Naitaji watu wenye uelewa mpana na busara wanishauri juu ya huyu mchumba wangu

Anna pita

JF-Expert Member
Jul 10, 2012
227
425
Juz nilileta Uzi wangu wa nimelikoroga ...nimeamua nifanye maamuzi magum kuna vitu kadhaa najiuliza sana
Naomba nitoe historian yangu fupi ili kidogo mjue tunaanzia wapi kulimaliza hili
Naomben watu kidogo wenye uelewa mpana na hapa naeleza ukweli wa maisha yangu acha hizo story/ nyuzi za nyuma zenye ujana ujana mwingi
Nimezaliwa 1987...
Elim yangu chuo
Nimejiajir kazi yangu inawejiweza kwa kiac kunipa mkate wa kila Sikh
Nov 2013 nilipata mchumba tulikutana kanisan akawa amenipenda na kuja kwa kasi ya ajabu maana tulionana Nov 26 lkn DEC 15 alinipeleka kwao akanivisha Pete mbele ya kanisa na January akaja nyumban kwetu kujitambulisha baaada ya WK wazazi wake wakaja kupatana mahar na kutoa siku hiyohiyo
wote tulishangaaa kasi ya jamaa lkn madai yake ni kanipenda ataki kunipoteza
Mimi nilikua naishi arusha nyumban mwanza basi baada ya mahar kabla ya kurudi kwangu nikawa nimeenda kwake ili kupajua nikawa nimepata ujauzito
Kumbe jamaa presha hizo alikua amezinguana na x wake ni mwl hapo hapo alipokua anafanyia kazi sasa akafanya kumkomoa kumbe x nae wameachana alikua tayar ana mimba so tulipishana miez 2 Mimi na xwake....
kufunga ndoa ikashindikana wazazi wake walikua watu wa dini ikabidi wasubirie nijifungue
Huku jamaa alipogundua X wake nimjamzito na walikua kijiji kimoja mapenz yakarudi upya kule
Du niliteseka sana maana alinifanyia visa vya kila rangi... Mimba ilinitesa ikabidi nije nyumban nikae nilipata mawazo hum nilifungua thread 1000 za ID tofauti ili kuomba ushauri...namshukuru mama angu alikua bega kwa bega kunifariji maana nilifikia hatua mbaya..sasa kukwepa aibu ya watu maana kwenye mahari walikula na kusherekea ikabidi tuwadanganye kua jamaa kapata matatizo kafungwa
Mpaka baba angu uwa sikai nae nimkali sana bamuogopa kama chui nae tukamdanganya hivyo mpaka leo anajua yule mchumba kafungwa
Baada ya yote nikarudi chuo nikawa na maisha yangu ya kujitegemea

Jan 2017 niakutana na huyu wa sasa tumeanzia urafiki mpana jun tukawa wapenz DEC akanipeleka kijijin kwao kunitambulisha kwao wakajua tumeshaoana maana hata kulala ilikua chumba kimoja
Feb akaja kujitambulisha kwetu baba angu akaitwa kwanza alikua amekataa kupokea posa akamwambia mama private je kamchunguza kwanza??? maana tunapisha miaka 2 tu na jamaa alafu mi namtoto jamaa hana
baba akasema je mmewe akitoka gerezan itakuaje??? Maana alimtolea mahari OK tukayabumba mzee kishingo upande akakubali posa akatushauri tuishi kwa Aman na upendo sababu wote watu wazima
Kasheshe imetokea ya kuwasiliana na huyo Dada
Jana huyo Dada kanitukana sana ananiambia Mimi kuolewa na jamaa nisali sana au niroge sana
Usiku nimeongea na jamaa nimemwambia sitaki mawasiliano na huyo Dada jamaa kanijibu hayo maisha nayimpangia nimagum mno hawez kosana na rafiki yake wametoka mbali
Watu wenye hekima naomben mnishauri nifanye nn? Baba namwambia nn? majiran kwa mwaka mwingine tena hii aibu naimalizaje??? Nimechanganyikiwa nataman nizime cm nipoteee kabisa Ila namuwaza mtoto wangu ataishi VP nakosa maamuz
 
Achana na hayo mambo yatakupotezea Muda, Muda wenyewe wa kuwapo duniani ni mdogo

Tatizo unapenda sana ndoa,

Hilo linakugharimu, maana kila atae kuja kukwwmbia anakupenda anataka kukuoa na we unavurugwa kabisa

Acha ujinga, Lea mtoto wako, tafuta pesa, furahia dunia,
 
pole sana, ANNA. hii ni ngumu kumesa, mshukuru Mungu una mtoto wako, focus on your life, muandalie mazingira mazuri ya sasa na ya baadae, kuolewa kwani lazima ? wanawake hapa ndipo napopata ukakasi, ishi maisha yako kwa amani, pengine huyo sio chaguo lako.
 
Nakushauri utulie kwanza,
Urelax achana na kuumizwa na mapenzi kila siku.

Mpe nafasi huyo jamaa,jipe nafasi na wewe pia,
Muda huwa ni rafiki mzuri wa kukupa maamuzi.
Na wewe uwe unatoa nafasi,sio kuwaambia wenzako tuu ndo watoe nafasi....hahhaha
 
Anna pita, wanaume wanakusoma akili zako na wanagundua unapenda ndoa (japo hakuna asiyependa ndoa bila sababu) sasa wanatumia ndoa kama fimbo...

Kingine ukiwa na mpenzi unaacha awe remote wewe tv, matokeo yake unaburuzwa tu, huwezi kumwambia mtu subiri kidogo tutaoana?

Pili hujipi muda wa kumchunguza MTU, akikurupuka huko nawe unakurupuka nae matokeo yake utaomba ushauri kila siku.

Fanya kazi zako, Lea mwanao, muda sahihi ukifika utapata mtu sahihi.....

Usione aibu watu watakuchukuliaje hakuna asiyekosea
 
Nakushauri utulie kwanza,
Urelax achana na kuumizwa na mapenzi kila siku.

Mpe nafasi huyo jamaa,jipe nafasi na wewe pia,
Muda huwa ni rafiki mzuri wa kukupa maamuzi.
Kupeana nafasi means kupumzika kwanza au inakuaje?
 
Anna pita, wanaume wanakusoma akili zako na wanagundua unapenda ndoa (japo hakuna asiyependa ndoa bila sababu) sasa wanatumia ndoa kama fimbo...

Kingine ukiwa na mpenzi unaacha awe remote wewe tv, matokeo yake unaburuzwa tu, huwezi kumwambia mtu subiri kidogo tutaoana?

Pili hujipi muda wa kumchunguza MTU, akikurupuka huko nawe unakurupuka nae matokeo yake utaomba ushauri kila siku.

Fanya kazi zako, Lea mwanao, muda sahihi ukifika utapata mtu sahihi.....

Usione aibu watu watakuchukuliaje hakuna asiyekosea
Shida ni mzee tunamwambiaje kwa hili??
 
Kupeana nafasi means kupumzika kwanza au inakuaje?
Yes,
Kila mtu ajitafakari kwa namna yake.

Usilazimishe mapenzi,huyo mwanaume ni mtu mzima na anajua nini anataka, utalazimisha leo,kesho yatajirudia yaleyale..
Nakushauri ukae kando kwa muda usome reaction ya mpenzi wako kwanza.
 
Back
Top Bottom