Najiandaa kugombea urais 2030

Onambali..sababu umetangaza nia ni vyema ukajitambulisha kabisa kwa majina halisi na details zingine watu wakufahamu..ili tuweze kukupima kwa mwenendo wako na kukushauri accordingly!
 
Kwanza nikupongeza kwa ndoto yako ila vile vile nikukumbushe unahitaji kufanya kazi ili kuifikia ndoto yako.Ni nzuri, ni halili na ni haki yako!

Ukimuondoa baba wa taifa, viongozi wetu hawakujiandaa kuongoza taifa letu ndo maana tumeshuhudia wa kiingia madarakani sio kwa sababuya sera zao bali kwa nguvu ya dola. Matokeo yake imekua kufanya programu za muda mfupi za kutafuta umaarufu japokuwa hazina maslahi kwa taifa(hapa nafikiria sera ya ruksa ambayo iliua viwanda vyetu, sera ya ubinafsishaji ambayo haikuhakikisha viwanda vyetu vinaendelea kuzalisha, machinga complex, mabilion ya rais etc).

Sasa ushauri wangu ni kwamba chagua taaluma ambayo itakupa uelewa mpana wa kuweza kuwa rais wa kizazi cha 2030, uisome na uwe na uwelewa na waledi wa kupigiwa mfano.vile vile kumbukua hii ni nadhiri yako na mungu wako wala usije public na kutangaza (with expectional ya JF) kwa sababu utapata marafiki mafisadi. Ningekushauri useme digrii ya sheria na usome constitutional then ufanye degree ya public administration/public management wakati unatupia macho vp mashirika/corporates yanaendeshwa.

Kama haujaanza kusoma vitabu vya Obama aanza kusoma sasa: The dreams of my father and the audicity of hope vitakusaidiana sana.

Mwisho na kupa tahadhari; I am bringing my daughter to become the first female president in Tanzania.so stay tuned!
 
Content iliyopo kweny ambition zako iko safi ila mchango wako katika taifa kabla ya 2030 usadifu malengo yako, ili kujenga imani kwa watakaokupigia kura wakati huo. Onesha kama unaweza kuwa presida sasa na c 2030!
 
WanaJF,
Nawasalimu.
Kama mtakumbuka mimi Onambali, nimetanagaza nia yangu kupitia JF ya kugombea urais wa nchi yetu mwaka 2030. Nashukuru kwa maoni yenu. Nina sababu nyingi kwa nini nataka kuomba ridhaa ya wananchi ili niwe mtumishi (rais) wao na nilishaeleza mambo machache katika thread yangu iliyopita.
Ninaumia sana kuona nchi yetu inaharibiwa mbele ya macho yangu. Tunahitaji viongozi watakaoweza kutafsiri wakati tulionao na ule ujao yaani kuamua na kupanga muelekeo wa taifa. Ni aibu na hatari kubwa katika maendeleo yetu kuwa na kiongozi wa uma ambaye ni mbinafsi (anayefikiri yeye na famila yake tu ndo wanastahili kufaidi mema ya Tanzania aliyotukirimia Mungu), mchoyo (anayenyima haki ya watu kumkataa- yaani mpenda madaraka), muongo (anayeongea bila facts kwa lengo la kuwadanganya wasiobahatika kwenda shule), mtapanya mali (anayetumia utajiri wa uma kwa mambo yasiyokuwa ya lazima), mlafi (anayekula hadi chenga ambazo waliokosa fursa wangezitumia kujiendeleza), fisadi (anayekumbatia ufisadi kwa sababu ya ufisadi), mropokaji (anayeongea bila kufahamu kwamba kuna watu wenye uwezo mkubwa wa kufikiri kuliko yeye), mtaka starehe ( kwa sababu hana uchungu na wanaoteseka kwa maisha), mzinzi (kwa sababu hajajiwekea taratibu za kuutawala mwili wake, hivyo pia kutumia nafasi hiyo kulipa fadhila katika utoaji wa huduma za kiuongozi). Ndugu wanaJF, viongozi wa aina hiyo niliyoeleza hapa hawawezi kutufikisha popote. Wataendelea kuwafanya waafrika watumwa wa umaskini. Maskini wa kufikiri sio mbunifu, hana maona ya mbali maana kwake uongozi ni kama ‘uungu' wa kuwafanya wengine kuwaabudu na kutokuwa na haki ya kufurahia urithi na utajiri wa nchi yao.
WanaJF,
Watanzania wengi wanachukizwa na mambo mabaya yanayoendelea katika nchi yetu na huishia kusema...'tunahitaji viongozi wasafi, watakaofanya jambo hili au lile'..., lakini wengi hawapo tayari kujitoa kuanza mashambulizi ili kufanikisha nia yao kwa nchi yao. Hufikiri kazi ya kukomboa nchi kutoka katika mikono ya umaskini na ujinga ni ya watu fulani na haiwahusu wao. Mimi Onambali, nimeamua kabisa kutoka moyoni kuwa kiongozi wa Tz. Naamini ninauwezo wa kuitoa Tanzania katika maji taka na kuifanya (kwa nguvu yetu wenyewe na rasilimali alizotujalia Mungu) kuwa nchi itakayotoa matunda mema ya upendo, amani, furaha, na umoja wa kweli wa kizalendo utakaotawaliwa na haki, usawa katika fursa zote na matumizi mazuri ya sayansi na tekinolojia. Nafahamu ukweli unauma na waweza kunigharimu kifo lakini heri nife kama shujaa kwa manufaa ya uma kuliko kuishi kama dhalimu.

Naipenda nchi yangu na watu wangu. Ee Mwenyezi Mungu, naomba uibariki nchi yetu TZ.
 
Unataka urais kwa chama gani? Jiweke bayana kwa kuanisha policy na itikadi zako uweze Chukua Chako Mpema. Tuweke bayana ndugu.
 
Unataka urais kwa chama gani? Jiweke bayana kwa kuanisha policy na itikadi zako uweze Chukua Chako Mpema. Tuweke bayana ndugu.

Sijawa mwanachama wa chama chochote bado. Ujitahidi kuepuka fikira hiyo hapo kwenye red. Siongelei changu, naongelea nchi yangu na watu wangu
 
Muogope kama ukoma mtu anautaka uongozi, maana akiupata itakuwa balaa kuuacha. Na wengi wanaishia kuwa madekteta na mafisadi. Shauri yako.
Kiongozi safi na bora ni yule ambaye watu wanamuomba kuwaongoza, si anawaomba watu awaongoze.

Ushauri wangu ndg: Usiombe uongozi kwa maana ukipewa hutasaidiwa. Ila watu wakikuomba kuwaongoza watakuwa nyuma yako na watakusaidia.

Kila la heri
 
Onambali:

Unless unajoke, ila kama uko serious disclose jina lako halisi na details zingine zinazokuhusu, then we can coment on your ambition. Otherwise it is meaningless to comment to someone you even dont know his/her name. By the way are you a man or a woman??
 
Onambali:

Unless unajoke, ila kama uko serious disclose jina lako halisi na details zingine zinazokuhusu, then we can coment on your ambition. Otherwise it is meaningless to comment to someone you even dont know his/her name. By the way are you a man or a woman??

Im a man.

Its too early to disclose all my deatils. Please comment on the content of my ambition. I can tell you that I am very sereous
 
Back
Top Bottom