Naipenda Jumamosi yangu - Stori bomba ya uhusiano

SEHEMU YA 43
View attachment 1151078

SEHEMU YA AROBAINI NA TATU.
Mama Naomi alibaki na watoto wake, akili yake ilikuwa imelemewa sana na mawazo tangu siku tatunne hapo nyuma.Alikuwa anawaza mambo mengi sana, alikumbuka namna ambavyo mama Saimoni alivyopitia kwenye changamoto kubwa ya ndoa yake, na anakumbuka wakati huo alipokuwa anayaona hayo aliuwa anasema … mimi mwanaume haninyii hivi, mimi sio wa hivi,, lakini leo nay eye anakumbana na changamoto hii na yuko ndani ya ndoa na hafanyi lolote zaidi ya kupata wehu wa muda lakini bahati nzuri sana anakutana na mwanamke kijana mwenye kitu cha kumwambia.
**********
Ni vyema kila mwanamke akawa na roho ya utiaji moyo,moyo wa ushauri na moyo wa kusaidia, . Mwanamke huyo anaenda kwa Lipina na hapati msaada wowote ulena alilala usiku mzima kule, na anakutana na mwanamke mwingine kijana ambaye kwa masaa machache ameweza kumuonya, kumelimisha, kumkaripia na kumuombea, Mwanamke ambaye amejaa maarifa,na anamuacha mama Naomi akiwa na ahueni,na jambo la kwanza kabisa analofanikiwa kumshauri ni kukubali kukabili changamoto, kitu ambacho sio wanawake wengi ambao wako tayari kukabiliana na changamoto bali kuzikimbia changamoto.
Naomi anachukua watoto wake na kuhakikisha wanalala kisha nay eye anaingia chumbani kwake, na kupanda kitandani.
Kuna mambo ukiruhusu yakiingia moyoni yatakugharimu kuyatoa.
Unapoacha moyo wakoukaingiza vitu ni ngumu kutoa vitu ndani ya huo moyo. Gharama za kulinda moyo zinaweza kuwa kubwa sana lakini sio kama gharama za kuruhusu jambo liingie moyoni alafu ulitoe. Mama Naomi kama angetumia gharama kulinda moyo ingekuwa ni afadhali kwani moyo ukilindwa vyema unaepuka mambo mengi, na ndio maana maandiko yanasema Linda sanamoyo wako kuliko vyote ulindavyo maana ndipo zitokako chemichemi za uzima . Kujaza vitu moyoni kunaziba zile chem chem za uzima. Mama Naomi hakufanya kazi ya kulinda moyo, na badala yake moyo wake ulikuwa umejaza mume ndani, na kuamini kabisa chem chem za uzima wake ni mume kumbe sio . Mama Naomi analia usiku kucha kitandani, anakumbuka maisha yake ya ndoa siku za nyuma, anakumbuka maombi aliyofanyiwa na sasa kaambiwa asamehe,, anajiuliza nitawezaje kusamehe? Kusamehe ni jambo linalohitaji hatua kwanza,
1. Kuamini kabisa kwamba kama hutasamehe na wewe huwezi kusamehewa.
2. Pili unayemsamahe umsamehe haijalishi atajua kosa lake ama la kwa maana kwamba hata asipokuomba msamaha umsemehe tu.
3. Lakini hata akirudia kosa wewe unatakiwa kusamehe tu.
Ni jambo zito sana hili. na.linahitaji mwanamke ambaye amekomaa Kiimani.
biblia inasema vaeni Ngao ya imani. ili kwa hiyo muweze kuizima mishale.yooye ya moto. hivi huoni sasa imani yake ni dhaifu na si thabiti hata kufuhusu mshale wa moto wa mume kumchoma na kumjeruji kiasi hiki.

Hizi hatua sio kitu cha siku moja wala mbili, ni kitu ambacho kinamhitaji mhusika kugangwa moyo wake. Maandiko yanasema, Mungu huganga miyoyo iliyojeruhiwa. Mama Naomi ni lazima aanze uponyaji wa moyo wake. Akishapata kuponywa na kugangwa jeraha zake itamsaidia sana kuweza kuendelea mbele kwani ndio mwanzo wa kuweza kulinda moyo wake. Mama Naomi anakosa usingizi kwa kuwaza ukubwa wa tatizo. Anamuwaza mume wake namna kamgeuka, anawaza namna mume wake alivyokuwa na mwanamke na zile sauti zinajirudia masikioni mwake, lakini anakumbuka shukrain ambazo Marino alizitoa kwa mumewe, kwa kupata penzi tamu lakini kupewa zawadi ya simu . Hivi vitu vinaisonga akili yake sana, na analia sananakushindwa kunyamaza kabisa.
KUSAMEHE, KUSAMEHE KUSAMEHE . Kusamehe ni kazi kubwa sana, ni lazima mtu uwe na ulinzi mkali sana kwenye moyo. Linda sana moyo wako kuliko vyote ulindavyo,, maana ndiko zitokako chem chem za uzima. Kumbe hatutakiwa kulinda mume kuliko moyo, hata kama mume tutamlinda lakini alindwe na moyo ambao unalindwa, maana ndiko zitokako chem chem za uzima . “Linda moyo wako kuliko vyote”, vingine tulinde lakini MOYO Kuliko vyote…
Neno la Mungu linasema WANA AMANI TELE WALISHIKAO SHERIA YABWANA , WALA HAKUNA LA KUWAKWAZA.. Jambo la kukusaidia ili uweze kusamehe ni kuishika Sheria ya Bwana,, kwani itakupa amani kwa sababu hakuna la kukukwaza. Hivyo moyo ili ulindwe ni lazima SHERIA YA BWANA UISHIKE.
Lakini maandiko matakatifu yanasema tena, Neno la Mungu ni taa ya miguu yangu na mwanga wa njia zangu,, na akasema tena, Moyoni mwako nimeliweka neno lako nisije nikakutenda dhambi,, na mahali pengine akasema,, NENO LAMUNGU NA LIJAE KWA WINGI NDANI YAMOYO KWANI
Huko ndiko kulinda moyo. Neno la Mungu lijae moyoni kwani Neno linafundisha, linahusisha, lina adabisha, lina onya pia.
Kukosa Neno moyoni ni matokeo ya kushindwa kusamehe.
Mama Naomi angetumia gharama nyingi kulinda moyo asingekutana na gharama za kushindwa kusamehe.
Ngoja nikupe ushuhuda kidogo wakwangu kama muandishi wa Mkasa huu wa naipenda jumamosi yangu
Nakumbuka mwaka 2008, Mwezi wa Saba nilikutana na changamoto ambayo mimi sikuionani changamoto kabisa, japo ndugu, marafiki , majirani waliona niko kwenye changamoto kubwa sana na wengine walijua kabisa ndio imefika mwisho wangu wa mafanikio katika afya , uchumi, ndoa na hata malezi ya watoto. Wengi walijua nimekwisha.. Unamuona mtu anavyoongea na wewe tatizo na changamoto sio yake lakini kachanganyikiwa , ana hasira kuliko wewe ambaye una changamoto hiyo. Lakini nakumbuka jambo moja tu ambalo lilinisaidia katika changamoto hiyo ambayo wengi waliamini kabisa, SITAWEZA KUSAMEHE KABISA.
Jambo ambalo lilinisaidia katika changamoto hiyo ni limoja tu, KULINDA MOYO.
Moyo wangu ulikuwa umelindwa kikamilifu na hakuna dhaifu, hata moja ambalo lilipatanafasi ya kuingia ndani ya moyo na kuujeruhi moyo huo. Na walinzi ambao walikuwa wakilinda moyo ni KUSOMA NENO Huyu ni mlinzi ambaye huwa nasema analinda upande wa Kaskazini.
, Ninapenda kusoma maandiko matakatifu sana, yani ni lazima nisome maandiko matakatifu kwa style ya ,
(i). Kujua historia ya Walioandikwa kwenye Biblia.
(ii)Kusoma kwa kufundishwa kanisani ama kwenye semina.
(iii)Kusoma kwa kufundishwana Roho Mtakatifu mwenyewe, ,kwa maana ya kujifungia ndani na kusoma maandiko nikiwa nimetulia.
Hivyo mlinzi huyu wa kuulinda moyo wangu alikuwa imara na nilikuwa na maneno mengi ya kunijenga , kunifariji, kunionya na kunitia nguvu. Hivyo hata ndani ya changamoto hii nilikuwa imara kwa sababu tayari nilikuwa nina maneno yenye nguvu ambayo yaliujaa moyo wangu.
Lakini pia Neno la Mungu ni taa na mwanga, hivyo nilikuwa naweza kabisa kupata maelekezo niendeje, nikanyage vipi, madhara ya tatizo nayaona na kuyakabili na kujua ukubwa ama udogo ama madhara mbeleni . Hivyo Neno la Mungu likijaa ndani ya moyo wa mtu ni msaada tosha.

Lakini mlinzi namba Mbili ambaye huwa namuita ni mlinzi ambaye amesmiama Kusini ni MAOMBI
Mlinzi huyu Maombi ni mlinzi ambaye kazi yake ni Kuniimarisha, Ninaomba bila kukoma, si ngoji mpaka nikutane na changamoto ndipo niombe , la hasha, nimejijengea utaratibu wa kuomba daima, kuomba kila wakati kuomba kuomba kuomba,na katika kuomba huko naomba kama sitaomba tena, Naomba kama ambaye nafasi ya kuomba sitaipata tena. Maandiko yanasema Ombeni bila kukoma, ombeni kila wakati, kesheni mkiomba. Hivyo ninakuwa nahakikisha naomba daima. Neno la Mungu linasema katika 1 Wakorintho 14: 4 “ Yeye anenaye kwa lugha hujijenga nafsi yake” Maana yake ni kwamba, unapokuwa kwenye maombi na inapotokea unanena kwa lugha unaijenga nafsi yako, na ni katika kuomba ndipo ambapo Roho wa Mungu hutuombea kwa mlio usioweza kutamkikwa Rumi 8:26 -27 . Roho hutusaidia, Roho anaona zaidi yetu, anajua, hivyo unapokuwa unaomba na kujipatia muda mzuri wa utulivu kwenye kuomba ndipo mahali na wakati ambao Roho Mtakatifu hukusaidia inavyopasa. Hivyo unaimarika zaidi na zaidi, Moyo unakuwa na ulinzi wa kutosha.
Lakini jambo lingine katika kuulinda moyo ninaye mlinzi mwingine wa upande wa Mashariki, Mlinzi huyu ni MAOMBI YA KUFUNGA.
Ninapoamua kulinda moyo wangu ili utoe chem chem za Uzima ninahakikisha pia ninakuwa mtu wa kuomba na kufunga mara kwa mara, Kama mama na kama mke ninakuwa na maombi yangu ya mwezi kama ifuatavyo.
Nina kuwa na maombi ya mapatano kutoka kwenye vikundi vyangu vya maombi na wanawake wenzangu. Lakini ninakuwa na maombi yangu binafsi ya siku saba kwa maana ya masaa 12 kila siku kwa siku saba katika mwezi,
Na katika maombi haya ninakuwa na maombi ya mfululizo ya kufunga tu. Na
1. Ninajiombea binafsi.
2. Naomboa mume wangu.
3. Naombea Huduma yangu.
4. Naombea watoto wetu.
5. Naombea Afya zetu.
6. Naombea uchumi wetu.
7. Naombea Nchi yangu.
Haya ni maombi ambayo yanafanyika kila mwezi kwa siku hizo saba kwa kuomba hasa kila siku nabeba hitaji moja moja. Na hi inakuwa ni ulinzi mkubwa ndani ya moyo wangu kwamba, Mume, huduma, watoto, afya, uchumi hauwezi kwamwe kuwa mwiba katika maisha yangu kwa sababu tayari nimefanya ulinzi ambao ninajiwekea mazingira ya kuwa salama ,hata tatixzo linapotokea kumbuka Roho huniombea kwa kuugua kwani siwezi kuomba ipasavyo, na hata jambo likijiinua katika hayo hapo ninakwua Imara kwa sababu nina amani tele moyoni mwangu. Amani ambayo imeshajitengeneza.
Lakini ninakuwa na maombi ya siku tatu kavu, kwa maana ya masaa 72 bila kula kitu chochote, Maombi hayani special sana. Ni maombi ambayo huwa ninayafanya pale ambapo ninaona jambo Fulani linakuwa gumu, hivyo nachukua lile andiko linalosema kwamba lakini mambo mengine hayatoki ila kwa kufunga na kuomba. Hivyo Haya nayafanya kispecial zaidi, ikibidi hakuna kusafiri ama kutoka nje ya nyumbani ili niwe katika hali ya utulivu sana, Na ndani ya haya maombi mara zote ninapoyafanya ndipo ninapata maonyo hasa, taarifa, maelekezo na mafunuo mbali mbali katika huduma ninayoifanya pia. Hivyo huyu naye huwa namuita Mlinzi wa Kuulina moyo wangu.
Lakini yuko mlinzi mwingi wa upande wa Magharibi. SADAKA.
Sadaka ni jambo jema sana katika maisha ya mwanake mkristo. Ni jambo ambalo linaubariki moyo wa Mungu. Hivyo katika kuulinda moyo wangu nimekuwa pia mtu wa kupenda kutoa sadaka. Neno la Mungu linasema katika kitabu cha Matendo ya Mitume kwamba, Kornelio alikuwa akiwapa watu wengi sadaka, na alikuwa akiomba Daima, hivyo unaona jinsi ambavyo malaika wa Bwana alimtokea katika maono wazi wazi. Na kumpa maelekezo. Hivyo ni vizuri sana kuhakikisha unakuwa mtu wa kutoa Sadaka , Na sadaka ninazozitoa nazitoa kwa mfumo ufuatao.
1. Fungu la kumi kwa maana ya kila ninachokipata kwenye kazi zangu.
2. Sadaka za kanisani sehemu ninapoamudu (michango nk)Utaratibu wa kanisa.
3. Sadaka za Kila jumapili ninapoingia ibadani nisiende mikono mitupu.
4. Sadaka za Shukrani, hii ni binafsi yangu ninapokuwa na jambo a kushukuru. Na hizi naweza kuzitoa katika namna nipendayo.
(i) Kupeleke kanisani ninapoabudu
(ii) Kupelekea kwa wahitaji nk.
5. Sadaka za wahitaji. Yatima, Wajane na Wasiojiweza. Nilijifunza kutoa kilo ya sukari kila mwezi mara moja kwa mhitaji, kisha mara mbili,kisha mara tatu,kisha mara nne. Kwa kadiri nitoavyo nikawa naongezwa na Yesu. Ikawa ni njia ambayo moyoni nakuwa na mambo mazuri tuu ya kufanya. Sina nafasi kujaza visivyo na faida.

6. Sadaka za Nadhiri. Kutoa nadhiri zangu ninazoweza kuziondoa.
7. Sadaka za msukumo. Kuna wakati Napata msukumo kutoa sadaka kwa mtu binafsi, mtumishi wa Mungu nk.
Sadaka hizi unaweza kuona ni nyingi sana lakini nikuambie tu natoa kwa moyo, sio lazima mamilioni ila natoa kwa moyo . Sadaka yenye heshima. Sadaka yenye kumgusa Mungu.

Hao ndio walinzi wangu ambao wananifanya kuulinda moyo wangu kuliko vyote nilindavyo. Na tangu nimeanza kujifunza hayo na ninaendelea kujifunza nimejikuta kwanza kuepukana na dhambi, kuna tabia mbaya na dhambi ambazo zilikuwa zinanisonga na nikawa mtumwa kwazo lakini leo najishangaa nimewezaje, ama kwa hakika UTUKUFU KWA JEHOVA MUNGU WA BWANA WETU YESU KRISTO.
Moyo wangu naulinda kwa namna hiyo. Hivyo mpenzi mtasomaji,unapoendelea kuburudika na kujifunza kupitia mkasa na ushuhuda huu nimeona mimi Irene Mbowe nikushirikishe kitu hichi cha kuulinda Moyo wako kuliko vyote ulindavyo kwa kuweka hao walinzi wan ne wazunguke kuta za Moyo wako,. Kuomba kwa kumaanidha kutakufanya uwe karibu na Mungu, kusoma neno hali kadhalika kutakutanya uache dhambi maana Biblia inaseme Neno la Mungu linaonya na kuadabisha. Hembu soma hili Andiko hapa kidogo uone,
2 TIMOTHEO 3: Kila andiko lenye pumzi ya Mungu lafaa kwa mafundisho, na kuwaonya watu makosa yao, ka kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki.
Unapokuwa mtu wa kusoma Neno la Mungu kwa kumaanisha unakuwa mlinzi wa Moyo wako sana kwa maana ya kupata ufahamu, ikiwa ni pamoja na KUJUA UMUHIMU NA UTHAMANI WA KUSAMEHE . Maana Biblia inasema je ni nini kitatutenga na upendo ulio katika Kristo Yesu? Je kutosamehe kutakutenga na upendo huuu??

lakini Mlinzi mwingine ni kuwa na watu sahihi,Waliojaa hekima na maarifa ya kimungu. watu ambao wamekomaa. unapokuwa na.changamoto unahitaji kuwa na watu waliokomaa. ambao watakushauri kabla ma baada ya changamoto. watu ambao watakuwa wanakuona na kukusaidia. haikuwa rahisi katika eneo hili .Kujitenga ama kutengwa na marafiki wasiofaa sio zoezi rahisi hata kidogo. ni zoezi lilouma sana. mnoo. lakini nikaanza kutengwa na marafiki wapotoshaji, wasiofaa.
Katika kuulinda moyo ni vyema sana kuwa na marafiki ama washauri bora na waliokomaa katika imani. hawa ni msaada mkubwa sana.
Ngoja nikuambie mwanamke kijana ambaye unanisoma katika ushuhuda ama mkasa huu. Kuna.gharama tunazikwepa lakini madhara yake yanatugharimu mara dufu. Hivi kuomba sasa hivi inakugharimu nini?Kusoma neno la Mungu sasa hivi inakugharimu nini? kumtolea Mungu sasahivi inakugharimu nini?Ama mpaka usikie toa upate utajiri ndio unakimbilia huko?Mwanamke kijana mchaji wa Mungu hayumbishwi na manabii feki. Ni mwanamke anayeishi kwa utaratibu mzuri katika maisha yake. ni mwanamke mwenye Ratiba endelevu maishani mwake. Ratiba nzuri za ibada zake , hababaishwi na nyakati. maana neno la Mungi liko ndani yake. Roho wa Mungu anamuongoza. Moyo wake unalindwa na umelindika sanaa.

sasa mama Naomi anaingia kwenye gharama hii ya kusamehe kwa sababu hajalinda moyo.
Kitanda kinakuwa kama kimemwagiwa maji. hapati usingizi kabisa.Kweli kaombewa,lakini sio mtu wa kujiombea. hajui aombe nini. ana hasira na uchungu ataombaje?
kujizoeza kuomba, kusoma neno la Mungu ni jambo zuri. kwani linakuwa ni sehemu ya maisha yako. hata Ukutane na changmoto gani hutaacha kuomba Mungu.
Katika hiyo changamoto yangu nilifamikiwa sana kuikabili kwa sababu Sikucha ratiba zangu za kuomba. Niliendelea kuomba na kufunga. na Kachangamoto nikakaona ni kadogo sanaa. na hata kalikopitia sikujua. lakini ni kwa sababu nilikuwa na walinzi hao. walinziwa kulinda moyo wangu.

Mama Naomi angepaswa tuu apige amagoti na kumwambia YESU Pigana wewe. nitetee nivike unajasiri katika hili.
Ninapokumbana na hali ambazo si swari huwa nakumbuka jambo moja la muhimu sana ,
YESU NISAIDIE NISIKUTENDE DHAMBI.
Maneno haya ni machache sana. Lakini huwa yana nguvu ya ajabu mnoo katika maisha yangu.
huwa najikuta kila kitu nakiona cha kipuuzi na kujikuta najiona mshindi na mqenye kupendwa na Yesu.
Mwanamke kijana nikushauri tuu ULINDE MOYO WAKO KULIKO VYOTE ULINDAVYO KAMA NENO LISEMAVYO.

Itaendelea sehemu ya 44..
Mahubiri yamekuwa mengi nimejukuta nina scroll down tu... Ila kazi nzuri pamoja na mambo mengine naona muandishi ameamua kuonyesha nguvu ya maombi katika mahusiano
 
Mahubiri yamekuwa mengi nimejukuta nina scroll down tu... Ila kazi nzuri pamoja na mambo mengine naona muandishi ameamua kuonyesha nguvu ya maombi katika mahusiano

Kwanini umeogopa kusoma maombi?
 
SEHEMU YA 42
Ujumbe wa Irene, mwandishi wa hii story.
View attachment 1150805
(Wadau kwa sababu nina C&P story hii nami naileta post ilivyo humu, sioni kama itakuwa vizuri nikiacha haya na kupost maandishi tu ya story. WANAWAKE OYEEEEE)
************************************
SEHEMU YA AROBAINI NA MBILI.
Nimekupa jini la kukulinda, hii sentensi ilikuwa haitoki akilini mwangu. Nimekupa jinni la kukulinda, Hivi jinni si ndio mashetani ama ni nini? Jini si ndio mapepo? Hivi mimi si ni mtoto wa Kikristo? Naanza kukosa amani, jinni, Lakini mbona kama ndio mlinzi huyu jinni? Nitamuuliza nani? Niko juu ya kitanda changu nimejilaza natafakari haya,. Kuna wakati nilikuwa nasikia watu wakisema kiti, sijui shetani wake hataki anywe pombe, shetani wake anataka nguo nyekundu, Lakini nikakumbuka miaka kadhaa wakati nasoma shule ya Sekondari kuna msichana tulisome naye ambaye alikuwa akisumbuliwa sana na majini, na alikuwa na rafiki yake ambaye alikuwa akimsomea maneno Fulani ili hayo majini yatutulie, Ilikuwa ni shule ambayo ni ya wasichana na wavulana msichana Yule alikuwa akianguka wasichana tu hatuwezi kumnyanyua ila mpaka waje na wavulana, na ilikuwa huyo rafiki yake akija anamshika sikio na kumwambia : acha kumsumbua kiti, acha kumpa shida kiti,, nakumbuka na msichana huyo mwenye jini alikuwa akitulia . Nilikumbuka haya.
Lakini nakumbuka tena siku moja tukiwa shuleni kwenye kipindi cha dini, Binti mmoja ambaye alikuwa kaokoa alikuwa akikemea sana mapepo, kuna wakati kulikuwa na wimbi kubwa sana la watoto kupagawa na mapepo na huyu msichana ambaye ameokoka alikuwa sasa kazi yake ni kukemea mapepo na kuyafukuza kwa Jina la Yesu wa Nazareti na hao walioombewa na kukemewa walipona japo walikuwa wakipata shida majini ama sijui ni mapepo ama mashetani hayo yakiwavaa. Sasa leo Napata jambo ambalo sijui ni majini ni mashetani ama ni mapepo, kwa nini isiwe ni Malaika? Niliwaza na kukosa jibu,, Nilisema potelea mbali ili mradi sio kitu kibaya potelea mbali.
Unajua Marino mimi ni mganga wa miaka mingi sana, si unaona hata lugha yangu imebadilika? Ninafahamu lugha nyingi sana, na ndio maana unaona nakusomea kwa lugha tofauti, usiogope hili jini litakutunza sana na mabaya hayatakupata kabisa . Kuna wanawake wanawekea dawa waume zao kuwalinda sasa nataka dawa zao kwako zigonge mwamba umesikia eee, hilo jini lako limetoka baharini,, na sisiwaganga huwa hatuwaaambii watu kama tunawapa majini, ila nimekuambia tu kwa sababu nakupenda ndio maana nimekuambia, ila kila mtu akienda kwa mganga hupewa jini lake, ukichanjwa , ukitoa sadaka za kuku, mbuzi, ng’ombe , unapewa jini, hatusemi ila ndivyo ilivyo, lakini wewe nimekuambia . usiogope. Hii ni risala ambayo nilikuwa naambiwa na mzee Palwa wakati ananifanyia dawa zake na kunisomea maneno ambayo nilikuwa sielewei mpaka aanze kuongea Kiswahili ndio naelewa. Ahaa, kwa hivyo hata mama Karisa ana majini eee,, nilijifariji, basi sio kitu kibaya. Nilijisemea.
Nilipitiwa na usingizi mzito sana kitandani, nilishtukia tu nimeamka na ile hali ya kusikia kizungu zungu ikawa inanirudia tena. Na niliambiwa nikisikia kizungu zungu niamke na kukoroga ile dawa na maji tu alafu nisemea “Salaaam mara 7” alafu ninywe. Nami nilitii hiyo hali, na hiyo dawa ni ya unga unga mweusi na mwekundu ukiweka kwenye maji inabadilika rangi haraka sana na kuwa kama juice Fulani hivi, ni chachu na tamu kwa umbali na hiyo dawa inauzwa elfu 40. Niliinunua na akaniambia ndio dawa yangu ya kutembea nayo,kila nikisikia kizungu zungu ninywe , ama nikiona mambo sio sawa nifanye hivyo. Basi nikaamka na kwenda kwenye pochi yangu na kutoa dawa na kuiweka kwenye glass na kusema Salaaam mara saba kisha nikainywa na nikajisikia ahuen na kurudi kulala.
Sijawasiliana na Fadhili muda, leo usiku nimemkumbuka sana, lakini nahitaji kumaliza masharti yah ii dawa kwanza kisha nitamtfuta, wacha siku mbili hizi ziishe alatu nitamfuta. Alininunulia gari ni lazima nimheshimu.
Nikiwa kitandani kabla sijapitiwa na usingizi najikuta nakumbuka maisha yangu ya ndoa, namkumbuka sana Baba Davis na wanangu. Dah, ama kweli maisha hubadilika, ila nikifanikiwa kupata biashara na kumkamata hasa Daniel nafuata watoto wangu, nimewakumbuka, ila sina pesa sina msichana nitawaleaje? Ngoja mambo yangu yakae sawa ngoja mambo yangu yakae sawa. ************************************************
Mama Naomi alimuelezea mkasa mzima Yule mwanamke kijana, Na alikuwa akilia sana wakati akimuelezea mkasa mzima. Na mwanamke kijana Yule alikuwa halii wala haonyeshi kusikitika , alimsikiliza kwa makini sana mama Naomi, na mwisho kabisa akaanza kuongea tena na mama Naomi.
Mama Naomi nisikilize, ni kweli umenieleza mkasa mzima, lakini ninakufahamu kitambo sana tangu umehamia hapa na mume wako, sisi majirani tumekuwa tukitamanai sana maisha mnayoishi na mume wako, mnapendana mnaelewana na mmekuwa watu wa mafanikio sana, Yani hatuachi kuwataja kwenye maongezi yetu tunapokutana, na kuna ambao tunakuonea wivu mzuri kwa maana ya kutanani na sisi waume zetu wawe kama wewe, lakini kuna ambao wanakuonea wivu mbaya na hili acha tu nikuambie, na ndio maana unaona nimekuja hapa. Yani kama kuna kitu kitafurahisha majirani hapa ni wewe kuacha hii ndoa, yani kila mtu atashangilia na kuna watu watafanya kabisa sherehe maana ni kama walikuwa wanasubiri siku tu itokee unashida wafurahie. Lakini sikufichi mimi ni mwanamke kama wewe nimepita kwenye changamoto mbali mbali kwenye ndoa na nikakomaa nazo na leo nina ndoa ambayo ina amani na furaha sana, yani haya unayopitia wewe mbona ni roho ya makasheshe yangu? Au umesahau mapito yangu? Inawezekana pengine hukumbuki kwa sababu haikuwa inakuhusu, lakini nakumbuka mara ya mwisho nilikuja kuwaomba mniongezee pesa ya kodi ya nyumba wakati tuliishiwa na pesa , umesahau?
Nimekumbuka nimekumbuka,, Mama Naomi ni kama alisahau mkasa wa mwanamke huyo, sasa kwa mbali kama kakumbuka.
Mh.. umekumbuka eee, unakumbuka mume wangu alivyokamatwa na Yule mwanamke mpaka na duka akamfungulia na akazaa naye? Unakumbuka nilivyokuwa nimekonda na kuchakaa? Unakumbuka lakini? Yani wala sitaki kukumbuka misri ila wacha tu nikukumbushe pengine itakusaidia leo. Mwanamke kijana huyo alifuta machozi yaliyokuwa yanatiririka machoni pake,,, na mama Naomi naye akaanza kulia tena. Sasa sikia, kama sio kusimama bila shaka leo hata ningekuwa nina kumbu kumbu ya makaburi ya wanangu. Si unakumbuka mume alihama kabisa na nilikuwa namuuguza Saimonii, si unakumbuka?
Ndio nimekumbuka, nimekumbua.
Sasa huoni kama unataka kuamkaribisha shetani ndani ya nyumba yako?hivi kama nisingesimama imara kuangalia watot o wangu unategemea nini? Hivi kama nisingesimama kumuangalia Yesu unafikiri ingekuwaje leo? Si ningekuwa naongea lugha zingine hapa mamaaa,, Mwanamke kijana Yule aliendelea kuonge a na mama Naomi kuhakikisha anamsikiliza n a kumuelewa.
Sikia, yani kama kuna kosa utafanya ni kumkaribisha shetani akutawale, na ninaona ni kama akili yako inaanz akuwehuka. Yani ukitulia n a ukimuomba Mungu mbona atakufunulia na utajua shida ilipo?
Mimi haikuwa rahisi lakini niliamua kutulia nakuanza kufanya maombi na kufunga na kutoa sadaka mpaka nikapata kujua tatizo lilipo. Umekuwa na ndoa nzuri sana, nimekuambia hivi,, wanawake wengine wanashika wanaume kwa mapenzi tu, yani wanakuwa ni ma alwatani wa mapenzi , akikaa na mumeo anamanyia michezo michezo ya mapenzi siku nzima, wanacheza wanataniana wanafanyia waume za watu mapenzi siku nzima wamajifungia hotelini ndio maana hata ulisikia hayo maneno ya Marino akimwambia mumeo na hizo msg za mapenzi, lakini kwani wewe huwezi mapenzi? Wewe sin i mwanamke? Kwani ukiamua kumfanyia mumeo mapenzi unafikiri huwezi? Hizo masaji mbona rahisi? Kukaa kimapenzi mbona rahisi? Sikia, usiachie kahaba mume wako, yani hata kama umemchoka mumeo aisee usimuachie kahaba mume , ni udhaifu wa hali ya juu na ni kulitukanisha Jina la Mungu, usiachie kahaba mumeo sawa mama,,, Mwanamke kijana alisisitiza.
Mapenzi unaweza, kama nishanga na wewe vaa, kama masaji na wewe fanya, kama kuongea vizuri na wewe unaweza kama kumtii mume na wee mtiii. Ili kama ni mapenzi kafuata ajikute ni marudio tu huko nje. Ama hujui dawa ya mtoto mlaku ni kumpa chakula ashibe? Mpe mumeo mapenzi, usimnunie, yani ukimnunnia umemrahishia huyo Marino Kahaba kufaulu sana. Mungu akusaidie jamani uweze, mimi niliweza, sikujua kama Yule mwanamke angekuja kuachwa, akanyang’anywa duka, akaachwa na kukutwa na mauchawi , haikuwa rahisi, lakini leo baba Saimonii unaona anavyonipenda na karibuni tunahamia kwetu mama yangu, yani acha, sikutegemea, miaka miwili nimelia mimi acha, lakini nilisema sitaachia kahaba mume wangu.
Lakini ngoja nikuambie kitu kingine, kuna mi wanawake huwa ina pesa na inashawishi waume zetu kuwa nayo, hata hilo limwanamke lilikuwaga na pesa likawa linampa mume wangu mpaka gari, lakini nikaja kujua, nikaanza kumuombea mume wangu sana Mungu ampe kazi nzuri na mafanikio, na kweli alifanikiwa kabla ile kampuni haijafilisika, si unakumbuka mume wangu naye alikuwa kwenye huo mzozo mpaka akapelekwaga mahakamani? Unakumbuka? Na lile li mwanamke ndio likamuacha? Unakumbuka? Lakini ningekuwa mwanamke mpumbavu ningeacha mume kwa vile ana kesi, lakini nilipat ufahamu kwamba atafukuzwa kazi, atakosa kazi na pesa na ndio utaakwua mlango wa kuachana na lile likahaba na kweli ikawa hivyo na ni kwenye maombi nilipata haya mambo nikiwa nimetulia hasa, na hata alipofukuzwa kazi unaona sikushtuka ndio maana ni lazima mke kuwa na kazi, kazi yako ipende, umesikia, usiharibu kazi yako hata kama mume ana kuudhi jikaze na komaa, penda watoto wako, nilisikia umewapeleka siju kwa Yule rafiki yako, yani story zako tunazo zootem mpaka umechukua pesa kwenye akaunti tunajua, sasa sijui kwa nini unaacha mambo yako yatapakae hivi, nimekuambia kuna watu wanaangoja tu uachane na mumeo wafanye sherehe. Sasa komaa wakomeshe mpenzi. Hembu muombe sana Mungu mama Naomi. Shika ndoayako . Huyo mwanaume wako mbona hata hajui umalaya, hivi unajua ndio anajifunza, tena muoga sana.
Lakini mama kuna wanawake wachawi hasa,Yani wakati ninapitia kwenye changamoto zangu ndio nilijua watu wachawi, nilifuatwa na wanawake wengi tu wakaniambia nikamtengeneze baba Saimoni, kwa sababu labda kafanyiwa dawa, yani sijui hata nikuambieje, ndio maana unaona nin a ujasiri wa kuongea na wewe nakutakia mema. Ila kama utanisikiliza utafaidi, lakini ukijidai kutosikia ushauri wangu yani utakuja kulia siku moja na utasema bora ningemsikiliza mama Saimonii. Kama hilo li dada ni lishawi aisee utashangaa, wewe kaa kizembe acha kumuombea mume wako utashangaa mauchawi mpaka na wewe yanakuvaa na watoto wako, yani huwa sijui wanawake wan je wanfanyaga nini, unakuta uko na mume wako mnapendana lakini ghafla unaanza maugomvi, mnachukiana, hakunahata hamu ya kufanya mapenzi, hakuna hamu ya kuongea pamoja yani ukiona hivyo ni maroho ya mafarakano, usikubali kabisa. Wewe komaa na maombi. Komaa na Maombi kila siku unakuwa mwanamke muombaji, usichoke kujiombea wewe, kuombea watoto wako, kuombea uchumi wako, na mumeo, kuombea afya zenu, yani hata siku moja usiache kufanya hivyo. Komaa na maombi mama Naomi, yani ukikomaa mbona ni rahisi sana ndoa yako kurudi?
Mwanamke kijana alimwaga ushauri mpaka mama Naomi akajikuta kasima kaka kwenye sofa. Na walipoangalia simu ya mezani ilikuwa ni saa nne usiku.
Asante sana mama Saimoni, asante sana.Umenisaidia sana.
Mama Saimoni mwanamke kijana alipiga simu na kumwambia shemeji yake awalete watoto wa mama Naomi na msichana nyumbani, yani awarudishe.
Baada ya muda walirudishwa na mama Saimoni akamwambia mama Naomi kwamba atakuwa akimsaidia kuomba pamoja kila siku jioni, watakuwa wanafanya maombi pamoja.
Asante sana, asante sana.
Na kabla hajaondoka alimwambia, uchukue simu, mtakie mumeo usiku mwema, usiache, ongea naye, mshukuru kwa pesa za matumizi alizoacha, yani makahaba hata wakipewa elfu moja wanashukuru sana. Hata kama ni wajibu wa mumeo kukupa pesa mshukuru tu kukupatia isiwe kama ni lazima kwake, kuwa na moyo wa kumshukuru na kumuombea. Yani mama Naomi nakuambia mambo ambayo mimi yamefanyika Baraka sana kwangu. Mume wangu alipofutwa kazi wengi walijua hatakaa apate tena kazi, na tutakuwa masikini wa kutupwa. Lakini maombi yana nguvu, maombi ni mtaji tosha. Unaapomba hujui unaweka nini mbele za Mungu. Nilikuwa naomba tu kwa kumaanisha. Sikujua kama mume wangu atakaa apate mradi mahali wa kufanya. Lakini imekuwa ni Neema ya ajabu. Mume wangu anapata makazi ya kujenga mahoteli makubwa , majengo makubwa, na anaaminika sana, ni kwa sababu nimeombea uchumi wake. Maana akifanikiwa na mimi nafanikiwa. Watoto wangu wanafanikiwa. Yani sio faida yake tu. Sasa wewe unaficha mpaka passport hivi unafikiri kupoteza kazi ni kitu kikubwa sana?huko anakoenda mmegombana ana mawazo, hivi unafikiri akili yake itatulia? Hembu usichanganye mambo kwenye maisha, kama tatizo ni yeye kuwa na tabia ya uzinzi angalia namna utakabiliana na uzinzi bila kuathiri maeneo mengine mfano kazi, maendeleo yenu, ama hujasoma maandiko yanasema Kahaba ni shimo refu na alalaye na mwanamke hana akili? Ama hujui mwanaume akiendekeza uzinzi anakuwa maskini? Amka mwanamke mwenzangu. Amka wao wakiloga sisi tunaomba. Umesikia?
Ndio nimesikia, nimesikia mama Saimonii, nimesikia.
Watoto waliingia ndani na mama Samioni aliwaita na kumwambia mama Naomi nataka sasa tuombe pamoja, omnba chochote wewe si mkristo si unajua kuomba? Hata kama hujui omba tu u Yesu anasikia.
Nataka uanze kujiombea mwenyewe, muombe Mungu akusamehe maana umemkosea sana umekuwa na hasira na visasi na matusi hembu omba msamaha kwa Yesu kwanza alafu tutaomba tena Yesu akupe neema ya kusamehe umesikia.
Tukimaliza tutaomba tena Yesu akusaidie kukuepushia balaa na mikosi yote kabisa ambayo shetani ameipanga juu yako. Ukiona mumeo anafuatwa maana yake ni wewe unatafutwa na wanao, si unajua maandiko yanasema uadui ni kati ya shetani na uzao wa mwanamke eee,. Sasa kinachotafutwa hapo ni uzao wako kupitia mumeo. Nataka usimpe shetani nafasi. Yani Yesu kunipa kibali cha kuingia kwako nataka kufanyika Baraka kwenye mji huuu, nataka Yesu afanye kitu kwa ajili ya familia hiii. Mwanamke kijana huyu alianza kutokwa na machozi, na akamshika mama Naomi mikono na kumuomba asimame ili waanze maombi.
Asante Yesu kunipa neema ya kuingia katika mji huu, nakushukuru mwana wa Mungu uliye hai, uliyenipa kibali YESU kukanyaga mahali hapa, Asante kwa sababu Yesu ulisema wakitupokea neema itakuwa pamoja nao. Asante Yesu kwa sababu unaenda kuonekana kwa namna ya ajabu na shetani hata pata nafasi kabisa kwenye mji huu. Tunakushuku kwa neema yako na upendo wako yakwamba hata leo tuna uhai wa kuweza kuliitia jina lako Yesu. Twende kwa nani na tumuite nani ? Tunakuita wee Yesu. Naomba utusaidie mwokozi, Ninamsogeza mama Naomi mikononi mwako Yesu, nakuomba umsamehe na kumtakasa na kumrehemu, muhurumie kabisa Yesu, usitazame dhambi zake Yesu, naomba umsamehe kwa jinsi alivyokukosea na kukengeuka, naomba umsaidie Yesu, msame na mtakase uovu wake wote, leo anapokiri kutubu makosa yake naomba umfanye kuwa mwana wako. Msadie Yesu, msamehe kwa yote aliyoyafanya. Ninaomba umtie Nguvu na ufahamu na maarifa ajue yeye ni mwana wako ni mtoto wako, wewe ni Mungu wake na Bwana kwake wewe ni muweza wa yote, mpe kujua hayo. Naomba itulize akili yake Yesu, ajue kuingia na kutoka katika kukabiliana nachangamoto hii mwokozi. Yeye ni mke na neno lako linasema mmwanamke mpumbavu atabomoa nyumba yake bali aliye na hekima ataijenga. Eee Yesu mwana wa Mungu uliye hai, ninaita sasa hekima, ufahamu maarifa ndan i ya mwanamke huyu, ninaomba Yesu mpe hekima, mpe maarifa mpe ufahamu Yesu . Usimuache mwenyewe wala peke yake mwokozi , usimuache apotee, usimuache aangamie mwokozi, usimuache. Nakushukuru kwa ajili ya maisha yake mfalme nakushukuru kwa sababu umemsamehe, umemtakasa na umemfanya awe mwanao. Nakushukuru mwana wa Mungu uliye hai Amen.
Mwanamke kijana huyu alikuwa akiomba na watu wote ndani walikuwa wamenyamaza na mama Naomi alikuwa akilia tu. Mwanake kijana alimtazama mama Naomi na kumwambia Yesu kakusamehe usiogope, anza upya usiogope. Sasa nataka Tuombe Baraka ndani yanyumba yako na kuvunja kila mipango mibaya ya Ibilisi shetani inayopangwa juu yako. Umesikia?
Ndio nimesikia, mama Naomi alikubali kwa huruma sana kwani ni kama alikuwa hana msaada na sasa kapata msaada.
Mama Naomi , maandiko yanasema hivi katika kitabu cha
Waefeso 6: 10 Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.
Sikia mama Naomi, kila kilicho cha hila kinatoka kwa shetani, katika ulimwengu wa giza mambo mabaya hutoka kwa shetani ikiwa ni pamoja na uzinzi, mafarakano na magomvi. Hivyo hii vita si ya kupigana kimwili, sio kutukana, sio kugombana sio kushtakiana sio kulalamika, ila ni vita ambayo inakutaka usimame Imara, uwe hodari, si unaona maandiko yanasema HATIMAYE MZIDI KUWA HODARI?Hata kama ulikuwa hodari sasa zidisha uhodari zidi kuwa hodari. Nataka kutumia mamlaka ya Jina la Yesu kufunga kila aina ya uharibifu uliopangwa juu yak o na Mwovu. Mungu wetu si wa machafuko bali wa Amani, kila chafuko linatoka kwa mwovu. Yani nakuambia hivi mama Naomi unisikilize na tuwe pamoja utashangaa ukuu wa Mungu.
Mama Saimonii alianza kumuabudu Mungu kwa kuimba pambio moja linasema,,
Baaabaaa nainua macho yanguuu,,, nikitazama ni wewe tuu haleluyaaa…
Kwa sababu wote walikuwa ni wakristo wa dhehebu moja ilikuwa ni raisi kuufahamu huo wimbo na waliimba pamoja.
Alirudia kuimba zaidi ya mara tano,, na ndipo akaanza tena Maombi.
Wakati huo mama Naomi alikuwa analia tuu kwa uchungu sana.
Na watoto wakiwa kimya wakimshangaa mama Saimonii akiomba,.
Yesu , ninainua macho yangu juu nikitazama ni wewe tu ambaye unaweza kuokoa, kuonya na kurejesha amani katika mji huu. Yesu ninakuja mbele zako kwani neno lako linasema katika kitabu cha Matendo 4: 12 Kwa maana hapana jina jingine tulilopewa wanadamu litupasalo kuokolewa kwalo zaidi ya jina la Yesu. Yesu natumia mamlaka ya jina lako na damu yako Takakatifu kuifunika nyumba hii kuanzia sasa, lolote lililopangwa na mwovu lisipate nafasi wala mpenyo kabisa kwa damu ya Yesu, ninatumia mamkala ya jina la Yesu kufunga kila mlango ulio wazi kuingiza balaa, misiba mikosi kwa jina la Yesu wa Nazareti, hali zozote mbaya nazikataa sasa kwa damu ya Yesu kristo wa Nazareti. Yesu neno lako linasema wako malaika wale walinzi ambao hufanya kitu kuwalinda wakuchao sawa saw a na neno lako katika Zaburi 34: 7 Yesu nakuomba malaika hao sasa wakafanye kitu kuilinda familia hii, kumlinda mama huyu na mji wake wote, Yesu naomba usiwaache wala kuwapungukia, naomba ulinzi juu yao, juu ya mama huyu, juu ya mume wake, juu ya watoto wao, juu ya afya zao, juu ya kazi na uchumi wao. Yesu jina lako lina nguvu na umesema tuombe na unasikia, Yesu umesema yote tuombayo kwa jina lako tuamini yamekuwa yetu, Yesu kuanzia sasa ninaamini ya kwamba yote tuliyokuomba yamekuwa yetu. Katika jina lako Takatifu mwana wa Mungu uliye hai tumeomba na kushukuru kwa kuamini ya kwamba yamekuwa yetu Amina.
Mwanakme kijana alimaliza kuomba na kisha kuwashika wote mkono huku akitamka Baraka juu yao alianza kumshika mama Naomi mkono na kumwambia,, Yesu akufunike na kukuimarisha usitikisike kwamwe uwe imara.. Mama Naomi aliitika na kusema amina. Kisha kammshika msichana wa kazi na kumwambia, Fanyika Baraka katika mji huu kama mjakazi aliyefanyika Baraka enzi za Naamani.. Mjakazi akasema amina. Kisha akawashika watoto na kuwaombe, Yesu akulinde Naomi,akufunike kwa damu yake takatifu. Akamshika na Ruth na akamkumbatia Yesu akulinde Ruth mabaya yoyote yanayopangwa juu yako kuanzia sasa hayana tena nafasi kwa jina la Yesu. Kisha akamshika shemeji yake mkono na kumtakia Baraka, Yesu akubariki kuwa mtii hata katika utumishi huu, hakika Bwana atakulipa usipozimia moyo. Kisha mwanamke kijana Yule akajikuta ameanguka chini na kuanza kulia kwamzigo huku akimshukuru Mungu na hapo alikuwa sasa ainena kwa lunga kwa namba ambayo hakuna hata mmoja ambaye angeweza kumsikia na kumuelewa walisikia tu akiongea lugha ngeni kwao na mwanamke huyo alitumia kama roho saa na kisha akasimama na kumkumbatia mama Naomi na kumuaga. Mama Naomi machozi ya furaha yalikuwa yakitiririka na kusema asante mama Saimoni, asante sana sikuwahi kuwaza uko hivi, asante mama saimoni , asante sana, sitasmani hata uondoke, natamani tukae pamoja tu usiku wote huu, asante sana.
Mama Saimoni mwanamke kijana aliondoka na kuwaacha na kurejea nyumbani kwake akisindikizwa na shemeji yake.
ITAENDELEA SEHEMU YA AROBAINI NA TATU.
KARIBU TUNAMALIZA, BADO SEHEMU 7 TUMALIZE TUMMA MUAMALA CHAP CHAP KWA 0655 030211 AMA 0754357118
Kumbuka sadaka yako hii infanyika Baraka kwa sababu nina safari za mikoani kuzindua maombi yaNaipenda jumamosi yangu kwa lengo la kumjenga mwanamke wa kitanzania kuwa muombaji daima. Kujiombea binafsi, ndoa, mume ,watoto, afya, uchumi na taifa lake. Asanteni.
INAENDELEA SEHEMU YA 43
post # 1179
hatimaye mama Naomi bangi aloyokua amevuta imeisha makali
 
Mmmmmmh!!!
Unajua ulichoandika au umekurupukia ndotoni? Ungekuwa unajua kufikiria hata nje ya boksi husingeandika upupwu wako huu.. nipanic napata nini kwa ya humu!!!!!!!!
Wivu.com
Siku ingine tumia ID unayotumia kizaidi kubwabwaja humu.
Sasa Mbona unazidi kupanic.. Relax dada.
 
Wanawake wengi hawajui kuwa MUME HAFOKEWI...hata hao waombaji wazuri hapo kabla walikuwa wafokaji wazuri ti Kwa waume zao... AKINA MAMA D, MAMA NAOMI ..ETC WA HUMU JF JIFUNZENI MAPEMA KUWA MUME HAFOKEWI.... usingoje Hadi umdhalilishe "DANIEL" wako Kwa majirani zako ndo ubadirike...!!! Achana na marafiki ambao USHAURI NAMBA MOJA KWAO NI KUMKIMBIA MUME...!!!! ONA MARINO ALIPO, SASA KAWA MLOZI... ONA MAMA NAOMI ALIVYOSHAURIWA...!!!?

Acheni roho za kushindana na waume zenu....
sawa tumekusikia tuta jaribu :D
 
FB_IMG_1562871255677.jpg



SEHEMU YA AROBAINI NA NNE
Panakucha mama Naomi akiwa kalegea kila mahali, hajui hata aanzie wapi. Anachukua simuyake na kupiga ofisini anapofanyia kazi. Anaomba ruhusa kwaba ana dharura hataweza kwenda kazini, Anajisikia kichwa kinauma, hana raha wala furaha . Hajui hata afanye nini.
Ni saa kumi na moja asbh ameamka na kuanza kupiga hizo simu kwa wafanyakazi wenzake. Saa kumi na mbili bado yuko kitandani si kama kapumzika la hasha, ni mawazo yamejaa akilini kwake. Nifanyeje akili yake inaanza kukusaka wanawake ambao wamepitia changamoto na anamkumbuka wamama wengi tu ambao wameamua kuishi maisha yao, kivyao vyao ni kama wanawake sita hivi kwa haraka haraka, wengi ni wale ambao wanasema kuna ukimwi, sitaki kufa na ukimwi, sitaki. Na anaona ukimwi huu hapa,,hivi huu ujinga nani aubebe? Hivi nikifa na ukimwi hapa nitasema nini? Hivi huyu Marino ana mume mmoja tu? Hivi si atakuwa jalala la wanaume huyu? Sifi na ukimwi na sitaki ujinga.. Sitaki upuuzi,, mfyu. Anafyonza kwa nguvu. Kisha anaendelea kufikiri, na anamkumbuka mama Saimoniii, akili yake inatulia sasa anaanza kumtafakari mama Saimonii,, anajiuliza mengi akilini mama Saimonii kawezaje kuishi na mumewe na mumewe alimkosea sana? Kawezaje? Ngoja niongee naye aje anisaidie tu kuhusu ukimwi aje tu. Maana siku tayari kufa na ukimwi siko tayari.
Mama Naomi anampigia simu mama Saimoni na kumuomba afike amsaidie jambo. Mama Saimoni anapokea simu na kumpa taarifa kwamba amekimbia kwenye biashara zake tayari, ni saa kumi na mbili asubuhi mwanamke huyo tayari kashakimbilia biashara zake. Mama Saimoni ana kmgahawa ambao ni yeye peke yake anakisimamia. Hivyo ni lazima awepo kwenye biashara yake hiyo kuanzia saa kumi na mbili asubuhi ili kuwahi wateja wa chai asubuhi na mtori kisha chakula cha mchana na ikifika jioni afunge. Mama Naomi, nikitoka kazini na wewe ukitoka kazini tuwasiliane sawa? Mama Saimoni alimpa maelezo hayo;.
Siendi kazini niko tu nyumbani nimepumzika.. mama Naomi alimmjibu. Mama Naomi jamani, cha kukufanya usiende kazini ni nin sasa? Hembu amka, oga, jiandae nenda kazini, na Yesu akungulie, sikia mama yangu kukaa hakupunguzi kosa, ila kufanya kazi kunapunguza kosa kwa sababu bado unaenda kazini haijalishi una changamoto gani, hembu nenda kazini mamii, amka oga nenda kazini.
Maneno ya mama Saimoni yanamtia moyo mama Naomi na anajikuta anajiandaa haraka na kuondoka kuelekea kazini kwake. Mama Naomi anafika kazini akiwa yuko na mawazo lakini anapofika pale pilika pilika za kazini zinampa kuwa busy na mara jioni hii hapa imeingia. Anamigia mama Saimoni simu na mama Saimoni anamwambia wakutane nyumbani jioni.
Ili waweze kuongea na kutiana moyo tena. Mama Naomi walau sasa ana mahali pa kupumulia, mahali ambapo panampa mwanga, japo ana maswali mengi kichwani kwake juu ya changamoto yake lakini walau kidogo ana mtu wa kumuuliza.
Jioni inafika, na wanakutana nyumbani kwa mama Naomi ili waongee, na swali kubwa la mama Naomi ni je atajikingaje na ukimwi kwa mwanaume ambaye ni mzembe kiasi hicho? Na ambaye hajali kulala na wanawake?
Sikia mama Naomi, yani kama kuna watu wenye bahati ni wanawake ambao wanajua ubaya wa waume zao na uzinzi wao, kuliko mwanamke ambaye mume ni mzinzi na hajui. Hivi ambaye hajui hapati ukimwi? Hivi kama usingejua usingepata ukimwi? Si bora umejua mume ana tabia za uzinzi hivyo, kwanza unaweza kumuonya, unaweza kutumia kondom ama la unaweza kumuombea. Hivyo ni bora umejua tabia zake mbaya za uzinzi alizo nazo ili sasa ufanye maamuzi sahihi katika kumsaidia kwenye kumshauri, kumuonya ama kumuadabisha. Ni mume wako,ongea naye. Mueleze namna ambavyo amekosea, msaidie, kwa sababu swala la mtu kuwa muaminifu ni swala la mtu binafsi, unaweza usione, usijue wala kuhisi kwamba mume ni mzinzi lakini akawa mzinzi wa kutupwa na kujificha sana, na akikutana na magonjwa ukayakwaa nab ado watu wakashangaa mbona walikwua wakiambatana na kuwa karibu hivyo ukimwi wametoa wapi? Na ndio maana nataka kukusaidia kwamba katika maisha tuliyo nayo haya , ni bora kuwa na tegemeo ambalo ni Yesu peke yake, Yesu akufiche kwenye mbawa zake, ndio maana nataka uanze kujifunza kuisha maombi na kuishi kumpendeza Mungu ili sasa yale mambo ambayo akili zetu hayawezi Yesu pekee aingilie kati. Sijui kama unanielewa?
Mama Naomi alitulia kidogo kisha akamtazama mama Saimoni na kumwambia kwa hivyo unataka kuniambia ujue mume ni mzinzi na uendelee kuishi naye?
Mama Saimoni alitabasamu na kumwambia mama Naomi, uitakaje mpenzi? Ulitaka nikuambie achana naye? Kamwe siwezi kukuambia achana na mumeo, lakini ninachoweza kukuambia ni kwamba uwe na akili ya kujua na kuweza kupambanua mambo .Jua mumeo uzinzi anaufanya kwa sababu zipi, ukishajua hilo ni rahisi kutatua tatizo na tatizo kupata majibu. Ndio maana nakuambia huyo ni mumeo, kaa naye ongea naye msaidie yamkini kakamatika mahali. Hujiulizi imekuwaje hakuwa mzinzi na leo kaanza matabia mpaka ya kulala nje? Wewe kama mke na kama mlinzi hujui kazi yako ni nini? Hivi unajua anguko na angamizo la mumeo linakudhuru hata wewe? Ama hujui hilo? Na ukiona mume kafuatwa jua anayetafutwa ni wewe na wanao tu basi na si vinginevyo na ukiachia mlango wazi ukasahau wewe ni mlinzi kama maandiko yanavyosema mwanamke atamlinda mumewe aisee anguko linalotokea siwezi kuuelezea. Biblia ilipomuita mwaname mjenzi ilijua kabisa ni mwanamke ambaye anaweza kujenga, ni Injinia na sio saidia fundi hapana ni Injinia hasa. Sasa kazi ni kwako ndoa yako ni kama gorofa angalia wapi ufa ukiwa mkukbwa utaleta madhara , na ndio maana nataka kabla hujaanza kupaka rangi anza kufanya plambing, weka pipe za kupitisha nyaya za umeme umesikia mamii? Alafu rangi inakuja baadae ukiwa umeshapitisha nyaya zako ndani ya kuta, wewe ni mjenzi. Ninachoweza kukuambia wewe ni mjenzi. Usikubali kujenga mjengo wako kizembe. Hembu inuka na anza sasa. Hakuna fundi ama mjenzi ambaye hana makovu, haumii, hana sugu. Kila mjenzi , kila fundi ambaye anajenga ni lazima awe anakwaruzika, anatobolewa na misumari, anaanguka, anachafuka, lakini mwisho wa siku ukiangalia mjengo aliojenga fundi huyo lazima ukuvutie sana. Amka, inuka, simamia ndoa yako mami simama kidete ili Jina la Mungu lisitukanwe. Mama Saimoni alimueleza mama Naomi maneno hayo, na Mama Naomi alionekana kuelewa, Alichukua simu yake ambayo ilikuwa kwenye chaja, na kutafut a namba ya mume wake na kisha akamwambia mama Saimoni,,
Mama Saimoni kwa hivyo natakiwa kumsamehe sio? Mama Saimoni alicheka akasema hivi kumbe bado hujatangaza msamaha mpaka sasa?
Hembu kwanza muandikie ujumbe mmoja, Mwambie tu unamsalimia kisha mwambie umemsamehe.
Mama Naomi aliuliza naandikaje? Mama Saimoni aimmwambia msalimie, mshukuru kukupatia pesa za matumizi, muombe msamaha kwa kukwaruzana, kisha mjulishe umejua amezini na Marino na umtangazie msameha. Na usiache kumwambia unampenda, umesikia,, Mama Saimoni alimaliza kisha akatabasamu na kufuata picha moja ambayo alikuwa amepiga mama Naomi na mumewe wakiwa wanatabasamu, akawa anaiangalia, huku nako Mama Naomi alichukua simu yake na kumuandikia mume wake ujumbe. Ufuatao baada ya kupata maelekezo kutoka kwa mama Saimoni.
Habari baba Naomi, bila shaka umefika salama, Sisi na watoto hatujambo tunaendelea vizuri. Asante kwa pesa za matumizi ulizotuachia. Unaendeleaje wewe? Jana ulipoondoka nyumbani tulipishana na kukwaruzana, ninaomba unisamehe,. Nimekusamehe pia kwa kugundua umezini na Marino. Nimekusamehe. Nakupenda , Uwe na amani jioni njema.
Baada ya mama Naomi kumaliza kuandika, mama Saimoni alimwambia Mama Naoami aliisome ile meseji kwa nguvu, Mama Naomi aliisoma huku akilia machozi, alilia sana, Mama Saimoni alimwambia , sikia, kuna mambo katika ndoa yangu nilikuwa nayafanya kama ujinga Fulani hivi, lakini yalifanyika nguvu na Baraka, unajua katika maneno kuna nguvu, hembu sema tu maneno yoyote juu ya huo ujumbe ambao unautuma kisha utume. Yani uombee huo ujumbe. kabla ya kuituma Hiyo meseji. Mama Saimoni alimwambia mama Naomi hivyo, kisha mama Naomi akiwa kashikilia simu akasema, Eee Mungu mimi siwezi mambo ya maugomvi, siwezi hizi aibu naomba msaidie huyu mwanaume aache uzinzi Yesu, mama Naomi alikuwa akilia, Mama Saimoni alimtazama akilia na kumwambia nipe hiyo simu nitumie mamlaka ya Jina la Yesu, nipe hiyo simu, nilikuwambia jana kwamba HAPANA JINA LINGINE TULILOPEWA WANADAMU LITUPASALO KUOKOLEWA KWALO , JINA LA YESU LINA NGUVU SANA HEMBU NIPE MAANA HII VITA KWANGU NI YA KITOTO SANA, NIPE HIYO SIMU. Mama Naomi alimshangaa sana mama Saimoni alivyokuwa na ujasiri wa kujivunia jina la Yesu.
Mama Saimoni alishika ile simu na Kusema, ee Yesu, umesema katika kitabu chako kwamba, lolote tuliombalo tuamini limekuwa letu, Yesu ninatumia jina lako takatifu sasa kuomba ufahamu katika akili ya baba Naomi, ajue kwamba kuwa na mahusiano nje ya ndoa yake ni dhambi,Yesu naomba fungua ufahamu wa baba Naomi mara atakaposoma ujumbe huu, ajue kwamba amemkosea mke wake, lakini ajue kwamba amekukosea wewe zaidi na pia Yesu naomba mfungue ajue kwamba uzinzi ni dhambi. Yesu nashukuru kwa sababu ujumbe huu unaenda kufanyika Baraka na ufahamu kwenye akili ya baba Naomi ameni. Mama Naomi haya tuma mama yangu ujumbe wako, Mama Naomi alipokea simu na kutuma ule ujumbe, kisha akatulia kusubiri majibu. Sikia mama yangu naomba nikuache, kuna kazi naenda kuuifanya nyumbani. Nina muda mrefu sijakagua mashati ya baba Saimoni kama yana vishikizo ama la, nataka kwenda kukagua walau mashati machache niyawekee vifungo kuna ambayo niliona hayana vifungo. Mama Saimoni alimuaga mama Naomi ambaye alikuwa akiendelea kumshangaa mama Saimoni. Mama Saimoni alitoka akaondoka zake.
***********************************************************
Siku ya kwanza imepita tayari, Marino hajawasiliana na Daniel, Daniel alimtafuta sana kwenye namba yake, kisha alipiga simu hotelini na akaambwia kwamba ile mizigo kuna mwanamke ambaye alienda kuichukua, na mwanamke huyo ni Marino mwanamke ambaye alikuwa amelala naye hotelini hapo. Alipopata taarifa hizo aliendelea kumtafuta sana Marino bila mafanikio yoyote. Daniel akiwa chumbani kwake amepumzika baada ya kazi kubwa siku hiyo ambayo kampuni ilimtaka kufanya, alichukua simu yake na kuandika jumbe kama tatu za mapenzi kumtumia Marino. Na akiwa katika kuandika ndipo sasa ujumbe unaingia, ni ujumbe kutoka kwa mke wake. Anausoma, nan i kama haamini anachokisoma. Kwa siku chache alizokumbana na mkasa wa mkewe kujua amelal ana Marino alikuwa akichezea matusi makubwa makubwa sana, matusi ambayo yalikuwa yanamuuma moyoni, ni kweli kakosea lakini aina yamatusi aliyokuwa akiyapata alihisi mke wake kapagawa. Leo anasoma ujumbe wenye utulivu kiasi hichi, Anarudia mara ya pili nay a atatu, anarudia mara ya nne. Kisha anaamua kusoma kwa nguvu akiwa chumbani kama ambaye ameambiwa amsomoee mtu ili asikie.
“Habari baba Naomi, bila shaka umefika salama, Sisi na watoto hatujambo tunaendelea vizuri. Asante kwa pesa za matumizi ulizotuachia. Unaendeleaje wewe? Jana ulipoondoka nyumbani tulipishana na kukwaruzana, ninaomba unisamehe,. Nimekusamehe pia kwa kugundua umezini na Marino. Nimekusamehe. Uwe na amani jioni njema.”
Baba Naomi ni kama haamini, anavua miwani yake, anafikicha macho yake, anashika simu yake na kutoka chumbani na kuelekea kwenye kisebule kiilichop chumbani kwake, anasoma tena ule ujumbe. Nini kimetokea, ni mama Naomi huyu ama. Baba Naoni ajishika kidevu chake na kukkikuna kama ambaye anatafakari kwa njia hiyo,, anaachia tabasamu kisha anaketi kwenye sofa. Akiwa ameshikilia simu yake anajiuliza, ajibu kwa ujumbe ama apige, lakini ajibu nini? “NIMEKUSAMEHE PIA KWA KUGUNDUA UMEZINI NA MARINO” kaujumbe haka kafupi sana kanamfanya sasa anajisikia aibu kubwa mno, siku zote katika malumbano yao hakuwahi kuona hili kosa, lakini leo ujumbe mfupi sana umemuelezea makosa yake yooote, Anasikia aibu, anasikia kujua amekosea sana, Nimpigie simu? Nimuombe msamaha? Nimwambieje? Baba Naomi alikuwa akitafakari afanyeje,, je nikane sijazini? Mbona inajieleza kila kitu? Hivi kweli amenisamehe ama kuna kitu anataka kufanya malipizi? Hivi kweli ananipenda ama ni kunisanifu? Anawezaje kujua nimemkosea kikubwa hivi alafu asema ananipenda? Daniel alikosa amani, alikosa amani, Alichukua simu yake na kuandika ujumbe,,, ASANTE MKE WANGU KUNISAMEHE, ASANTE SANA. NASHUKURU, NAKUPENDA PIA.
Alimtumia mkewe ujumbe huo huku moyo wake ukiwa na huzuni sana na alikuwa akiklia ndani kwa ndani japo machozi yalikuwa hayatoki nje. Mama Naomi alipoona simuyake imeingiza ujumbe alisoma ule ujumbe na mara moja alimpigia mama Saimoni simu na kumwambia mumewe kamjibu na akamsomea ujumbe ule ,
Safi sana, Asante Yesu, nimefurahi amejibu,mwanzo mzuri, hongera umejibiwa, lazima ameelewa ameelewa. Mama Saimoni alimpongeza mama Naomi. Sasa nimjibu? Nimjibu nini? Mama Naomi ni kama alikuwa anataka maelekezo kwa mama Saimoni. Mama Saimoni alicheka ha ha ha,, unanichekesha kweil mamii mumeo huyo,, jana nilikuambia jua mapenzi, jua kuuongea vizuri, maneno mazuri ni afya hivi husomagi maandiko mamii? Kuna nguvu ya ajabu katika kinywa chako, hasa wewe kama mwanamke jifunze kinywa chako kuwa na afya ili uponye na wengine umesikia mamii, Yani mbona nina kazi? Wacha nije kukufunda, yani nije kabisa kukufunda ama nikupeleke kwa Kungwi lao ukafundwe. Kungwi lao, kufundwa? Mama Saimoni aliongea kwa mfululizo mpaka akamchanganya mama Naomi, mama Naomi akawaza, Huyu mara maombi, mara kungwilao, mh,, mama Naomi kama anapata kujiuliza, ukungwi tena, mambo ya Kiswahili? Mbona huyu mama anaomba vizuri sana? Mbona kaokoka huyu mama? Sasa kungwi tena? Mh.. Mama Naomi anawaza. Mbona kimya? Mama Saimoni anamuuliza mama Naomi baada ya kuona kanyamaza kama sekunde kumi hivi.. Hapana, niko sawa, niambie nimjibuje? Nisaidie tu dada yangu maana akili hii sio yangu, yani sio kabisa, nisadie..Nisaidie tu. Mama Saimoni akamwambia, una Biblia hapo karibu? Ndio mama Naomi akajibu na kwenda kuifuata Biblia sebuleni kwenye shelfu za vitabu,, ninayo mamii niambie.
Hembu andika hii milango alafu utaisoma pole pole nataka ujue nguvu ya maneno yako mdomoni katika kuongea na mumeo. Uone maneno yalivyo na nguvu, sitaki uwe na maneno ya matusi ama kashfa, nataka uwe na maneno machache ambayo ni afya,
Umepata kalamu? Mama Saimoni alimuuliza, ndio nimepata mama Naomi alijibu,, oky haya anza kuandika mamii.
Fungua Mithali 18: 20-21, Yeremia 1: 8 -10, Zaburi 34: 12- 13,Mithali 15: 30, Mithali 16; 24,Mithali 25:11,12, 15 Mithali 31: 26. Mama Saimoni alimtajia mama Naomi hayo maandiko kwa kasi ya ajabu, huku mama Naomi akimwambia pole pole, Naalipomaliza alimwambia umemamaliza kuandika ama nirudie? Rudia, nimemaliza ila rudia nihakikishe,, Mama Naomi alimuomba mama Saimoni arudie ile mistari ili aiandike kwa usahihi, na mama Naomi alirudia na kuandika kwa usahihi, japo ni mistari michache tu alikosea, huo wa Yeremia aliandika mithali badala ya Yeremia.
Sawa sawa, naomba usome ukiwa umetulia alafu kama hutaelewa basi nitakuja kukuelewesha kesho nikotoka kazini, nina tenda ya kupikia wafanyakazi kiwandani wana sherehe, hivyo nikitoka jioni kama nitakuwa sijachoka nitapitia nikufafanulie, wewe soma tu umesikia? Mama Saimoni alimsisitiza mama Naomi asome . Sawa nimesikia. Mama Naomi alichukua Biblia yake na kuanza kusoma mstari mmoja baada ya mwingine, aliambiwa juu ya nguvu ya Maneno na ulimi wake. Alianza kujikuta akisoma maandiko matakatifu kwa kumaanisha, ni kweli huwa anaenda kanisani lakini biblia ataishika jumapili kwa jumapili tu, Biblia yake bado mpya sana, haiguswi wala kusumbuliwa n i siku za jumapili ataibeba na wakati mwingine wala habebi anatumia simu yake kusoma maandiko matakatifu. Hivyo Leo ni kama anapasa kazi ya kuanza kufungua Biblia kwamara ya kwanza kwa kumaanisha baada ya kufanya hivyo miaka mingi kidogo. Anakaa sebuleni kwenye meza ya chakula huku akifungua mandiko yale na kuyasoma. Andiko la kwanza alilofungua lilisema, “Mauti na uzima viko katika uwezo wa ulimi, na wao waupendao watakula matunda yake, Kisha akasoma andiko lililofuata, Akafungua kitabu cha Yeremia, 1 mstari wa 8mpaka wa 10, Akalisoma pole pole, alipomaliza kusoma akarudia tena, ni kama anaelewa sasa, akatulia na kurudia tena, Neno hili mbona kama linakuja kwake kama Unabii,, ameambiwa asiogope, na mama Saimoni kamambia ulimi wake unanguvu,, mama Naomi alitulia, akachukua simu yake iliampigie mama Saimoni,, Akapiga namba za mama Saimoni, Mama Saimoni akapokea na kumwambia, kuna kazi anafanya amekamatika . na watongea kesho. Mama Naomi neno hili limeushika moyo wake sana, Anaendelea kusoma mistari mingine yote na anaangalia saa yake ni muda wa kulala yani hata hajaoga, wala hajala , watoto walikula na wameenda kulala, Aliamka na kwenda vyumbani kuangalia watoto wake na kisha kurudi chumbani kwake na kuingia bafuni na kuoga. Ni saa sita kamili ndipo anajitupa kitandani baada yakunywa glass ya maziwa na vipande viwili vya mkate, jana yake hakulala , juzi yake hali kadhalika, na leo ni saa sita usiku, Anachukua simu yake anajiuliza atume ujumbe kwa mume wake ama alale tu? Anaamua kulala tu asije akajikuta analikoroga maana anajijua kwa maneno yake mabaya , yamkini akakosea hivyo alisema anasubiri mwailmu wake ama kungwi wake amsaidie nini cha kufanya. Anajibwaga kitandani na usingizi msito hasa unampata.
*********************************************
Waooo, siku mbili nimefanikiwa kabis kufuata masharti, sijatoka ndani kabis, sijawasiliana na mtu kabisa, safi sana, Nilisimama na kwenda kuangalia pete yangu nilipokuwa nimeiweka,, waoooo, niichukua na kusema maneno ambayo niliambiwa niyaseme, kisha nikanywa na ile dawa ambayo niliambiwa ninywe huku nikisema maneno yale kwenye ile pete, kisha nikaivaa kidoleni kwangu na kusema mimi na Daniel daima tusiachane, anisikilize mimi tu. Anipende mimi tu. Nilimaliza kuongea na kuitoa ile pete na kuiacha kidoleni kwangu. Niliamini sasa nimeshakuwa msindi, ni siku sijaongea na Fadhili, sina haja naye, nina haja na Daniel, ni asbh sana nilichukua simu yangu na kumpigia Daniel , Daniel alipokea, na alikuwa down sana,, mambo Daniel? Salama kabisa Marino, nimekutafuta sana, mbona hupokei simu zangu?Daniel alimhoji Marino.
Samahani sana mpenzi, nimekuwa na pilika pilika, nikasema nimalize kisha niwe na wewe full full kama hivi,, sasa yani vitu vyote vilivyokuwa vinanisumbua nimevimaliza mpenzi wangu nakusikiliza wewe tu na hata kama unataka nije Uganda nakuja mpenzi. Nilimueleza Daniel kwa furaha zoote, nikijua nimeshamkomesha na kwangu hafurukuti. Weee,, unaweza kuja Uganda? Daniel ni kama alipagwa aliposikia nimemuambia kuhusu kwenda Uganda,,
Ndio naweza, wewe ni mpenzi wangu, sina mpenzi mwingine kwa nini nisije? Niambie tu kama unanihitaji niko kwa ajili yako, niambie tu mpenzi. Daniel kusikia hivyo akaniambia basi sawa, Naomba nitoke kwenye kikao mchana kisha nikujibu. Sawa mpenzi? Sawa niilimjibu, tena nikuletee na Pete yako maananaona inazua ugomvi,, Na mimi sitaki ikuletee ugomvi na mke wako. Nilipiga picha nyingi sana kwa kutummia simu yangu mpya niliyonunuliwa na Daniel, simu inayotoa picha vizuri sana, na kumtumia Daniel picha nyingi sana, zingine nikiwa na khanga tu, ili kumpagawisha, ninajua yuko peke yake, hivyo nikimpagawisha kisha nikimwambia naomba kwenda nilijua hawezi kamwe kunikatalia, na kuku nimeweka picha zaangu kwenye profile yaw hats app za kutosha huku vidole vyangu vya mikoni vikiwa na kucha za kubandika na rangi nzuri ya kucha tunaita rangi ya jeli. Na zile pete kuonekana vyema.
Marino alipiga picha nyingi sana za selfie huku ile pete ikiwa kenye kidole chake, na zile zake zikiwa kidoleni pia, kiasi kwamba kama Mama Naomi akiwa mchunguzi na mpekuzi lazima ataiona ile pete ya Daniel yaani mumewe kwenye kidole cha Marino.


Inaendelea sehemu ya Arobaini na tano.
Post #1432
 

Similar Discussions

8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom