Naipenda Jumamosi yangu - Stori bomba ya uhusiano

Mahubiri yamekuwa mengi
nimejukuta nina scroll down tu... Ila kazi nzuri pamoja na mambo mengine naona muandishi ameamua kuonyesha nguvu ya maombi katika mahusiano
 
Mahubiri yamekuwa mengi
nimejukuta nina scroll down tu... Ila kazi nzuri pamoja na mambo mengine naona muandishi ameamua kuonyesha nguvu ya maombi katika mahusiano

Kwanini umeogopa kusoma maombi?
 
hatimaye mama Naomi bangi aloyokua amevuta imeisha makali
 
Mmmmmmh!!!
Unajua ulichoandika au umekurupukia ndotoni? Ungekuwa unajua kufikiria hata nje ya boksi husingeandika upupwu wako huu.. nipanic napata nini kwa ya humu!!!!!!!!
Wivu.com
Siku ingine tumia ID unayotumia kizaidi kubwabwaja humu.
Sasa Mbona unazidi kupanic.. Relax dada.
 
sawa tumekusikia tuta jaribu
 



SEHEMU YA AROBAINI NA NNE
Panakucha mama Naomi akiwa kalegea kila mahali, hajui hata aanzie wapi. Anachukua simuyake na kupiga ofisini anapofanyia kazi. Anaomba ruhusa kwaba ana dharura hataweza kwenda kazini, Anajisikia kichwa kinauma, hana raha wala furaha . Hajui hata afanye nini.
Ni saa kumi na moja asbh ameamka na kuanza kupiga hizo simu kwa wafanyakazi wenzake. Saa kumi na mbili bado yuko kitandani si kama kapumzika la hasha, ni mawazo yamejaa akilini kwake. Nifanyeje akili yake inaanza kukusaka wanawake ambao wamepitia changamoto na anamkumbuka wamama wengi tu ambao wameamua kuishi maisha yao, kivyao vyao ni kama wanawake sita hivi kwa haraka haraka, wengi ni wale ambao wanasema kuna ukimwi, sitaki kufa na ukimwi, sitaki. Na anaona ukimwi huu hapa,,hivi huu ujinga nani aubebe? Hivi nikifa na ukimwi hapa nitasema nini? Hivi huyu Marino ana mume mmoja tu? Hivi si atakuwa jalala la wanaume huyu? Sifi na ukimwi na sitaki ujinga.. Sitaki upuuzi,, mfyu. Anafyonza kwa nguvu. Kisha anaendelea kufikiri, na anamkumbuka mama Saimoniii, akili yake inatulia sasa anaanza kumtafakari mama Saimonii,, anajiuliza mengi akilini mama Saimonii kawezaje kuishi na mumewe na mumewe alimkosea sana? Kawezaje? Ngoja niongee naye aje anisaidie tu kuhusu ukimwi aje tu. Maana siku tayari kufa na ukimwi siko tayari.
Mama Naomi anampigia simu mama Saimoni na kumuomba afike amsaidie jambo. Mama Saimoni anapokea simu na kumpa taarifa kwamba amekimbia kwenye biashara zake tayari, ni saa kumi na mbili asubuhi mwanamke huyo tayari kashakimbilia biashara zake. Mama Saimoni ana kmgahawa ambao ni yeye peke yake anakisimamia. Hivyo ni lazima awepo kwenye biashara yake hiyo kuanzia saa kumi na mbili asubuhi ili kuwahi wateja wa chai asubuhi na mtori kisha chakula cha mchana na ikifika jioni afunge. Mama Naomi, nikitoka kazini na wewe ukitoka kazini tuwasiliane sawa? Mama Saimoni alimpa maelezo hayo;.
Siendi kazini niko tu nyumbani nimepumzika.. mama Naomi alimmjibu. Mama Naomi jamani, cha kukufanya usiende kazini ni nin sasa? Hembu amka, oga, jiandae nenda kazini, na Yesu akungulie, sikia mama yangu kukaa hakupunguzi kosa, ila kufanya kazi kunapunguza kosa kwa sababu bado unaenda kazini haijalishi una changamoto gani, hembu nenda kazini mamii, amka oga nenda kazini.
Maneno ya mama Saimoni yanamtia moyo mama Naomi na anajikuta anajiandaa haraka na kuondoka kuelekea kazini kwake. Mama Naomi anafika kazini akiwa yuko na mawazo lakini anapofika pale pilika pilika za kazini zinampa kuwa busy na mara jioni hii hapa imeingia. Anamigia mama Saimoni simu na mama Saimoni anamwambia wakutane nyumbani jioni.
Ili waweze kuongea na kutiana moyo tena. Mama Naomi walau sasa ana mahali pa kupumulia, mahali ambapo panampa mwanga, japo ana maswali mengi kichwani kwake juu ya changamoto yake lakini walau kidogo ana mtu wa kumuuliza.
Jioni inafika, na wanakutana nyumbani kwa mama Naomi ili waongee, na swali kubwa la mama Naomi ni je atajikingaje na ukimwi kwa mwanaume ambaye ni mzembe kiasi hicho? Na ambaye hajali kulala na wanawake?
Sikia mama Naomi, yani kama kuna watu wenye bahati ni wanawake ambao wanajua ubaya wa waume zao na uzinzi wao, kuliko mwanamke ambaye mume ni mzinzi na hajui. Hivi ambaye hajui hapati ukimwi? Hivi kama usingejua usingepata ukimwi? Si bora umejua mume ana tabia za uzinzi hivyo, kwanza unaweza kumuonya, unaweza kutumia kondom ama la unaweza kumuombea. Hivyo ni bora umejua tabia zake mbaya za uzinzi alizo nazo ili sasa ufanye maamuzi sahihi katika kumsaidia kwenye kumshauri, kumuonya ama kumuadabisha. Ni mume wako,ongea naye. Mueleze namna ambavyo amekosea, msaidie, kwa sababu swala la mtu kuwa muaminifu ni swala la mtu binafsi, unaweza usione, usijue wala kuhisi kwamba mume ni mzinzi lakini akawa mzinzi wa kutupwa na kujificha sana, na akikutana na magonjwa ukayakwaa nab ado watu wakashangaa mbona walikwua wakiambatana na kuwa karibu hivyo ukimwi wametoa wapi? Na ndio maana nataka kukusaidia kwamba katika maisha tuliyo nayo haya , ni bora kuwa na tegemeo ambalo ni Yesu peke yake, Yesu akufiche kwenye mbawa zake, ndio maana nataka uanze kujifunza kuisha maombi na kuishi kumpendeza Mungu ili sasa yale mambo ambayo akili zetu hayawezi Yesu pekee aingilie kati. Sijui kama unanielewa?
Mama Naomi alitulia kidogo kisha akamtazama mama Saimoni na kumwambia kwa hivyo unataka kuniambia ujue mume ni mzinzi na uendelee kuishi naye?
Mama Saimoni alitabasamu na kumwambia mama Naomi, uitakaje mpenzi? Ulitaka nikuambie achana naye? Kamwe siwezi kukuambia achana na mumeo, lakini ninachoweza kukuambia ni kwamba uwe na akili ya kujua na kuweza kupambanua mambo .Jua mumeo uzinzi anaufanya kwa sababu zipi, ukishajua hilo ni rahisi kutatua tatizo na tatizo kupata majibu. Ndio maana nakuambia huyo ni mumeo, kaa naye ongea naye msaidie yamkini kakamatika mahali. Hujiulizi imekuwaje hakuwa mzinzi na leo kaanza matabia mpaka ya kulala nje? Wewe kama mke na kama mlinzi hujui kazi yako ni nini? Hivi unajua anguko na angamizo la mumeo linakudhuru hata wewe? Ama hujui hilo? Na ukiona mume kafuatwa jua anayetafutwa ni wewe na wanao tu basi na si vinginevyo na ukiachia mlango wazi ukasahau wewe ni mlinzi kama maandiko yanavyosema mwanamke atamlinda mumewe aisee anguko linalotokea siwezi kuuelezea. Biblia ilipomuita mwaname mjenzi ilijua kabisa ni mwanamke ambaye anaweza kujenga, ni Injinia na sio saidia fundi hapana ni Injinia hasa. Sasa kazi ni kwako ndoa yako ni kama gorofa angalia wapi ufa ukiwa mkukbwa utaleta madhara , na ndio maana nataka kabla hujaanza kupaka rangi anza kufanya plambing, weka pipe za kupitisha nyaya za umeme umesikia mamii? Alafu rangi inakuja baadae ukiwa umeshapitisha nyaya zako ndani ya kuta, wewe ni mjenzi. Ninachoweza kukuambia wewe ni mjenzi. Usikubali kujenga mjengo wako kizembe. Hembu inuka na anza sasa. Hakuna fundi ama mjenzi ambaye hana makovu, haumii, hana sugu. Kila mjenzi , kila fundi ambaye anajenga ni lazima awe anakwaruzika, anatobolewa na misumari, anaanguka, anachafuka, lakini mwisho wa siku ukiangalia mjengo aliojenga fundi huyo lazima ukuvutie sana. Amka, inuka, simamia ndoa yako mami simama kidete ili Jina la Mungu lisitukanwe. Mama Saimoni alimueleza mama Naomi maneno hayo, na Mama Naomi alionekana kuelewa, Alichukua simu yake ambayo ilikuwa kwenye chaja, na kutafut a namba ya mume wake na kisha akamwambia mama Saimoni,,
Mama Saimoni kwa hivyo natakiwa kumsamehe sio? Mama Saimoni alicheka akasema hivi kumbe bado hujatangaza msamaha mpaka sasa?
Hembu kwanza muandikie ujumbe mmoja, Mwambie tu unamsalimia kisha mwambie umemsamehe.
Mama Naomi aliuliza naandikaje? Mama Saimoni aimmwambia msalimie, mshukuru kukupatia pesa za matumizi, muombe msamaha kwa kukwaruzana, kisha mjulishe umejua amezini na Marino na umtangazie msameha. Na usiache kumwambia unampenda, umesikia,, Mama Saimoni alimaliza kisha akatabasamu na kufuata picha moja ambayo alikuwa amepiga mama Naomi na mumewe wakiwa wanatabasamu, akawa anaiangalia, huku nako Mama Naomi alichukua simu yake na kumuandikia mume wake ujumbe. Ufuatao baada ya kupata maelekezo kutoka kwa mama Saimoni.
Habari baba Naomi, bila shaka umefika salama, Sisi na watoto hatujambo tunaendelea vizuri. Asante kwa pesa za matumizi ulizotuachia. Unaendeleaje wewe? Jana ulipoondoka nyumbani tulipishana na kukwaruzana, ninaomba unisamehe,. Nimekusamehe pia kwa kugundua umezini na Marino. Nimekusamehe. Nakupenda , Uwe na amani jioni njema.
Baada ya mama Naomi kumaliza kuandika, mama Saimoni alimwambia Mama Naoami aliisome ile meseji kwa nguvu, Mama Naomi aliisoma huku akilia machozi, alilia sana, Mama Saimoni alimwambia , sikia, kuna mambo katika ndoa yangu nilikuwa nayafanya kama ujinga Fulani hivi, lakini yalifanyika nguvu na Baraka, unajua katika maneno kuna nguvu, hembu sema tu maneno yoyote juu ya huo ujumbe ambao unautuma kisha utume. Yani uombee huo ujumbe. kabla ya kuituma Hiyo meseji. Mama Saimoni alimwambia mama Naomi hivyo, kisha mama Naomi akiwa kashikilia simu akasema, Eee Mungu mimi siwezi mambo ya maugomvi, siwezi hizi aibu naomba msaidie huyu mwanaume aache uzinzi Yesu, mama Naomi alikuwa akilia, Mama Saimoni alimtazama akilia na kumwambia nipe hiyo simu nitumie mamlaka ya Jina la Yesu, nipe hiyo simu, nilikuwambia jana kwamba HAPANA JINA LINGINE TULILOPEWA WANADAMU LITUPASALO KUOKOLEWA KWALO , JINA LA YESU LINA NGUVU SANA HEMBU NIPE MAANA HII VITA KWANGU NI YA KITOTO SANA, NIPE HIYO SIMU. Mama Naomi alimshangaa sana mama Saimoni alivyokuwa na ujasiri wa kujivunia jina la Yesu.
Mama Saimoni alishika ile simu na Kusema, ee Yesu, umesema katika kitabu chako kwamba, lolote tuliombalo tuamini limekuwa letu, Yesu ninatumia jina lako takatifu sasa kuomba ufahamu katika akili ya baba Naomi, ajue kwamba kuwa na mahusiano nje ya ndoa yake ni dhambi,Yesu naomba fungua ufahamu wa baba Naomi mara atakaposoma ujumbe huu, ajue kwamba amemkosea mke wake, lakini ajue kwamba amekukosea wewe zaidi na pia Yesu naomba mfungue ajue kwamba uzinzi ni dhambi. Yesu nashukuru kwa sababu ujumbe huu unaenda kufanyika Baraka na ufahamu kwenye akili ya baba Naomi ameni. Mama Naomi haya tuma mama yangu ujumbe wako, Mama Naomi alipokea simu na kutuma ule ujumbe, kisha akatulia kusubiri majibu. Sikia mama yangu naomba nikuache, kuna kazi naenda kuuifanya nyumbani. Nina muda mrefu sijakagua mashati ya baba Saimoni kama yana vishikizo ama la, nataka kwenda kukagua walau mashati machache niyawekee vifungo kuna ambayo niliona hayana vifungo. Mama Saimoni alimuaga mama Naomi ambaye alikuwa akiendelea kumshangaa mama Saimoni. Mama Saimoni alitoka akaondoka zake.
***********************************************************
Siku ya kwanza imepita tayari, Marino hajawasiliana na Daniel, Daniel alimtafuta sana kwenye namba yake, kisha alipiga simu hotelini na akaambwia kwamba ile mizigo kuna mwanamke ambaye alienda kuichukua, na mwanamke huyo ni Marino mwanamke ambaye alikuwa amelala naye hotelini hapo. Alipopata taarifa hizo aliendelea kumtafuta sana Marino bila mafanikio yoyote. Daniel akiwa chumbani kwake amepumzika baada ya kazi kubwa siku hiyo ambayo kampuni ilimtaka kufanya, alichukua simu yake na kuandika jumbe kama tatu za mapenzi kumtumia Marino. Na akiwa katika kuandika ndipo sasa ujumbe unaingia, ni ujumbe kutoka kwa mke wake. Anausoma, nan i kama haamini anachokisoma. Kwa siku chache alizokumbana na mkasa wa mkewe kujua amelal ana Marino alikuwa akichezea matusi makubwa makubwa sana, matusi ambayo yalikuwa yanamuuma moyoni, ni kweli kakosea lakini aina yamatusi aliyokuwa akiyapata alihisi mke wake kapagawa. Leo anasoma ujumbe wenye utulivu kiasi hichi, Anarudia mara ya pili nay a atatu, anarudia mara ya nne. Kisha anaamua kusoma kwa nguvu akiwa chumbani kama ambaye ameambiwa amsomoee mtu ili asikie.
“Habari baba Naomi, bila shaka umefika salama, Sisi na watoto hatujambo tunaendelea vizuri. Asante kwa pesa za matumizi ulizotuachia. Unaendeleaje wewe? Jana ulipoondoka nyumbani tulipishana na kukwaruzana, ninaomba unisamehe,. Nimekusamehe pia kwa kugundua umezini na Marino. Nimekusamehe. Uwe na amani jioni njema.”
Baba Naomi ni kama haamini, anavua miwani yake, anafikicha macho yake, anashika simu yake na kutoka chumbani na kuelekea kwenye kisebule kiilichop chumbani kwake, anasoma tena ule ujumbe. Nini kimetokea, ni mama Naomi huyu ama. Baba Naoni ajishika kidevu chake na kukkikuna kama ambaye anatafakari kwa njia hiyo,, anaachia tabasamu kisha anaketi kwenye sofa. Akiwa ameshikilia simu yake anajiuliza, ajibu kwa ujumbe ama apige, lakini ajibu nini? “NIMEKUSAMEHE PIA KWA KUGUNDUA UMEZINI NA MARINO” kaujumbe haka kafupi sana kanamfanya sasa anajisikia aibu kubwa mno, siku zote katika malumbano yao hakuwahi kuona hili kosa, lakini leo ujumbe mfupi sana umemuelezea makosa yake yooote, Anasikia aibu, anasikia kujua amekosea sana, Nimpigie simu? Nimuombe msamaha? Nimwambieje? Baba Naomi alikuwa akitafakari afanyeje,, je nikane sijazini? Mbona inajieleza kila kitu? Hivi kweli amenisamehe ama kuna kitu anataka kufanya malipizi? Hivi kweli ananipenda ama ni kunisanifu? Anawezaje kujua nimemkosea kikubwa hivi alafu asema ananipenda? Daniel alikosa amani, alikosa amani, Alichukua simu yake na kuandika ujumbe,,, ASANTE MKE WANGU KUNISAMEHE, ASANTE SANA. NASHUKURU, NAKUPENDA PIA.
Alimtumia mkewe ujumbe huo huku moyo wake ukiwa na huzuni sana na alikuwa akiklia ndani kwa ndani japo machozi yalikuwa hayatoki nje. Mama Naomi alipoona simuyake imeingiza ujumbe alisoma ule ujumbe na mara moja alimpigia mama Saimoni simu na kumwambia mumewe kamjibu na akamsomea ujumbe ule ,
Safi sana, Asante Yesu, nimefurahi amejibu,mwanzo mzuri, hongera umejibiwa, lazima ameelewa ameelewa. Mama Saimoni alimpongeza mama Naomi. Sasa nimjibu? Nimjibu nini? Mama Naomi ni kama alikuwa anataka maelekezo kwa mama Saimoni. Mama Saimoni alicheka ha ha ha,, unanichekesha kweil mamii mumeo huyo,, jana nilikuambia jua mapenzi, jua kuuongea vizuri, maneno mazuri ni afya hivi husomagi maandiko mamii? Kuna nguvu ya ajabu katika kinywa chako, hasa wewe kama mwanamke jifunze kinywa chako kuwa na afya ili uponye na wengine umesikia mamii, Yani mbona nina kazi? Wacha nije kukufunda, yani nije kabisa kukufunda ama nikupeleke kwa Kungwi lao ukafundwe. Kungwi lao, kufundwa? Mama Saimoni aliongea kwa mfululizo mpaka akamchanganya mama Naomi, mama Naomi akawaza, Huyu mara maombi, mara kungwilao, mh,, mama Naomi kama anapata kujiuliza, ukungwi tena, mambo ya Kiswahili? Mbona huyu mama anaomba vizuri sana? Mbona kaokoka huyu mama? Sasa kungwi tena? Mh.. Mama Naomi anawaza. Mbona kimya? Mama Saimoni anamuuliza mama Naomi baada ya kuona kanyamaza kama sekunde kumi hivi.. Hapana, niko sawa, niambie nimjibuje? Nisaidie tu dada yangu maana akili hii sio yangu, yani sio kabisa, nisadie..Nisaidie tu. Mama Saimoni akamwambia, una Biblia hapo karibu? Ndio mama Naomi akajibu na kwenda kuifuata Biblia sebuleni kwenye shelfu za vitabu,, ninayo mamii niambie.
Hembu andika hii milango alafu utaisoma pole pole nataka ujue nguvu ya maneno yako mdomoni katika kuongea na mumeo. Uone maneno yalivyo na nguvu, sitaki uwe na maneno ya matusi ama kashfa, nataka uwe na maneno machache ambayo ni afya,
Umepata kalamu? Mama Saimoni alimuuliza, ndio nimepata mama Naomi alijibu,, oky haya anza kuandika mamii.
Fungua Mithali 18: 20-21, Yeremia 1: 8 -10, Zaburi 34: 12- 13,Mithali 15: 30, Mithali 16; 24,Mithali 25:11,12, 15 Mithali 31: 26. Mama Saimoni alimtajia mama Naomi hayo maandiko kwa kasi ya ajabu, huku mama Naomi akimwambia pole pole, Naalipomaliza alimwambia umemamaliza kuandika ama nirudie? Rudia, nimemaliza ila rudia nihakikishe,, Mama Naomi alimuomba mama Saimoni arudie ile mistari ili aiandike kwa usahihi, na mama Naomi alirudia na kuandika kwa usahihi, japo ni mistari michache tu alikosea, huo wa Yeremia aliandika mithali badala ya Yeremia.
Sawa sawa, naomba usome ukiwa umetulia alafu kama hutaelewa basi nitakuja kukuelewesha kesho nikotoka kazini, nina tenda ya kupikia wafanyakazi kiwandani wana sherehe, hivyo nikitoka jioni kama nitakuwa sijachoka nitapitia nikufafanulie, wewe soma tu umesikia? Mama Saimoni alimsisitiza mama Naomi asome . Sawa nimesikia. Mama Naomi alichukua Biblia yake na kuanza kusoma mstari mmoja baada ya mwingine, aliambiwa juu ya nguvu ya Maneno na ulimi wake. Alianza kujikuta akisoma maandiko matakatifu kwa kumaanisha, ni kweli huwa anaenda kanisani lakini biblia ataishika jumapili kwa jumapili tu, Biblia yake bado mpya sana, haiguswi wala kusumbuliwa n i siku za jumapili ataibeba na wakati mwingine wala habebi anatumia simu yake kusoma maandiko matakatifu. Hivyo Leo ni kama anapasa kazi ya kuanza kufungua Biblia kwamara ya kwanza kwa kumaanisha baada ya kufanya hivyo miaka mingi kidogo. Anakaa sebuleni kwenye meza ya chakula huku akifungua mandiko yale na kuyasoma. Andiko la kwanza alilofungua lilisema, “Mauti na uzima viko katika uwezo wa ulimi, na wao waupendao watakula matunda yake, Kisha akasoma andiko lililofuata, Akafungua kitabu cha Yeremia, 1 mstari wa 8mpaka wa 10, Akalisoma pole pole, alipomaliza kusoma akarudia tena, ni kama anaelewa sasa, akatulia na kurudia tena, Neno hili mbona kama linakuja kwake kama Unabii,, ameambiwa asiogope, na mama Saimoni kamambia ulimi wake unanguvu,, mama Naomi alitulia, akachukua simu yake iliampigie mama Saimoni,, Akapiga namba za mama Saimoni, Mama Saimoni akapokea na kumwambia, kuna kazi anafanya amekamatika . na watongea kesho. Mama Naomi neno hili limeushika moyo wake sana, Anaendelea kusoma mistari mingine yote na anaangalia saa yake ni muda wa kulala yani hata hajaoga, wala hajala , watoto walikula na wameenda kulala, Aliamka na kwenda vyumbani kuangalia watoto wake na kisha kurudi chumbani kwake na kuingia bafuni na kuoga. Ni saa sita kamili ndipo anajitupa kitandani baada yakunywa glass ya maziwa na vipande viwili vya mkate, jana yake hakulala , juzi yake hali kadhalika, na leo ni saa sita usiku, Anachukua simu yake anajiuliza atume ujumbe kwa mume wake ama alale tu? Anaamua kulala tu asije akajikuta analikoroga maana anajijua kwa maneno yake mabaya , yamkini akakosea hivyo alisema anasubiri mwailmu wake ama kungwi wake amsaidie nini cha kufanya. Anajibwaga kitandani na usingizi msito hasa unampata.
*********************************************
Waooo, siku mbili nimefanikiwa kabis kufuata masharti, sijatoka ndani kabis, sijawasiliana na mtu kabisa, safi sana, Nilisimama na kwenda kuangalia pete yangu nilipokuwa nimeiweka,, waoooo, niichukua na kusema maneno ambayo niliambiwa niyaseme, kisha nikanywa na ile dawa ambayo niliambiwa ninywe huku nikisema maneno yale kwenye ile pete, kisha nikaivaa kidoleni kwangu na kusema mimi na Daniel daima tusiachane, anisikilize mimi tu. Anipende mimi tu. Nilimaliza kuongea na kuitoa ile pete na kuiacha kidoleni kwangu. Niliamini sasa nimeshakuwa msindi, ni siku sijaongea na Fadhili, sina haja naye, nina haja na Daniel, ni asbh sana nilichukua simu yangu na kumpigia Daniel , Daniel alipokea, na alikuwa down sana,, mambo Daniel? Salama kabisa Marino, nimekutafuta sana, mbona hupokei simu zangu?Daniel alimhoji Marino.
Samahani sana mpenzi, nimekuwa na pilika pilika, nikasema nimalize kisha niwe na wewe full full kama hivi,, sasa yani vitu vyote vilivyokuwa vinanisumbua nimevimaliza mpenzi wangu nakusikiliza wewe tu na hata kama unataka nije Uganda nakuja mpenzi. Nilimueleza Daniel kwa furaha zoote, nikijua nimeshamkomesha na kwangu hafurukuti. Weee,, unaweza kuja Uganda? Daniel ni kama alipagwa aliposikia nimemuambia kuhusu kwenda Uganda,,
Ndio naweza, wewe ni mpenzi wangu, sina mpenzi mwingine kwa nini nisije? Niambie tu kama unanihitaji niko kwa ajili yako, niambie tu mpenzi. Daniel kusikia hivyo akaniambia basi sawa, Naomba nitoke kwenye kikao mchana kisha nikujibu. Sawa mpenzi? Sawa niilimjibu, tena nikuletee na Pete yako maananaona inazua ugomvi,, Na mimi sitaki ikuletee ugomvi na mke wako. Nilipiga picha nyingi sana kwa kutummia simu yangu mpya niliyonunuliwa na Daniel, simu inayotoa picha vizuri sana, na kumtumia Daniel picha nyingi sana, zingine nikiwa na khanga tu, ili kumpagawisha, ninajua yuko peke yake, hivyo nikimpagawisha kisha nikimwambia naomba kwenda nilijua hawezi kamwe kunikatalia, na kuku nimeweka picha zaangu kwenye profile yaw hats app za kutosha huku vidole vyangu vya mikoni vikiwa na kucha za kubandika na rangi nzuri ya kucha tunaita rangi ya jeli. Na zile pete kuonekana vyema.
Marino alipiga picha nyingi sana za selfie huku ile pete ikiwa kenye kidole chake, na zile zake zikiwa kidoleni pia, kiasi kwamba kama Mama Naomi akiwa mchunguzi na mpekuzi lazima ataiona ile pete ya Daniel yaani mumewe kwenye kidole cha Marino.


Inaendelea sehemu ya Arobaini na tano.
Post #1432
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…