Najiandaa kwenda Kufanya Mtihani mchana na nimeambiwa hili Swali lipo hivyo naomba mnipe majibu ili nifaulu

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,054
107,538
Swali lenyewe linasema...." Waafrika wengi ni Wahitimu tu wa Vyuo Vikuu ndiyo maana nchi zao zinahangaika Kimaendeleo na Wazungu wengi ni Wasomi wa kweli wa Vyuo Vikuu ndiyo maana kila siku wanazidi Kuendelea ", Jadili ( Alama 50 )

Nitawashukuruni wana JamiiForums.

Nawasilisha.
 
Bila shaka ni ukweli usiopingika, wahitimu wengi wa vyuo afrika kwa ujumla magonjwa yafuatayo yanawatafuna;
1. Kukariri
2. Kusoma kwaajili ya kuajiriwa
3. Kusoma kwaajili ya kufaulu vyuoni
4. Ukimuuliza swali lolote la kada aliyosomea atakwambia hiyo atukufundishwa

Kuna mmoja kahitimu chuo cha NIT mechanical engineering, kuna mashine ndogo nlimuonyesha aitengeneze tupige pesa, alichonijibu nilisikitika sana eti anasema wamefundishwa kutengeneza mashine kubwa tuu.

Nkajiuliza kama mtu anashindwa kutengeneza mashine ambayo haizidi kilo mbili atawezaje kubuni au kutengeneza mashine inayozidi tani moja.

ELIMU YETU HAINA MSAADA
 
Pamoja na kuhitimu ni wachache ambao huona fursa na kuzifanyia kazi,Hii inatokana na milolongo mirefu katika ufuatiliaji,usajili,umiliki wa fursa.Hata kama utakuwa na malengo ya kuwekeza katika fursa mbalimbali hususan viwanda vidogovidogo sana sana utakamatwa na kufungiwa pasipo kuambiwa nini ufanye kuendeleza utashi wako.Ndiyo maana nchi za wenzetu unaweza kuanzisha hata "shindano la kula pilipili na watu wakatoa kiingilio ukapata hela na maisha yakaendelea" sasa Africa uunda ndege au gari kwa local material usikilizie balaa lake.
 
Ndio maana ukaambiwa wengi ni wahitimu tu lakini sio wasomi,hapa umedhihirisha hilo unataka ulishwe wewe umeze tu ili uwe muhitimu usiwe msomi?
 
Jibu lake ndo hili Kama swali simple unashindwa kuchanganua unataka tukupe majibu umeze tu.. ndo mana nchi zetu hazina maendeleo

Ukiwa na ' akili ' ndogo na Pumbavu / Popoma siku zote utakuwa unapata shida na taabu sana na GENTAMYCINE hapa Jamvini ila ukiwa ' Genius ' basi kila ' bandiko ' langu utakuwa unalielewa haraka mno kwani ' uwasilishaji ' wangu ni wa Kifasihi na Kifikirishi zaidi na ningeshangaa kama huu ' Uzi ' wangu usingewapata wenye ' Fikra ' finyu na ' Kukurupuka ' nazo.
 
Bila shaka ni ukweli usiopingika, wahitimu wengi wa vyuo afrika kwa ujumla magonjwa yafuatayo yanawatafuna;
1. Kukariri
2. Kusoma kwaajili ya kuajiriwa
3. Kusoma kwaajili ya kufaulu vyuoni
4. Ukimuuliza swali lolote la kada aliyosomea atakwambia hiyo atukufundishwa

Kuna mmoja kahitimu chuo cha NIT mechanical engineering, kuna mashine ndogo nlimuonyesha aitengeneze tupige pesa, alichonijibu nilisikitika sana eti anasema wamefundishwa kutengeneza mashine kubwa tuu.

Nkajiuliza kama mtu anashindwa kutengeneza mashine ambayo haizidi kilo mbili atawezaje kubuni au kutengeneza mashine inayozidi tani moja.

ELIMU YETU HAINA MSAADA

' Reasoning ' kama hii ndiyo nilikuwa naitaka. Safi sana Mkuu na uko vizuri.

Cc: Bravo , badoo
 
Ukiwa na ' akili ' ndogo na Pumbavu / Popoma siku zote utakuwa unapata shida na taabu sana na GENTAMYCINE hapa Jamvini ila ukiwa ' Genius ' basi kila ' bandiko ' langu utakuwa unalielewa haraka mno kwani ' uwasilishaji ' wangu ni wa Kifasihi na Kifikirishi zaidi na ningeshangaa kama huu ' Uzi ' wangu usingewapata wenye ' Fikra ' finyu na ' Kukurupuka ' nazo.
Pole sana
 
Wapo wa
Bila shaka ni ukweli usiopingika, wahitimu wengi wa vyuo afrika kwa ujumla magonjwa yafuatayo yanawatafuna;
1. Kukariri
2. Kusoma kwaajili ya kuajiriwa
3. Kusoma kwaajili ya kufaulu vyuoni
4. Ukimuuliza swali lolote la kada aliyosomea atakwambia hiyo atukufundishwa

Kuna mmoja kahitimu chuo cha NIT mechanical engineering, kuna mashine ndogo nlimuonyesha aitengeneze tupige pesa, alichonijibu nilisikitika sana eti anasema wamefundishwa kutengeneza mashine kubwa tuu.

Nkajiuliza kama mtu anashindwa kutengeneza mashine ambayo haizidi kilo mbili atawezaje kubuni au kutengeneza mashine inayozidi tani moja.

ELIMU YETU HAINA MSAADA
Wapo wazungu waliosoma na kuona vyuo vina poteza muda na kunza kupiga pesa...

MF. Mark zukernburg
Bill gate
Enos musk

Na wengine utaongezea hawa kwa sasa wana mikwanja ya hatari... Swali la nyongeza he elimu ndio kila kitu??? Iwe una soma japani au Tanzania
 
Mkuu wewe nenda kakose tu hilo swali maana hamna namna kila kitu wazungu walikufundisha ufwate wanavyotaka mfano mzr hakuna vitabu vya chuo kikuu vilivyo andikwa kiswahili kasoro Bible tu
 
Ni kweli mkuu, wahitimu wengi wa vyuo vikuu katika nchi za Africa huishia kufa masikini kutokana na kutokuwa na mfumo rafiki wa elimu ambao unaweza kumwandaa na kumjenga kijana tokea ngazi za awali.

Mifumo yetu ya elimu imejijenga katika kuwajanza wanafunzi hard disk zao kwa mambo mengi yasiyokuwa na msingi wala maana yoyote kwenye maisha yao. Chukulia masomo kama History yanafundishwa ili iweje?

Pia, kusoma bila focus nalo ni tatizo kubwa. Kwetu sisi wa Africa ni fahari zaidi kusoma na kumaliza madarasa lakini wenzetu huwa wana focus kwenye fani fulani na kubobea na pale anapohitimu mtu anakuwa na ujuzi wa hali ya juu na kuweza kujiajiri katika fani husika au hata kuajiriwa na kuleta mchango chanya.

Elimu ya nchi zilizoendelea imejikita zaidi kumpa uwezo mhitimu akimaliza masomo yake aweze kujiendeleza mwenyewe na ndio maana utaona wasomi wengi huweza kuanzisha makampuni yao kutokana na ubunifu walioupata kutoka kwenye vyuo.

Hata wale ambao hawakufanikiwa kumaliza shahada zao nao huwa tayari wana ujuzi mwingi kutokana na mfumo wa elimu kuwa rafiki toka ngazi za chini.

Mfano akina Zuckerberg, Bill Gate hawakufanikiwa kumaliza elimu zao za juu lakini walikuwa na uwezo na ubunifu wa kufanya mambo makubwa na kuwa ma CEO wakubwa duniani.

Naweza kuandika kitabu hapa lakini kufupisha tu nashauri serikali zetu kufanya ammendments katika sera za elimu na mifumo ya elimu ili ziweze kuendana na mabadiliko yaliyomo kwenye karne hii ya 21.

Mitaala mingi tunayotumia tumenakili kutoka kwa wenzetu ambao tayari walishaizika zamani kutokana na kukosa feasibility katika dunia ya sasa. Ubaya ni kuwa sisi bado tumeikumbatia na ndio chanzo cha kuzidi kuachwa na wenzetu ambao wanazidi ku advance kila siku na kufanya mambo ambayo kiakili za kibinadamu ni kama ndoto.. Refer Elon Musk (Space X and Mars Colonizatio e.t.c

Bila kuifumua mifumo ya elimu na serikali kuwekeza ziaidi kwenye sekta hiyo hakika hakuna jipya tutakaloliona.

Tuache kuwapa watahiniwa majibu ili tujisifie ufaulu. Ni upumbavu.
 
Acha ' Bange / Bangi ' Mkuu hebu nipe ' madini / maarifa ' ili niweze Kufaulu huu Mtihani wangu muhimu mno wa leo mchana.
Kwakushindwa kujibu hili swali basi ni kweli Waafrika ni wahitimu wa vyuo vikuu tu.

Hivyo kitendo cha kushindwa kujibu mpaka kutuuliza Swali lako limethibitisha.
 
Kama swali lako liilivyo; nitalijadili kama i fuatavyo:
Kwanza nianze na waafrika; sio kweli kwamba waaffika wengi ni wahitimu wa vyuo vikuu; wengi hawajaenda hata level ya kidato cha nne. Hivyo wale wachache waliohitimu vyuo vikuu wanajiona kama wazungu weusi; hawako tayari kuleta maendeleo kwenye nchi zao ndiyo maana Africa haiendelei.
Wazungu ni wasomo wa vyuo vikuu; walishajua fika kwao hakuna la kufanya ndiyo maana wanafanya ujasusi wa kiuchumi, kisiasa na kijamii ili kuendelea kutetea kazi zao.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom