Hahaha mkuu kloro nachapa usingizi nitarudi kesho tuendeleze hii mada
Nina wasiwasi na derevea...
Dereva e ndugu yangu, eleza ulikosoma,
Elmu yatoa ukungu,sharti uishike vema,
Ni kama wa ndizi mkungu, hakika utasimama,
Umesomea wapi udereva? Una leseni gani?
Vyuo vya uchochoroni, na NIT hapo ubungo,
Vingine vya redioni, havichemshi ubongo,
Hawapo barabarani, kuonesha kwa vitendo,
Umesomea wapi udereva? Una leseni gani?
Leseni kila aina, wewe yakwako ni ipi,
Ulipata kiaina, eleza lipata vipi,
Tupe ujumbe kwa kina, sije lipata ka pipi,
Umesomea wapi udereva? Una leseni gani?
Kuna za makaratasi, leo zipo za kuswapu,
Karatasi ka patasi, lazima pige pushapu,
Najua hata wa Nkasi, lifika zama kishapu,
Umesomea wapi udereva? Una leseni gani?
Alikuletea mjomba, jasho hata hukutoa,
Ukiendesha ka komba, kote kote unayumba,
Hata nyepesi ka pamba, wasiwasi nakushika,
Umesomea wapi udereva? Una leseni gani?
Lengo kukuelimisha, haya mambo ni mafunzo,
Naona ulichemsha, mtaani meacha gumzo,
Jaribu kubadilisha, mbinu kuondoa mzozo,
Umesomea wapi udereva? Una leseni gani?
Hahahaha.....! Usije ukawa ulikula chumvi....!
Kloro wacha vioja, naomba nisaidie
Mwanzo ulitoa hoja, jipya nijipatie
Vipi tena wakoroga, lazama jichukulie
Mwanzoni ulinambia, jipya nijipatie
Safari siwezi fika, kwa gari ilo chakavu
Je vipi likipinduka, nikavunja zangu mbavu
Nataka la uhakika, mimi dereva shupavu
Mwanzoni ulinambia, jipya nijipatie
Gari zilizotumika, vishindo hazihimili
Vipi utasafirika, kuweka gia ya pili
Mwishowe taghadhibika, yanini nijikatili
Mwanzoni ulinambia, jipya nijipatie
kila niliyoliona, zamani lilitumika
Ukitaka piga kona, gari lafanya koroma
Kwa kweli mtaminyana, bado gari litagoma
Mwanzoni ulinambia, jipya nijipatie
Hivi mpya ziwapi, kote nimehangaika
Mengi ya sasa makapi, yaani ni patashika
Maisha sasa mafupi, madereva twatabika
Mwanzoni ulinambia jipya nijipatie
Jipya likipatikana, hilo la mwanzo chaguo
Kwavile adimu sana, umethibitisha hilo
Iweje tena wakana, lilotumika chipuo
Jipya halipatikani , lilotumika hulitaki?
Ulikiri kudanganywa, eti jipya latoka japani
Mapesa ukanyang'anywa, kumbe lavuja jamani
Sasa nini kitafanywa , nimekwama klorokwini
Jipya halipatikani , lilotumika hulitaki?
Kuna yale ya zamani, madhubuti nakwambia
Jinale volkswageni , kwa safari aminia
Hata kipata Nissani, Wala hutoijutia
Jipya halipatikani , lilotumika hulitaki?
Karata nairejesha, kwako ewe wa ganzi
Meshindwa kusuluhisha, ni gumu lako chaguzi
Nachelea kuchemsha, bora fanya maamuzi
Jipya halipatikani , lilotumika hulitaki?
Mwenzenu nilitamani, gari kulisafiria
Laonyesha la thamani, kwa nje na ndani pia
Kiumbo li wastani, mfano wa gari KIA
Gari hili gari gani, najuta kulipandia
Gari hili lavutia, kwa hilo nakubalia
Rangi yake kahawia, machoni imetulia
Wengi wanaliwazia, na sifa kulisifia
Gari hili gari gani, najuta kulipandia
Kilitazama kwa mbele, pembeni limetanuka
Utapatwa na vipele, mwilini kusisimka
Natetemekwa vidole, nikipanda sita shuka
Gari hili gari gani, najuta kulipandia
Kwa nyuma linapendeza, napenda wake mbinuko
Na mwendo likiongeza, lapepea kama puto
Ni kweli sijalikweza, gari hili moto moto
Gari hili gari gani, najuta kulipandia
Muda nilipo patia, gari hili nilipanda
Tena nikashikilia, katikati nikatanda
Kelele nilisikia, ila gari halikwenda
Gari hili gari gani, najuta kulipandia
Gari lilikakamaa, lilishindwa nifikisha
Pale nilipo tazama, mafuta linavujisha
Si kama nalisakama, mashineni kulitisha
Gari hili gari gani, najuta kulipandia
Nimebaki na majuto, gari limekinaisha
Sina tena ule moto, wa gari kulipaisha
Mwili bado umzito, bora nisinge liwasha
Gari hili gari gani, najuta kulipandia
Bora kupanda bajaji, popote wajipitia
Hazina mwingi mtaji, injini ni ndogo pia
Beteri ukisha chaji, wajitambia na njia
Gari hili gari gani, najuta kulipandia
KLORO na SPRINI, mwaonaje hii hoja
SHOSI naye WAKIJIJI, mchango wenu nangoja
MAGULU uko kundini, LIZZY pia tupamoja
Gari hili gari gani, najuta kulipandia
Na wote nisowataja, msiache kuchangia
Nipeni nyingi faraja, hoja sitapuuzia
Safari niloipanga, katu haikutimia
Gari hili gari gani, najuta kulipandia
Malenga wenu
Sindano ya ganzi (Local anaesthesia)
U wapi asprini
Mkongwe ninakuita, mtaalamu wa fani
Mbona hapa hujapita, wewe mwalimu wa ghani
Mwenzio leo najuta, nilikumbwa tafrani
Nangoja mchango wako, e ndugu asprini
Malenga wameshasema, mengi kunisaidia
kweli sijisikii vyema, mchango nahitajia
Hiki sasa ni kilema, injini zinafojiwa
Nangoja mchango wako, e ndugu asprini
sindano mwana wa ganzi
didy service station iko kwa ajili yakoHilo gari used au brand new?? Natania bana
Tatizo naona hukulifanyia service ya kutosha kabla ya safari kuanza hata hukucheki rejeta kama ina maji poa
Okeyyyy mdudu ndani ya kokwa la embe kaingiaje?
Salamu Yakuonea, Sikukukwepa garini,
Linifika ya dunia,Nikaenda safarini,
Mpendwa kumfukia, kwa udongo kaburini,
Mungu amlaze pema, Kaka yangu kwa amani.
Tukirudia hojani, Gari kuzungumzia,
Hilo gari ni la nani, naomba kuulizia,
Je ni lako la ndani, au umekodishia,
Shuka upande jingine, Safari yaendelea.
Sikutie ajalini, gari ulokodishia,
Au peleka sokoni, kama lako linunua,
Likuumize kwanini, Uteseke na dunia,
Nunua gari jingine, Safari iendelee.
Magari tele dukani, hilo acha ng'ang'ania,
Kakuasa klorokwini, nami ninamuungia,
Epukazo tafurani, na gari nalosumbua,
Chukua gari jingine, Safari yakungojea.
Salamu Yakuonea, Sikukukwepa garini,
Linifika ya dunia,Nikaenda safarini,
Mpendwa kumfukia, kwa udongo kaburini,
Mungu amlaze pema, Kaka yangu kwa amani.
Tukirudia hojani, Gari kuzungumzia,
Hilo gari ni la nani, naomba kuulizia,
Je ni lako la ndani, au umekodishia,
Shuka upande jingine, Safari yaendelea.
Sikutie ajalini, gari ulokodishia,
Au peleka sokoni, kama lako linunua,
Likuumize kwanini, Uteseke na dunia,
Nunua gari jingine, Safari iendelee.
Magari tele dukani, hilo acha ng'ang'ania,
Kakuasa klorokwini, nami ninamuungia,
Epukazo tafurani, na gari nalosumbua,
Chukua gari jingine, Safari yakungojea.
Hivi kweli viloja,walai na waambia.
Kati sijawai ona,wala masikio kusikia.
Dereva ana lalama,ati gari kumfia.
Na uliza tena,chuo gani umepitia?
Aibu wala huna,majigambo una yatia.
marekani umesoma,vyeti wame kugawia.
Vyombo vyete waendesha,Huku umesimamia.
Wasiwasi nime tia,Ngandya kumkumbatia.
Jitulize tuli kijana,darasani sasa nakutia.
Bora ngeshika supana,boliti kuzi fungua.
Uwoga uka ondoa,matatizo garini kuchungua.
Maji kwenye rejeta hiyo yake asilia.
istizahi ukazifanya,gari kulitukania.
Injini ili kupozwa,maji yana hitajika.
kau kau rejeta,gia hazita ingia.
kabla ya kuendesha,gereji ungepitia.
kupanda na kuendesha,haitoshi nakuambia.
Gari lako ukipata,mifumo utaijua.
upozaji wa rejeta,umeme taa kuwashia.
Oili kuongezea,vyuma visije chubua.
Fumbo fumbia mjinga,
Mwelevu huling'amua
Tungo weka tata,
Vifungo ukafungia
Wala sizo palapata,
Kwa ukweli zimetua.
Wala sio kwadhihaka.
Sanda nina zisifia.
Ugwiji mie sina,
Wakijiji ani jua,
wala sikupata hinda
Hoja zako kufumbua,
Mabano siku fungua,
Gari uchi kuwachia,
Tenzi zangu maridhia,
Lako gari kusifia,
Ila kigugumizi napata,
Udereva hujajua.