Naishi na Mwanaume, tatizo nikimgusia suala la ndoa anadai nisubiri hayuko tayari kwa sasa

Pisi kali

JF-Expert Member
Dec 31, 2019
1,215
2,418
Habari zenu wanaJF

Waislam wenzangu A’alaykum (eid inanukia)

Niko na mtu tuna miaka mitatu hadi sasa tumepitia changamoto nyingi furaha na huzuni, kiukweli ni mtu ambaye hajawahi kuniacha hata hatua moja. Suala lililonileta kwenu.

Huyu mtu ni Muislam mwenzangu hamna changamoto zingine zozote isipokua kwenye suala la sisi kuhalalisha anakua mgumu mno (ndoa) ukimwambia tu basi tuhalalishe ni yuko muwazi yeye kwasasa hataki.

Huduma zote anatoa kuanzia matumizi (pesa) na huduma za chumbani, tunaishi wote. Shida ni hiyo tu hataki tuhalalishe ndugu zangu nifanyaje na kuachana nae siwezi japokua mwenyewe alinambia kama naona ananichelewesha basi anipe nafasi ndani ya muda fulani ikiwa bado sijaipata hiyo ndoa turudiane.

Hata funga yangu naona haiswihi kabisa maana tunaishi wote then tunafunga eti. Kwenye kila kitu mnakubaliana ila suala la ndoa hapo hataki anasema nivumilie.

Simuelewi! Au ana miiko. Niko hoves nimechoka kuzini

istockphoto-176830145-612x612.jpg
 
Ujue kuna jambo haliko sawa kwako, au kuna kitabia unacho ambacho kinampa Mashaka kuhalalisha kwa kuogopa mkiingia kwenye ndoa hicho kitabia kitaleta matatizo yeye kukwambia hawezi das why anakusubirisha tu kila mtu anahisi may be you can change later

Tunarekebishanaga mara kwa mara sasa hiyo tabia si angenambia tu
 
Ndo hapo wanapokosea wadada wengi! Wamekuwa cheap sana unakubali kuishi na jamaa na hapo unatarajia mfunge ndoa!

Kwa taarifa ya mtoa mada hii tabia yao ya kuishi kwa boifrend ndiyo imefanya vijana tusione umuhimu wa kuhalalisha/kuoa.

Itakua hivyo

Sababu hatukupeana space muda mrefu sana tumeishi wote muda wote huo

Ananiambia ndoa zipo tu na ndoa sio kila kitu
 
Hakupendi huyo ndio maana yupo tayari kukuachia muda utafute mwingine wa kukuoa. Lengo kuu la mahusiano hua ni mwisho wawili wapendanao wawe pamoja na kuanzisha familia.....Ukimpenda mtu kwa dhati kabisa muda wote unatamani umchukue/oe awe wako daima sasa kama mtu yupo tayari kukuachilia utafute wa kukuoa jua hakupendi. Yupo zake hapo kutimiza haja zake tena inawezekana hizo haja zake unazomtimizia ameshakina.

Wake up mate, Does this ain't ring a bell to you??

Itakua kweli hanipendi mimi pia nawaza hilo

Lakini sasa wanaume wote wanakasoro yeye kasoro yake ndio hiyo hataki kunioa naogopa nisije nikaolewa na mtu ambaye hatuendani vitu vingi huyu 99.9% vyote tunaendana tatizo ni hilo tu hayuko tayari na ananiambia kabisa sipo tayari kwasasa but i’ll marry you
 
unaishije na mwanaume kabla hajakuoa , hilo ni kosa kubwa ??
pia inaonekana dada umekufa umeoza yaani huambiliki .
anyway endeleeni kuzini mpaka mtakapo chokana .

Nachoogopa naweza kuachana na huyu nikampata mwingine ana mapungufu mengi zaidi

Najipa moyo ndoa hupangwa na Mungu maybe atanioa

Au nianzishe mahusiano mengine kimya kimya
 
Wanawake Suala la ndoa limekua TATA sana kwenu. Imagine hapo ukicheza vibaya unakua umepoteza miaka 3. Na uhakika wa kupata ingine at a time haupo pengine umri unakua ushakuacha hapo.

Mtu anakutumia kama mke na mume lakini kuihalalishia HATAKI haoni muda unaenda na sisi wanawake tunawahi kubadilika kimaumbile tofauti na wanaume
 
Back
Top Bottom