Najuta kulipandia........

Salamu nawatumia, magwiji mlochangia,
Swali nimelipitia, majibu yanavutia,
Nami nikaazimia, ujumbe kuwapatia,
Gari siyo gari “lile,”
Gari ni mkokoteni!

Muda nimeutumia, swali kulifikiria,
Ndipo iliponijia, hadi nikashangilia,
Jibu nikalipatia, la fumbo alilofumbia,
Gari siyo gari “lile,”
Gari ni mkokoteni!

Linafanana na kia, ndivyo ametuambia,
Gharama ni rahisia, si ghali tumesikia,
Miye namkubalia, la chee kalipandia,
Gari siyo gari “lile,”
Gari ni mkokoteni!

La rangi ya kahawia, gari akalisifia,
Magari tunajulia, hakuna ya kahawia,
Ni mbao kazisifia, mkokoteni karukia,
Gari siyo gari “lile,”
Gari ni mkokoteni!

Tena akatuambia, mbele limetanukia,
Lipi liko kama kia, mbele limejiachia?
Yale ya kusukumia, kwa mbele na nyuma pia,
Gari siyo gari “lile”!
Gari ni mkokoteni!

Nyuma akalisifia, mbinuko unavutia,
Wallahi sijasikia, gari linabinukia,
Jinsi ninavyojulia, mkokoteni kasifia!
Gari siyo gari “lile”,
Gari ni mkokoteni!

Tena akalipandia, kati akajiachia,
Wapi umeshasikia, kupanda ukatandia,
Mkokoteni ukipandia, kati utatanulia!
Gari siyo gari “lile”,
Gari ni mkokoteni!

Gari alilopandia, kelele alisikia,
Mbele halikuhamia, kashindwa kusukumia,
Limekosa girisia, mkweche kaudandia!
Gari siyo gari “lile”,
Ni gari mkokoteni!

Pole ninakugaia, kwa uliyojitakia,
Gari ulilopandia, si gari nakuambia,
Tairi zilizugia, wewe ukalidandia,
Gari siyo gari “lile”,
Ni gari mkokoteni!

Kelele ulizosikia, mgosi anavutia,
Wewe ukafikiria, benzi umelidandia,
Nne ukajikunjia, sigara unavutia,
Gari siyo gari “lile”,
Ni gari mkokoteni.

Safari ikikujia, kwanza anza ulizia,
Tafiti na tafutia, kabla hujalidandia,
Ujue kama ni kia, au lori la skania,
Gari siyo gari lile,
Ni gari mkokoteni!

Beti ninaziachia, fumbo nimefumbulia,
Natumai utaachia, gari la kufikiria,
Kisha utajipangia, la ukweli kupatia,
Gari ulilodandia,
Ni gari mkokoteni!!

Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)
I salute mzee
 
Wadai mkokoteni, jamvini watuambia
Nami nakupa yakini, KIA lilifanania
Naomba uniamini, mimi nililipandia
Ni gari niliopanda, nakana mkokoteni

Itakuwaje safari, ndani ya mkokoteni
Kwa hizo zake kikiri, safari hutotamani
Mimi si kama tumbiri, najua nini thamani
Ni gari niliopanda, nakana mkokoteni

Utaendaje arusha, wapanda mkokoteni
Safari itakuchusha, bila fika kileleni
Hapa nakuhabarisha, na wengine sikizeni
Ni gari niliopanda, nakana mkokoteni

Kwa vipi waishangaa, rangi ya kahawia
Mbona yametapakaa, mjini wayasifia
Si kama nakuhadaa, jaribu kufuatilia
Ni gari niliopanda, nakana mkokoteni

Iweje mkokoteni, una injini kwa mbele
Hili kwangu ni geni, wakijiji tueleze
Uache yenye utani, na hoja usiibeze
Ni gari niliopanda, nakana mkokoteni

Mengi yana mifumuko, ni sifa yenye misingi
Na kwa nyuma mibinuko, angalia 'mashangingi'
Mbona wafanya vituko, au ushakuwa dingi?
Ni gari niliopanda, nakana mkokoteni


Sindano mwana wa ganzi



Salamu nawatumia, magwiji mlochangia,
Swali nimelipitia, majibu yanavutia,
Nami nikaazimia, ujumbe kuwapatia,
Gari siyo gari “lile,”
Gari ni mkokoteni!

Muda nimeutumia, swali kulifikiria,
Ndipo iliponijia, hadi nikashangilia,
Jibu nikalipatia, la fumbo alilofumbia,
Gari siyo gari “lile,”
Gari ni mkokoteni!

Linafanana na kia, ndivyo ametuambia,
Gharama ni rahisia, si ghali tumesikia,
Miye namkubalia, la chee kalipandia,
Gari siyo gari “lile,”
Gari ni mkokoteni!

La rangi ya kahawia, gari akalisifia,
Magari tunajulia, hakuna ya kahawia,
Ni mbao kazisifia, mkokoteni karukia,
Gari siyo gari “lile,”
Gari ni mkokoteni!

Tena akatuambia, mbele limetanukia,
Lipi liko kama kia, mbele limejiachia?
Yale ya kusukumia, kwa mbele na nyuma pia,
Gari siyo gari “lile”!
Gari ni mkokoteni!

Nyuma akalisifia, mbinuko unavutia,
Wallahi sijasikia, gari linabinukia,
Jinsi ninavyojulia, mkokoteni kasifia!
Gari siyo gari “lile”,
Gari ni mkokoteni!

Tena akalipandia, kati akajiachia,
Wapi umeshasikia, kupanda ukatandia,
Mkokoteni ukipandia, kati utatanulia!
Gari siyo gari “lile”,
Gari ni mkokoteni!

Gari alilopandia, kelele alisikia,
Mbele halikuhamia, kashindwa kusukumia,
Limekosa girisia, mkweche kaudandia!
Gari siyo gari “lile”,
Ni gari mkokoteni!

Pole ninakugaia, kwa uliyojitakia,
Gari ulilopandia, si gari nakuambia,
Tairi zilizugia, wewe ukalidandia,
Gari siyo gari “lile”,
Ni gari mkokoteni!

Kelele ulizosikia, mgosi anavutia,
Wewe ukafikiria, benzi umelidandia,
Nne ukajikunjia, sigara unavutia,
Gari siyo gari “lile”,
Ni gari mkokoteni.

Safari ikikujia, kwanza anza ulizia,
Tafiti na tafutia, kabla hujalidandia,
Ujue kama ni kia, au lori la skania,
Gari siyo gari lile,
Ni gari mkokoteni!

Beti ninaziachia, fumbo nimefumbulia,
Natumai utaachia, gari la kufikiria,
Kisha utajipangia, la ukweli kupatia,
Gari ulilodandia,
Ni gari mkokoteni!!

Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)
 
Ati....!!!!,nini?? Mkokoteni..!!!!!????ha ha ha ha ha ha ha!

Nguli kaja jamvini, jipya katuambia
Eti ni mkokoteni, labda sikuujulia
Hili sikubaliani, ni gari nimemwambia
Ni mzee wa kijiji, mkokoteni kanena.............
 
JAMANI EEH,HILO SIO GARI.ETI LIMEBINUKA,DOH!HAKUNA GARI LENYE MA BEHIND MAKUBWA,HILO NI UPANDE WETU WA PILI TU.LOL:becky:
 
Angalia hizi gari nyingi za sasa ( new model -face lift) nyingi utaona kwa nyuma zimebinuka na utapenda kuziangalia hasa zinapoendeshwa.........hahaha, hapa tunazungumzia magari bana, twende sasa.......


Magari haya ya sasa, si kama ya enzi zile
Yameongezwa anasa, dereva ufurahie
Na tena yana hamasa, kwa ndani usisusie
Magari haya ya sasa, mengi yamebinuliwa

Yale yasio binuka, machoni yanachusha
Na huwezi kusisimka, kuendesha yanachosha
Hutoweza kuridhika, ijapo umeendesha
Magari haya ya sasa, mengi yamebinuliwa

Ukiyatizama kwa mbele, nako nyuma yavutia
Waweza fika kilele, safari kidhamiria
Hayana nyingi kelele, raha utajisikia
magari haya ya sasa, mengi yamebinuliwa


Na sindano mwana wa ganzi



JAMANI EEH,HILO SIO GARI.ETI LIMEBINUKA,DOH!HAKUNA GARI LENYE MA BEHIND MAKUBWA,HILO NI UPANDE WETU WA PILI TU.LOL:becky:
 
Ewe mkulima mwema, nashukuru ulosema
magari haya ya zama, ni sawa vile kilema
Jipya nitatazama, nataka lenye neema
Mwenyezi akijalia, jipya ntajitwalia


Na sindano mwana wa ganzi

Hongera kwa mashairi mazuri,pole mwanakwetu mbona kuna gari mpya zipo zinauzwa hayo ya zamani sisi tumeyaacha
 
Back
Top Bottom