Naitafuta FURAHA niipate wapi mie Jamani.

Naitafuta FURAHA niipate wapi mie Jamani.

Habari zenu wanajamii wenzangu. Mimi ni mwanamke umri miaka 32. Mwenzenu ninasumbuliwa na tatizo la kutokuwa na FURAHA. Tatizo hili limeanza miaka mingi sana nadhani tangu nikiwa mdogo sikumbuki mara ya mwisho nimefurahi lini.Kilichonifanya niweke hapa na kuomba ushauri ni baada ya kugundua week iliyopita kuwa nina miaka mingi pia SIJACHEKA maana kuna mtu alinisimulia story tena ya kijinga jinga tu ila NILICHEKA SANA hadi nikasikia mapafu/moyoni kama kuna mzigo nimeupunguza hapo ndipo nikastuka kumbe nina siku nyingi sana sijacheka. Ina maana siku zote nilikuwa natoa Plastic Smile tu na si kuwa nilikuwa NAFURAHI toka MOYONI.
Ninaomba umnipe Ushauri mwenzenu nifanye nini ili niwe na furaha (Happy) pia nicheke kicheko cha Ukweli sio Plastic Smile.
Maisha yangu kwa kifupi yako hivi:
1) Mie sio mtu wa kutoka (Outing),Nililelewa na Mama wa Kambo na sikupata muda wa kucheza na wenzangu nilipokuwa mdogo except muda ule nilipokuwa shuleni tu,muda wote nilikuwa nasaidia kazi za nyumbani..so sikuwa na marafiki zaidi ya niliosoma nao darasa moja. Tangu nikiwa mdogo nimekuwa mwenyewe mwenyewe tu,siwezi kusocialize kabisa,starehe yangu ni kulala. Inaweza kuwa ni sababu pia lakini mbona ninaishi kwangu tangu 2006 lakini sina FURAHA/AMANI YA MOYO.
2) Nina ugonjwa unaonisumbua miaka mingi sana kama 20 yrs sasa niko kwenye tiba maendeleo ni mazuri tu .Ila nimehangaika sana hadi kufikia hapa.Je hili pia laweza kuwa ni chanzo cha kukosa Furaha na kama ni ndio chanzo mbona nimeana kupata nafuu ya ugonjwa lakini bado sina FURAHA/AMANI YA MOYO.
3) Sijaolewa
Nishaurini mwenzenu nifanye nini ili niweze kuwa na FURAHA au AMANI YA MOYO.
Nenda Somalia kumependeza sasa
 
Jifunze kusamehe, ukute kutokana na mzingira uliyokulia kuja mengi uliyabeba moyoni yaliyo kua yanakuumiza, yaache yaende.......afu jikubali ulivyo.....na mpe Mungu Maisha yako mwombe akuonesha furaha yako ilipo......


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana, tatizo lako linaanzia pale ambapo hausocialize na jamii. Ku-socialize na jamii kunaweza kukutoa katika msongo mkubwa wa mawazo hivyo jitahidi sana kuwa karibu na jamii mfano. Mzuri tu hapa jf ulipo unakua upo socialize hivyo kwa namna fulani unaipata kampani ya kutokaa peke yako.

Kumbuka kukaa peke yako pia ni ugonjwa na pia ndio chanzo pekee cha tatizo lako. Pia usisahau kuwa mwepesi wa kusamehe hii itaujenga moyo wako vyema na kukupa tumaini na kuijenga furaha ndani yako. Lakini ukiwa ni mtu wa hasira/ visasi unauponda moyo sana na kuipoteza furaha yako.

Kila lakheri



Sent from my SM-J530F using Tapatalk
 
Achana huyo befriend. Anza kugegedwa kila siku na watu tofauti. Utapata furaha ambayo hujawahi ona.
 
Back
Top Bottom