mtoa mada ni mmoja ya wasomi uliowaongelea hapoBila shaka ni ukweli usiopingika, wahitimu wengi wa vyuo afrika kwa ujumla magonjwa yafuatayo yanawatafuna;
1. Kukariri
2. Kusoma kwaajili ya kuajiriwa
3. Kusoma kwaajili ya kufaulu vyuoni
4. Ukimuuliza swali lolote la kada aliyosomea atakwambia hiyo atukufundishwa
Kuna mmoja kahitimu chuo cha NIT mechanical engineering, kuna mashine ndogo nlimuonyesha aitengeneze tupige pesa, alichonijibu nilisikitika sana eti anasema wamefundishwa kutengeneza mashine kubwa tuu.
Nkajiuliza kama mtu anashindwa kutengeneza mashine ambayo haizidi kilo mbili atawezaje kubuni au kutengeneza mashine inayozidi tani moja.
ELIMU YETU HAINA MSAADA
kama majibu yake ni ya kuchagua yani a b c d au e.
me nakushauri uchague b
Utaanzia wapi kuifumua wakati wakoloni weusi wako kazini?Ni kweli mkuu, wahitimu wengi wa vyuo vikuu katika nchi za Africa huishia kufa masikini kutokana na kutokuwa na mfumo rafiki wa elimu ambao unaweza kumwandaa na kumjenga kijana tokea ngazi za awali.
Mifumo yetu ya elimu imejijenga katika kuwajanza wanafunzi hard disk zao kwa mambo mengi yasiyokuwa na msingi wala maana yoyote kwenye maisha yao. Chukulia masomo kama History yanafundishwa ili iweje?
Pia, kusoma bila focus nalo ni tatizo kubwa. Kwetu sisi wa Africa ni fahari zaidi kusoma na kumaliza madarasa lakini wenzetu huwa wana focus kwenye fani fulani na kubobea na pale anapohitimu mtu anakuwa na ujuzi wa hali ya juu na kuweza kujiajiri katika fani husika au hata kuajiriwa na kuleta mchango chanya.
Elimu ya nchi zilizoendelea imejikita zaidi kumpa uwezo mhitimu akimaliza masomo yake aweze kujiendeleza mwenyewe na ndio maana utaona wasomi wengi huweza kuanzisha makampuni yao kutokana na ubunifu walioupata kutoka kwenye vyuo.
Hata wale ambao hawakufanikiwa kumaliza shahada zao nao huwa tayari wana ujuzi mwingi kutokana na mfumo wa elimu kuwa rafiki toka ngazi za chini.
Mfano akina Zuckerberg, Bill Gate hawakufanikiwa kumaliza elimu zao za juu lakini walikuwa na uwezo na ubunifu wa kufanya mambo makubwa na kuwa ma CEO wakubwa duniani.
Naweza kuandika kitabu hapa lakini kufupisha tu nashauri serikali zetu kufanya ammendments katika sera za elimu na mifumo ya elimu ili ziweze kuendana na mabadiliko yaliyomo kwenye karne hii ya 21.
Mitaala mingi tunayotumia tumenakili kutoka kwa wenzetu ambao tayari walishaizika zamani kutokana na kukosa feasibility katika dunia ya sasa. Ubaya ni kuwa sisi bado tumeikumbatia na ndio chanzo cha kuzidi kuachwa na wenzetu ambao wanazidi ku advance kila siku na kufanya mambo ambayo kiakili za kibinadamu ni kama ndoto.. Refer Elon Musk (Space X and Mars Colonizatio e.t.c
Bila kuifumua mifumo ya elimu na serikali kuwekeza ziaidi kwenye sekta hiyo hakika hakuna jipya tutakaloliona.
Tuache kuwapa watahiniwa majibu ili tujisifie ufaulu. Ni upumbavu.
Sasa mbona hujagawa booklets?
Dah noma sana ndomana hata asiesomea hiyo fani akitafuta cheti basi kamaliza hata kama ajajifunza kitu atajulia humo humo kazini inauma sana unaweza kuta alopewa hiyo kazi cheti cha kufoji sio cha ukweli.Hii ni matokeo ya kuamini kupima uwezo wa mtu kupitia alichokipresent kwenye karatasi, pasipo kutumia njia sahihi ya kupima uwezo halisi wa mtu alionao. Hili si tatizo la Elimu kwa Afrika pekee bali dunia nzima, isipokuwa wenzetu wametuzidi katika kutambua uwezo halisi alionao mtu. Katika recruitment sisi tunaangalia unajua nini badala ya unaweza kufanya nini!
Nitakupa mfano wa kijana mmoja. Huyu kijana alisoma mwaka mmoja tu katika fani fulani ya uhandisi, alikuwa discontinued kutokana na kufeli. Lakini katika huo mwaka alipoenda field alijipenyeza katika kampuni hiyo hadi akabaki hapo, na watu wakampenda kutokana na uwezo wake wa kufanya kazi. Kampuni hiyo wakaamua kufanya recruitment, watu wakampenyeza hadi kwenye interview kuona kama anaweza kufanya lolote na kufikiriwa na watoa uamuzi. Kijana alifaulu vizuri interview kuliko walio na vyeti hata vya abroad. Lakini cha ajabu watoa uamuzi wamemdisqualify kwa sababu hana certifying papers. We don't recognize the real human potential. We measure people on memory basis. Hivyo tunapoteza vipaji vya kweli.
Changamoto kubwa katika usomi wetu Africa tunashindwa kutafsiri kile tulichokisoma darasani katika Ulimwengu halisi.