Onambali
Member
- Mar 11, 2011
- 67
- 10
WanaJf,
Kwanza nawasalimu.
Naomba maoni yenu katika kusudi langu la kutaka kuwa rais wa Tz mwaka 2030 kama Mungu akinipa uhai.
Ninachotarajia kufanya nitakapopata uraisi ni pamoja na:
1. Kuvunja mpango wa muda mrefu wa wazungu (walioanzisha pale Berlin mwaka 1884) ambao hadi sasa unatawala kifkra za mwafrika na kufanya vipaji na mazuri ya muafrika kutoendelezwa. Natarajia kuongoza Taifa letu lijenge watu huru wanaojiamini na kufurahia utaifa wao.
2. Kuweka mpango wa muda wa miaka 500 wa Tanzania katika maeneo mbalimbali ya maendeleo mfano miundombinu, kilimo na ufugaji, utunzaji wa maji ambayo yanaendelea kutoweka kutoka katika vyanzo vyetu vya maji, elimu itakayoongozwa na utashi na vitendo, afya, makazi na mipango miji itakayo kidhi haja ya miaka hiyo 500 mbeleni (sio kujenga na kubomoa bomoa kama ilivyo sasa), kutunza na kuhifadhi mbuga zetu za wanyama ili kutufaidisha sisi na vizazi vijavyo, kuanzisha mtindo wa kujengea wananchi makazi bora, kutunza na kuendeleza fukwe zetu za bahari na maziwa ili kuimarisha utalii, na mengineyo kama nitakavyoshauriwa na wanachi.
3. Kuondoa utegemezi wa misaada kutoka nje ya chi kwa maana ya kutumia kwa uangalifu pato letu la Taifa kwa kuondoa matumizi ya yasiyo ya lazima mfano magari ya kifahari serekalini, kuziba mianya yote ya rushwa kwa vitendo ikiwa ni pamoja na kutaifisha mali za walio-wanaona watakaotuibia na kuwasweka gerezani.
4. Kutoa heshima inayostahili kwa wataalamu wetu ikiwa ni pamoja na kuwalipa mishara mizuri itakayowafaya wasiondoke nchini, pia kuwawezesha kutumia taaluma zao katika kujenga nchi badala ya kuleta wataalamu kutoka nje.
5. Kuwalinda, kuwapenda, kuwaheshimu na kuwakuza katika maadili mema watoto wetu ili waipende nchi yao na kufurahi kuzaliwa Tanzania
6. Kuwa mtumishi wa wanachi na sio kuwa mtawala wa wanachi
7. Kuwa msikivu na mtendaji wa matokeo ya tafiti za wataalamu wetu katika kuijenga nchi yetu
Hitimisho
Taaluma mbalimbali zinazotolewa Tz hazijaweza kumfanya mtanzania (kwa wastani) akomboke kutoka kwenye umaskini wa akili na ushirikina. Nafahamu miaka 19 ijayo ni mingi na mambo mengi yatakuwa yamebadilika ila ni vizuri nijinoe kuanzia sasa. Moyoni mwangu nina nia njema kabisa ya kuongoza taifa letu katika kuweka na kuanza kuainisha jinsi ya kufikia malengo ya miaka 500 ijayo.
NB. Mimi ni mwananchi wa kawaida na sijawa mwanachama wa chama chochote cha siasa.
Ee Mwenyezi Mungu naomba uibariki nchi yetu Tanzania.