Naitafakari sana kauli nzito ya Celina Kombani "hujafa hujaumbika"

AMA wewe unazaliwa wapi? waziri asiye na wizara maalumu "minister without portfolio" mbona hiki ni kitu cha zamani sana tangu enzi mwalimu enzi hizo Hayati R.M. Kawawa aliwahi kuwa waziri asiye na wizara maalum, wakati wa mkapa Dr. Hasy Kitine pia aliwahi kuwa waziri asiye na wizara maalum. labda kama unasema hiki ni kitu cha kipekee kwa Tanzania, lakini sio eti hujawahi kuona. wewe umezaliwa lini. naona ama umri unakusumbua au wewe ni bongolala
 

Uzi wako haueleweki kwa mtiririko mbovu! Unadhani kila unachokickia ww kila mtu anakickia? Tuambie kwanza Celine Kombani ilikuwaje akasema hujafa hujaumbika? Alisema wapi na baada ya nini? Unatiririka tu bila kunfafanulia msomaji heading yako inamahusiano gani na kilichomo?
 
Tafadhali usipotoshe historia; Salim Ahmed Salim hajawahi kuwa naibu waziri mkuu bali waziri mkuu!!!

Alikuwa Naibu Waziri Mkuu chini ya Waziri Mkuu Joseph Warioba.
Na hapo hapo akawa Waziri wa Ulinzi (na Jeshi la Kujenga Taifa)...
 

Watu wanakurupuka tu bila kufanya rejea hata moja! Hata historia hawana! Generally uwaziri nao hauna maana hawana tofauti na wakuu wa mikoa!
 
Rashid Kawawa pia amewahi kuwa waziri asiye na wizara maalum enzi za Mwinyi.
 

At least hao hawakuwa wagonjwa ................ HUJAFA HUJAUMBIKA! The bottom line is two wrongs do not make right! Serikali za awamu hizo hazikushindwa kutoa OC kwenye Idara na Taasisi zake. Lakini awamu hii haiwezi kutoa OC kwenye Idara na Taasisi zake, halafu eti katika mazuri yote yaliyofanywa na awamu zilizopita, awamu hii IMEONA ZURI MOJA TU LA KUTEUA MAWAZIRI WASIO NA WIZARA MAALUMU! But to add salt to the wound, yenyewe imekwenda mbali zaidi, kwa kuteuwa WAGONJWA kuwa mawaziri wasio kuwa na wizara maalumu. haya ndiyo mambo yanayotetewa na SPIN DR(?) wa awamu hii!!
 


Kama ugonjwa ndio unadhani ndio disqualification ya mtu kuwa waziri basi wabunge wengi ni wagonjwa ambao hawastahili kuteuliwa!!! Angalia tu jinsi bajeti yao ya wabunge wanaoongozana kwenda India; na hiyo ni siri yao wasioyoitaka ijadiliwe hadharani!!! Hakuna hata memba mmoja wa cabinet ambaye sio mgonjwa!!!! Huyo Celina Kombani mwenyewe ana maradhi yasiyotibika.
 
The look of her lips confirm your assertion.
 

Aisee, hiyo sijawahi kuisikia, bila shaka alitamka wakati wa mazishi kujipa promo kwa ndugu na jamaa ya marehemu wamwone ana mapenzi makuu na marehemu huyo mnafiki mkubwa. Amchague mtanzania yupi? Mbona hata sisi watanzania kama Mungu angekuwa anachukua kura tungewalisti na Mungu angeshawaondoa kitambo! Akiwepo yeye spika, si basi tu Mungu hajatoa hiyo chance, tena Mungu alivyo wa ajabu kiumbe ambaye hatakiwi ndiye anayeachwa muda mrefu, bila shaka ili atubu, huku wenyewe hawawezi hata kufikiria kutubu
 
Mbona kunachama kinachoitwa ukawa na hakina usajilli lakini husemi
 
Tanzania kwa vipindi mbalimbali imekuwa na mawaziri wasio na wizara maalum. Miongoni mwao ni marehemu Kawawa.

Pia nchi nyingine nyingi zina mawaziri wasio na wizara maalum. Miongoni mwa hizo nchi ni Uingereza ambayo kwa vipindi mbalimbali imekuwa na mawaziri kama hao. Serikali ya sasa ina mzee Ken Clarke.

Lengo hasa la hii nafasi ni kuwapa wale watu ambao uzoefu wao unaweza kulisaidia baraza la mawaziri kufanya maamuzi ya maana, lakini wakati huo huo, wahusika wanaweza kuwa ni wazee au wanaumwa na hivyo hawawezi kuwa kwenye hekaheka za kila siku za kuongoza wizara kamili.

Kwa case ya prof. Mwandosya ni kwamba anaumwa. Kikawaida ungetegemea JK asimweke tena kwenye baraza la mawaziri. Lakini huenda kaona bado wanahitaji busara zake lakini pia hawawezi kumpa wizara kamili kwasababu bado hajapona.
 

Asante kwa ufafanuzi. Yaani vijana wa JF wengi vichwa maji. Hii inaonesha jinsi taifa lilivyokosa vijana wenye weledi wa kuchambua mambo kabla ya kutoa comments. JK amekuwa rais bora mwenye huruma sana na mchapa kazi.
 
Wanapeana vyeo kirafiki ila sio kwa kuangalia credibility ya mtu
 

Kuna vitu viwili hapa unachanganya. Kuwa mgonjwa na ukawa capable kufanya kazi (kutumiza majukuma yako). Pili kuwa mgonjwa na ukawa incapable kutimiza majukumu yako. Sheria za utumishi wa umma ziko wazi kabisa, mtumishi yeyote yule ambaye ni mgonjwa na hawezi kutimiza majukumu yake, mwajiri anapaswa kumuachisha kazi na kumlipa sitahiki zake zote. Hakuna mahala ambapo kunamtaka mwajiri ampangie kazi zisizokuwa maalamu mfanyakazi anayeumwa aliyeshindwa kutimiza majukumu yake. (Ref Waziri asiyekuwa na wizara maalumu).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…