaye muwahi mwenzie ndiyo hali halisi ilivyo, Hii hali kiukweli siyo nzuri maana tunapoelekea hata ndoa zitakuwa hazipo au zikiwepo ni za muda mfupi ambapo ni jambo la hatari sana.Pole kwa yaliyokusibu ila chaanzo ni hicho vijana wengi sana wamelizwa kwa tabia za kuombwa wakiamini wamepata wenza kumbe siyo.
 
Back
Top Bottom