Jifunze kuelewa kiongozi, kisheria kosa moja linaweza kuza makosa hata mia moja. Ngoja nikupe mfano: Jangiri amekutwa na meno ya tembo, hilo ni koja moja ambalo ndilo lililomfanya atiwe mikononi, sasa ona mtiririko wa makosa yanayofuata: 2. Amehujumu uchumi 3. Kuingia kwenye hifadhi bila kibali maalumu 4. Kumiliki silaha kinyume na sheria 5. Kuharibu mazingira na bio diversity. 6. Kukiuka misingi ya haki za wanyama za kuishi na haki za viumbe hai wengine 7. Kupoteza pato la taifa litokanalo na utalii 8, 9, 10, nk. Utaona kuwa kunamtiririko wa makosa chungu nzima yaliyotokana na kosa kuu la kukutwa na nyala za serikali.
Turudi kwenye Zitto saga: Kosa kuu la Zitto ni kushiriki kwenye mpango waliouita mkakati wa mabadiriko 2013 yeye pamoja na wenzake. Hapo utakutana na makosa yafuatayo yaliyotokana na kosa la kwanza 2. Kukiuka misingi ya uongozi yeye km naibu katibu mkuu 2. Kwenda kinyume na katiba 3. Kuhujumu chama 4. Kuwagombanisha viongozi wa juu, pia kugombanisha viongozi na wanachama 5. Mkakati wa kuangamiza chama badala ya kukijenga 6. Kupelekea mpasuko ndani ya chama 7,8,9,10 nk. (NB:Sijakwambia kuwa hayo ndiyo makosa ya Zitto, nilikuwa nakuweka sawa kuhusu andiko lako)