Najuta kumkataa

Sabaganga

Member
May 15, 2023
19
45
Katika harakati za kutafuta mke wa kuoa, classmate wangu mmoja ni mwanamke aliniunganisha na mfanyakazi mwenzake ni mwalimu.

Kweli tukapanga nikaenda kuonana nae mchumba mtarajiwa nyumbani kwao kabisa. Kwao maisha mazuri, na mtoto mwenyewe alikuwa ni mshika dini.

Lakini sikuvutiwa na muonekano wake kwa hivyo sikuendelea na mchakato wa kumuoa. Hiyo ni kama miaka 15 iliyopita.

Hivi sasa nina mke na watoto wawili lkn nimemkumbuka yule mchumba naona nilikosea kwani nimejua kuwa mambo ya muonekano kwa mwanamke utaeishi nae kwenye ndoa si muhimu ispokuwa ni akili na awe na tabia njema.
 
Back
Top Bottom