Tanzania kwa vipindi mbalimbali imekuwa na mawaziri wasio na wizara maalum. Miongoni mwao ni marehemu Kawawa.
Pia nchi nyingine nyingi zina mawaziri wasio na wizara maalum. Miongoni mwa hizo nchi ni Uingereza ambayo kwa vipindi mbalimbali imekuwa na mawaziri kama hao. Serikali ya sasa ina mzee Ken Clarke.
Lengo hasa la hii nafasi ni kuwapa wale watu ambao uzoefu wao unaweza kulisaidia baraza la mawaziri kufanya maamuzi ya maana, lakini wakati huo huo, wahusika wanaweza kuwa ni wazee au wanaumwa na hivyo hawawezi kuwa kwenye hekaheka za kila siku za kuongoza wizara kamili.
Kwa case ya prof. Mwandosya ni kwamba anaumwa. Kikawaida ungetegemea JK asimweke tena kwenye baraza la mawaziri. Lakini huenda kaona bado wanahitaji busara zake lakini pia hawawezi kumpa wizara kamili kwasababu bado hajapona.
Je hao mawaziri waliochanguliwa huko nyuma wasiokuwa na wizara maalumu walikuwa WAGONJWA?! Maana hivi vituko vya JK kuchagua WAGONJWA havijaanza kwa Mwandosya. JK amewahi kumteua Mama mmoja kuwa Judge wa Mahakama kuu akiwa ICU. Leo nafikiri mwaka 4 tangu amteua huo Judge hajawahi hata kukanyaga ofisini achilia mbali kusilikiza shauri lolote.