Naipongeza TFF sio timu ya Taifa (Taifa Stars).

Jacobus

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2011
Posts
4,709
Reaction score
1,735
Kwanza naanza na hili la kutoipongeza timu yetu ya taifa (Taifa Stars). Dhumuni la timu ni kushinda kila mechi dhidi ya timu pinzani kwa lengo la kunyakuwa kombe katika mashindano yoyote, sasa baadhi ya watu (hasa wenye 'access na media' wamejitokeza kuipongeza mno timu yetu kwa kuishinda timu ya Morocco juzi tu kwa 3-1 wakati bado tutakutana nao tena kwao, sipingi kuwapongeza hasa wachezaji kwani inawapa moyo lakini kwa hili INAKITHIRI. Hebu tuangalie matokeo machache huko Ulaya ya UCL round of 16:-
1. AC Milan 2 FC Barcelona 0 - FC Barcelona 4 AC Milan 0 => AC Milan nje na
2. Porto 1 Malaga 0 - Malaga 2 Porto 0 => Porto nje.
UEROPA round of 16:- Steaua 1 Chelsea 0 - Chelsea 3 Steaua 1 => Steaua nje.
Mifano hii ni kuwa timu inaweza kushinda nyumbani katika round ya kwanza na kushindwa/kutolewa katika round ya pili! Sote tulishuhudia jinsi AC Milan walivofurahia kutufunga katika round ya kwanza kwao lakini wapo nje.
Hebu angalia mfano huu katika FIFA world cup quarlifiers round 1 Ulaya, England 5 San Marino 0 - San Marino 0 England 8, lakini sijasikia Waingereza wakiipongeza timu yao kiasi tufanyavo sisi.
Sasa nije na pongezi zangu kwa TFF, hawa nawapongeza si kwa ushindi wetu dhidi ya Morocco ila nawapongeza kwa kukaa kimya kuhusiana na UCHAGUZI MKUU wake. Tokea wawe na kikao na wizara tarehe 19 March mwaka huu sijasikia wakisema mchakato wake, kama kuna mtu aliisha sikia namuomba anihabarishe tafadhari.
 
Jacobus, acheni Watanzania wafurahie jamani hiyo ni dalili ya kuchoka maumivu yakufungwa kila mara na hizi timu kubwa. Watz wanazo sababu nyingi za kufurahia kuliko kawaida zikiwemo;

1. Ni mara ya kwanza tangu dunia kuumbwa kuifunga Morocco. ( I stand to be corrected)
2. Ni ushindi mkubwa kwa kipindi cha takribani zaidi ya miaka 20 katika mashindano ya kombe la dunia
3. Ni ushindi mtamu ulioambatana na soka safi la kisasa na magoli ya kwenye video
4. Ni ushindi unaoiweka Tz ktk sehemu ya matumaini ya kuendelea na kampeni za kufuzu WC 2014 - Brazil
5. Ni ushindi uliodhihirisha kuwa kumbe Stars haikubahatisha kuwafunga Kenya,Zambia na Cameroun
6. Ni ushindi unazidi kuwafanya wachezaji wetu wajiamini zaidi na kuona kuwa kumbe wakizidisha juhudi na kujitunza
hakuna lisilowezekana.

Sasa kwa nini watu wasifurahi? Furaha,huzuni, hasira, n.k hazilazimishwi zinakuja tu kutokana na vichocheo husika.

Hata hivyo nakubali kwamba muda wa kusherekea ufikie tamati na badala yake tuendelee na maandalizi
 
Mkuu nimekuelewa na mie sipingi kuwa na furaha kwa ushindi (mie nimefurahi vilevile), ila tatizo nilionalo ni kuwa hatuli hatulali kwa ushindi huo kana kwamba tumechukua kombe!
 
Hacha watanzania wafurahie ushindi, kuhusu mechi ya marudiano hakuna anaejua matokeo. kumbuka ata burkna faso tuliwafunga nje ndani
 
Kwanza naanza na hili la kutoipongeza timu yetu ya taifa (Taifa Stars). Dhumuni la timu ni kushinda kila mechi dhidi ya timu pinzani kwa lengo la kunyakuwa kombe katika mashindano yoyote, sasa baadhi ya watu (hasa wenye 'access na media' wamejitokeza kuipongeza mno timu yetu kwa kuishinda timu ya Morocco juzi tu kwa 3-1 wakati bado tutakutana nao tena kwao, sipingi kuwapongeza hasa wachezaji kwani inawapa moyo lakini kwa hili INAKITHIRI. Hebu tuangalie matokeo machache huko Ulaya ya UCL round of 16:-
1. AC Milan 2 FC Barcelona 0 - FC Barcelona 4 AC Milan 0 => AC Milan nje na
2. Porto 1 Malaga 0 - Malaga 2 Porto 0 => Porto nje.
UEROPA round of 16:- Steaua 1 Chelsea 0 - Chelsea 3 Steaua 1 => Steaua nje.
Mifano hii ni kuwa timu inaweza kushinda nyumbani katika round ya kwanza na kushindwa/kutolewa katika round ya pili! Sote tulishuhudia jinsi AC Milan walivofurahia kutufunga katika round ya kwanza kwao lakini wapo nje.
Hebu angalia mfano huu katika FIFA world cup quarlifiers round 1 Ulaya, England 5 San Marino 0 - San Marino 0 England 8, lakini sijasikia Waingereza wakiipongeza timu yao kiasi tufanyavo sisi.
Sasa nije na pongezi zangu kwa TFF, hawa nawapongeza si kwa ushindi wetu dhidi ya Morocco ila nawapongeza kwa kukaa kimya kuhusiana na UCHAGUZI MKUU wake. Tokea wawe na kikao na wizara tarehe 19 March mwaka huu sijasikia wakisema mchakato wake, kama kuna mtu aliisha sikia namuomba anihabarishe tafadhari.

england hapongezw kw sabab giant hasifiwi kumfumua underdog, ila underdog anasifiwa kumfumua giant that z how it is.
 
Sawa mkuu ndio maana nimeuweka mfano huo wa England na San Marino ili je sisi tunavosherehekea kumfunga Morocco inaweza kuwa na San Marino siku watakavo ifunga England??
 
Katika final moja ya kombe la dunia, kuna team ya kiarabu ilichapwa 5 - 1, mfalme wa nchi ya kiarabu aliamua kutoa zawadi ya benzi new model. Kwa kuwa tu lilikuwa ni goli la kwanza kwa historia ya nchi katika final ya kombe la dunia.

Nakubaliana na mtoa hoja kuhusu swala la "celebrating while is too early" wakati vita inaendelea kwani inaweza kutufanya tuvimbe kichwa. Ila kuna wakati tunu inabidi tu ifurahiwe hasa unapokuwa underdog
 
Kweli mkuu, sisi tunavoonekana kana kwamba hatuna malengo. Kama lengo letu ni kushiriki (si kunyakua kombe) katika fainali za kombe la dunia basi mikakati ingewekwa kufikia lengo hilo na si kusherehekea ushindi wa mechi moja tu tena ya mwanzo kati ya mbili. Pana mdada mmoja aliisha sema kwenye radio moja hapa nchini kuwa hakuna kiongozi wa soka hapa ila wote ni wapenzi wa soka tu.
 
Back
Top Bottom