Najiandaa kuchukua jimbo la Kongwa; Ndugai hakuna anachowafanyia wananchi

Kila la heri. Kuna thread ilikuwa na guidelines za mtu anayetaka kuwa mbunge afanyeje? By the way unapitia chama gani?

Siri za kushinda ubunge Tanzania

1. Kuwa karibu na wanachi hadi wakuzoee na kukuamini.
2. Ujichanganye na wananchi hadi wakuone ni mwenzao.
3. Utumie kwa uangalifu ushawishi wako na elimu yako hadi ilete mwanga mawazoni mwa wanachi na katika matarajio yao mbalimbali ya maendeleo
4. Jitofautishe na wowote wanaoaminika kuwa wana potentials za kugombea ili wewe uonekane unang'ara zaidi
5. Weka ratiba yako wazi na shughuli zako zote uzifanyazo ziwe wazi
6. Tenga muda wa kukutana na kubadilishana mawazo na makundi yote katika jamii kama wazee, vijana, akina mama nk
7. Onyesha upeo wako halisi juu ya mapinduzi ya kilimo na shughuli nyingine za kiuchumi kwa ujumla; itakupa uzito zaidi kama upeo huo ni sahihi kwa mazingira tuliyonayo
8. Zifahamu vizuri sera za wapinzani wako na uzifafanue vizuri bila husuda kwa wapiga kura wako kabla hujaonyesha wapi zilipo na mapungufu.
9. Jivunie bila haya chama chako na historia yake ya kuongoza mageuzi nchini mwetu. Hapa unapaswa kujivunia hata kama chama chako si maarufu
10. Jenga ushirikiano na wanasiasa wengine wenye ushawishi na wananchi wajue hilo hata kama wako nje ya jimbo lako

Kwa leo niishie hapa, siku nyingine nitawaletea siri zaidi za kuibuka na ushindi katika chaguzi za kidemokrasia
 
Job Ndugai anajiandaa kujiunga na baraza la Mawaziri........sasa unafanya kosa kumshtua.............kaa kimya aje aipate mwishoni mwishoni ambako hatakuwa na kuwadanganyia wananchi wa Kongwa..................na uelewe sasa anazo CDF...........subiri uone atazitumiaje?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom