Naitaji ajira

Naitaji ❌
Nahitaji βœ…

Mshara ❌
Mshahara βœ…

Ata ❌
Hata βœ…

dsm ❌
DSM βœ…

muhimu Cha msingi ❌
muhimu cha msingi
βœ…

Naitaji ajira ELIMU ❌
Nahitaji ajira elimu βœ…
 
Muhimu = Cha Msingi
 
Habari zenu wana jamii Naitaji ajira ELIMU kidato Cha 6 sema kidato sio muhimu Cha msingi mshara nipo dsm....nimepga JKT ata wenye connection za majeshi njooni mnipe . Asante ❌

Habari? Nina uhitaji wa kazi, elimu yangu ni kidato cha sita, niko Dar es Salaam. Niko tayari kufanya kazi kwa malipo tutakayokubaliana. Pia nimepitia mafunzo ya JKT, hivyo ninaweza kuhudumu katika vyombo vya ulinzi. Asanteni. βœ…
 
Kuna utoto pia mkuu.
 
Huyu kijana namtilia shaka sana uwezo wake katika kufanya kazi
Me namuelewa kama amepiga comb za sayansi au hesabu nyingi Kuna Hali flani unasahau kuandika maneno mengi ya kiswahili ndiyo analopitia

Ingependeza mumsaidie kama Kuna uwezekano kwenye hitaji lake kuliko hivi mnavyomkosoa sana hata mtu anayetaka kumpa ajira anaweza kughairi kwa kusoma comment zenu
 
Mbona kaweka sample hapo juu arekebishe tu, shida siyo kuandika maneno. Jinsi alivyoandika hilo ombi ndiyo tatizo lilipoanzia
 
Mbona kaweka sample hapo juu arekebishe tu, shida siyo kuandika maneno. Jinsi alivyoandika hilo ombi ndiyo tatizo lilipoanzia
Sawa mkuu ila kusema hafai kuajiliwa kisa alichokiandika sio jambo zuri kuliongelea kama kumzibia rizki mwanadamu mwenzio
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…